Kisukari ni muhimu kuwapimwa mara kadhaa, hasa kama una historia ya kisukari kwa familia na/ama una uzito mkubwa.
Kwa ajili ya monitoring, fasting blood sugar ndio kipimo kizuri. Hii hufanywa asubuhi kabla ya kula chochote. Njia inayotumika haswa ni ya kutumia tone la damu kutoka kidoleni.
Njia ya kupima mkojo ilikuwa inafanyika zamani. Nadhani imepitwa na wakati, japo haiko conclusive lakini inafaa kuashiria uwepo wa tatizo (watabibu watahusika hapa)
Kwa yeyote anayejua naomba anifahamishe ni njia gani sahihi ya kupima kisukari.
-Kupima pale unapopatwa na dalili au kabla ya dalili? Na ukipima kabla ya dalili unaweza kuonekana?
-Njia nzuri ni ipi kupima damu au mkojo? Je njia ya kupima damu ni ile ya kutoboa kidole nakuweka damu kwenye kimashine au kuna nyingine. Msaada tafadhali.
Mkuu Oleni, ni ngumu sana kuweka dalili(Symptoms) za mgonjwa na kupata kwa uhalisia tatizo ni nini (exact Diagnosis).. kwani kila dalili inaweza kusababishwa na magonjwa mengi... na dalili ukizosema (<18yrs, Absence of familial history of DM doesnt rule out DM) kwani kuna kitu kinaitwa Type I DM/ Juvenile Diabetes Mellitus.
Ningekushauri, fika katika HOSPITALI yeyote ya karibu ili kujua shida ni nini kama vile Kujua tatizo ni nini, (nini kilichoanza), kwa muda gani, kilikuwa kinaendeleaje, kinapata unafuu kwa kufanyaje, nk...lakini pia vipimo mbali mbali vitaweza kusaidia kujua shida ni nini.
Baada ya kuona dalili au hata kabla.
Ni muhimu kupima kila wakati kama una risk factors nilizotaja hapo juu:
Uzito mkubwa (obesity)
Historia ya kisukari (type 2) kwenye familia
Kama mwanamke alipata kisukari wakati wa ujauzito (gestational diabetes)
Kama una dalili
Kwa huyu mdogo wako, kama huna hakika na maamuzi ya daktari, basi tafuta daktari mwingine umuone na vipimo vyote awape ushauri wa ziada.
Wakati mwingine ni wasiwasi tu.