son_african_star
Member
- May 30, 2023
- 9
- 15
Fursa zipo kila mahali, ila changamoto huwa inakuwa kwetu ambao tumezungukwa na fursa hizo. Wengine wetu hudhani fursa ni kitu ambacho kipo wazi kama wengine wadhaniavyo, hapana fursa hii.
Fursa huwa zina tabia za kujificha, ambapo ili uweze kuona fursa hizo unatakiwa kufanya uchunguzi juu ya fursa hizo. Vile vile fursa mara nyingi huwa zina tabia ya kuona aibu ambapo zinasubiri uzifuate zilipo.
Robert kiyosaki aliwahi kusema "umaskini ni kupitia fursa kila wakati".
Ikiwa una changamoto ya kutokuona fursa kwenye eneo fulani basi hakikisha anatafuta majibu ya changamoto fulani katika eneo husika, hapo utakuwa umewaza kuiona fursa husika ambayo mwanzo ulikuwa huioni.
