SoC02 Njia rafiki ya kukusanya kodi (Sekta ya Burudani)

SoC02 Njia rafiki ya kukusanya kodi (Sekta ya Burudani)

Stories of Change - 2022 Competition

Safari79

Member
Joined
Sep 15, 2022
Posts
6
Reaction score
7
Utangulizi
Kwa muda mrefu nimekuwa nikiwaza tunawezaje kukusanya kodi bila ya kutumia gharama kubwa ama bila ya mlipa kodi kulalamika ama bila ya kukwepa kulipa kodi.

Baadaye nikaona njia nyepesi ni ya kumhamasisha mlipa kodi ni pamoja na kwanza aone fahari kulipa kodi yenyewe kwa hiari lakini pia awajibike katika kuchukua hatua za kulipa kodi kwa wakati.

Nimekuwa nikiwaza kwa mfano: kwa msanii yoyote mkubwa Tanzania, ikitokea anaulizwa kwa mwaka 2020 ama 2021 alilipa kodi yenye thamani ya kiasi gani kwa kazi zake za muziki? -sina hakika na majibu yake yatakavyokuwa.

Sekta ya burudani
Mawazo yangu ni kwamba ulipaji wa kodi kwa serikali uwe ni sehemu ya furaha, mlipaji ajifanyie tathmini mwenyewe na kuipa thamani kazi yake kwa kodi anayolipa.

Serikali kwa upande wake inaweza kuwashindanisha wasanii kwa kiasi cha kodi wanazo lipa kwa serikali. Kuwa msanii kubwa kuakisiwe na mchango wake katika kutunisha mfuko wa serikali.

Ufike wakati tuwe na mlipa kodi bora katika muziki ama sanaa ya filamu ama mpira ama mshehereshaji ama maeneo mengine ya burudani. Mamlaka yamapato Tanzania inaweza kulibeba hili na kusaidia kuweka hamasa katika ulipaji wa kodi kwa serikali.

Wasanii wengi Tanzania wanaonekana wakiwa na matumizi makubwa sana katika majumba ama magari ya kifahari ama sherehe za kifahari: lakini kwa upande wa pili jamii haiwezi kupata picha halisi ya thamani ya sanaa na mchango wake katika maendeleo ya nchi.

Maana unaweza kukuta msanii ana jina kubwa sana Tanzania lakini ukakuta hana mchango hata kidogo katika mfuko wa serikali ambao unaenda kuhudumia sekta zingine za maendeleo.

Mapendekezo yangu
Itapendeza sana kama kutakuwa na namna msanii akawa anaruhusiwa kufanya shughuli flani ya maendeleo katikajamii kwa mfano kujenga shule ama kituo cha afya ama kuendelea eneo la wazi kwa kuijenga vizuri na likawa na mvuto basi badala ya kuja kulipa kodi yake basi mchango wake huo kama utaratibiwa vizuri basi uwe ni sehemu ya kodi yake ama kupitia msamaha wa kodi ama vinginevyo.

Hii itasaidia sana badala ya mlipa kodi kuwazia kodi yake haitamnufaisha mwananchi basi yeye binafsi awe ni gurudumu la kufikisha kodi yake kwa mwananchi moja kwa moja.

Hitimisho
Bado naamini kuwa ulipaji wakodi unapashwa kuwa burudani badala ya watu kuona kero na kuchochea ukwepaji wa kodi mara kwa mara. Na pia bado naamini ya kuwa thamani ya jina la msanii linapashwa kuendana na kiasi cha kodi anacholipa kwa serikali kwa mwaka.

Itapendeza siku moja tukawa na tuzo za walipakodi bora kwenye sekta ya burudani kuanzia waigizaji, muziki, studio za kurekodi, wachezaji wa mpira, washereheshaji nakadhalika nakadhalika.
 
Upvote 2
Back
Top Bottom