Njia nzuri ya kuuziana kiwanja ni ipi?

Njia nzuri ya kuuziana kiwanja ni ipi?

jigili

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2011
Posts
350
Reaction score
344
Samahani wakuu,

Naombeni ushauri, nataka kununua kiwanja, kwa sh.7,000,000 mshikaji anayeniuzia nimepeleleza ni kweli ni chake na ndio anayetambulika na majirani.Tatizo lipo kwenye mauziano mshikaji anasema kadeposit pesa benki baada ya hapo tuje tuandikishane kitu ambacho kwangu mimi naona kama ni risk.

Naomba ushauri ni vipi tunaweza fanya mauziano ya namna hii kwa kuzingatia maslahi ya pande zote mbili yaani muuzaji anakuwa na uhakika wa pesa na mnunuaji anakuwa na uhakika wa kupewa documents.
 
Kumuamin mtu kazi kwel. Usikubali kulipa kwanza mpaka akupe documents
 
mimi sio mtaaramu sana ila kwa uzoefu wangu si sahihi kumlipa mtu kabla hajakukabidhi. kwa suala la kiwanja inatakiwa uende wewe na mashaidi zako wawili, pia yeye na mashaidi wawili 'mmoja awe ni mjumbe wa mtaa kiwanja kilipo' pia ni vizuri makabidhiano yafanyike serekali za mtaa sio kyenyeji, pia ni vizuri kupata ramani ya eneo husika kabla hujanunua. suala la aridhi linahitaji umakini katika manunuzi maana kuna viwanja vingine vinakuwa na mgogoro wa kifamilia, au mtu anaweza kuuza kiwanja kwa watu hata wawili, wapo wajuzi wa hili watakuja kukujuza zaidi
 
Back
Top Bottom