Afya ni inajumuisha utimamu wa kiakili, kimwili na ustawi wa jamii, na ni nyenzo muhimu kuhakikisha uwepo wa nguvu kazi itakayosaidia katika maendeleo au mapinduzi ta kiuchumi. Nchini Tanzania sekta ya Afya inakumbwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa vifaa tiba na wataalamu katika idara mbalimbali zinazohusisha afya kiujumla.
Kwa hiyo serikali kupitia wizara ya afya, mashirika yasiyo ya kiserikali na wadau mbalimbali hazina budi kuhakikisha uwepo au uanzishwaji wa Mbinu sahihi za molekuli ya baiolojia zijumuishazo matumizi ya sayansi na teknolojia ya Hali ya juu, Mbinu hizi ni mahususi na imara katika kupata suluhisho dhidi ya majanga ya Dunia mfano Ugonjwa wa virusi vya korona , na magonjwa mbalimbali yanayoathiri jamii kama homa ya mgunda, UKIMWI, ebola, selimundu, Kansa,homa ya ini, ugonjwa wa Alzheimer's na Parkinson's na magonjwa mengine hatarishi. Kupata suluhisho kunajumuisha kupata chanjo sahihi, dawa sahihi,na vitendanishi sahihi ambapo njia za molekuli ya baiolojia zina mchango mkubwa mno katika hili.
Njia hizi ni madhubuti kwa kuwa huchunguza vinasaba vya kisababishi cha ugonjwa fulani au jeni inayochochea ugonjwa huo, Mbinu hizi zinahitaji uwepo wa mitaji/ ruzuku kutoka kwa wadau/ wafadhili mbalimbali wanaofanya kazi katika sekta ya afya,mfano wa njia za molekuli ya baiolojia ni kama ifuatavyo
A: Njia ya mwitikio wa mnyororo wa polimerasi.
Hii ni mbinu ya molekuli baiolojia inayotumika kugundua uwepo wa Jeni za kiumbe kisababishi cha ugonjwa na ukuzaji wa Jeni hizo Ili kuzalisha nakala ya Jeni zinazofanana. Njia hii huhitaji sampuli za ugonjwa unaohisiwa na kinasaba/ Jeni hutenganishwa kwa mbinu ya electroforesis ndioo hatua tatu hufuata ambazo ni uchanganuzi wa kinasaba ( denaturation), ufungaji( annealing) na urefushaja( elongation) ambapo kinasaba hugawanywa kwa kiwango cha chini Ili kuzalisha nakala nyingi iwezekanavyo
B: Mpangalio wa DNA/ kinasaba na jenomiki
Hii ni mojawapo ya teknolojia ya msingi kwenye afya na ni muhimu katika utafiti wa magonjwa ya binadamu kwa kufanya uchunguzi wa jenomi nzima na Mpangalio wa nyukleotaidi katika kipande cha kinasaba au Jeni inayahusika na ugonjwa fulan, jenomu za viumbe wengi hutunzwa kwenye database ya nyukleotaidi na za za kimahesabu maarufu kama computation biology, database hizi husimamiwa na chombo kiitwacho National centre for Biotechnology information ( NCBI) ambazo huambatana na mbinu mbalimbali za bioinformatiki katika uchunguzi wa Jeni zinazohusika na ugonjwa.
C: Teknolojia ya mchanganyiko wa jenetiki ( recombinant DNA technology)
Hii ni teknolojia muhimu katika sayansiya dawa na tiba ambayo huhusisha Uundaji wa recombinant DNA kwa kuchanganya vinasaba kutoka vyanzo mbalimbali kupitia mchakato uuitwao uunganishaji wa jenetikia, hii huanza na utambuzi na utenganishaji wa Jeni husika kwa kutumia vimeng' Enya vizuizi ,uwekaji na Uundaji wa Jeni kwenye vekta na mwisho uwekaji wa vekta na Jeni kwenye bacteria maarufu kama Escherichia coli na mwisho utengenezaji wa seli na ukuzaji hufanyika na ndipo dawa, chanjo na molekuli mbalimbali mfano homoni ya insulini huzalishwa ambayo husaidia watu wenye tatizo la kisukari.
D: Uundaji wa mti wa ukoo wa fylojeni
Hii ni mbinu mojawapo ya molekuli ya baiolojia ambayo itakuwa ni muhimu katika sekta ya afya nchini Tanzania kwa sababu njia hii huchunguza uhusiano wa Jeni inayahusika na ugonjwa fulani kwa kuchunguza historia ya jenomu ya vizazi vilivyopita ( ancestors) ndipo watafiti hutumia uhusiano katika Jeni hiyo na chati ya ukoo Ili kupata chimbuko halisi la kisababishi cha ugonjwa.
Hitimisho: kwa hiyo mabadiliko katika sekta ya afya ni muhimu sana kwa ustawi wa jamii kwa sababu ulimwengu umebadalika na magonjwa yanazidi kuongezeka kila siku, serikali kupitia wizara ya afya Haina budi kushirikiana vyema na mashirika na wadau mbalimbali Ili kuwezesha miradi ya afya nchini, kwa sababu uanzishwaji au uboreshaji wa mbinu za molekuli ya baiolojia katika vituo vya afya inahtaji mtaji mkubwa na uwekezaji wa Hali ya juu kwa kuwa njia hii inatumia sayansi na teknolojia ya Hali ya juu pia
Ahsantee 🙏🏼

Upvote
24