Salam mdau wangu!
Ulishawahi kujiuliza kipi wanafunzi wanatakiwa kufanya kwa kutumia tekinolojia?
Siku ya leo nimependa kuandika makala yangu ya kwanza kwa lengo la kuhamasisha matumizi ya tekinolojia ya sasa na baadae. Ni ukweli usiopingika kwamba tekinolojia inakua kwa kasi ya ajabu. Dunia inazidi kubadilika katika tekinolojia, kwani tumeona kuongezeka kwa wataalamu wa kompyuta, mitandao,simu nakadharika. Mitandao inaongezeka siku hadi siku,watumiaji wanaongezeka siku hadi siku.
Siku hizi ni kitu cha kawaida kuona mtoto anajua kutumia simu au kompyuta hata kama bado hajaanza shule. Viwanda vya simu vinazidi kuleta matoleo mapya ya simu, makampuni ya kompyuta vilevile bila kusahau. Kila toleo jipya linakua limeboreka zaidi. Makampuni mengi ya vitu vya tekinolojia yapo kwenye ushindani hivyo kusababisha simu,kompyuta na vitu kama hivyo kuzidi kupungua bei siku hadi siku.
Sawa tumeipokea tekinolojia, lakini je tumejiandaa kuitumia katika shughuli mbalimbali? Je tunajua maadili ya utumiaji? Je tunajifunza nini kwa kutumia tekinolojia?
Katika uchunguzi wangu binafsi na kwa kusoma maandiko mbalimbali nimegundua kua watu mbalimbali shuleni wanafundishwa kompyuta ila sio kutumia kompyuta katika shughuli mbalimbali. Kinachofuata mtu amejua kompyuta lakini hajui kujifunza kwa kutumia kompyuta. Pia ni ushahidi tosha kwamba wanafunzi hawafundishwi maadili ya kutumia komputa ili waweze kuepuka kufanya mambo yasiofaa.
Wanafunzi wanatakiwa kujua kua hawajifunzi tu kutumia Simu, Kompyuta na mitandao mbalimbali tu, bali wanatakiwa kuelewa kuwa bado wanasoma . Tekinolojia ni kifaa kinachoweza kuwasaidia katika masomo yao kama Hesabu, Kiswahili na kadhalika. Mwandishi Jeff Dunn anasema Technology is a tool for learning, it is not a learning outcome , akiwa na maana kwamba Tekinolojia ni zana ya kusoma,tekinolojia sio matokeo ya kusoma. Tunajua kuwa walimu wengi hawajaandaliwa kuwafundisha wanafunzi wao kwa kutumia tekinolojia.
Hata kama kukiwa na vifaa vya kutumia bado hatujawa na uelewa wa kutumia vifaa hivi ili kutusaidia kwa vizazi vya baadae. Tupende tusipende tekinolojia haipingiki na haikwepeki katika ulimwengu wa sasa, hivyo wazazi na walimu tulichukulie uzito hili swala ili kukiandaa kizazi hiki kisije kukumbana na changamoto baadae.
Siku zinakuja, siku hizo kutakua na ushindani usio kifani. Ubunifu utakua ni wa hali ya juu katika tekinolojia. Pia niwaombe wataalamu na makampuni mbalimbali kuweka mitandao rasimi kwaajili ya wanafunzi kwani wanafunzi wanajua kutumia mitandao lakini wanaangalia vitu visivyo vyao kwasababu hawana sehemu zao rasimi kwaajili ya kujifunza.
Mwandishi mmoja anasema Let us direct them,Let us support them and Let them do. Akiwa na maana kwamba Tuwaoneshe, Tuwasaidie na wao wafanye. Tukitumia hizo hatua tutakua tumewasaidia katika kufanikisha mahitaji yao. Kuna taasisi mbalimbali pamoja na watu binafsi wamekua wakitoa misaada ya kompyuta mashuleni. Tatizo linakuja pale ambapo waliopewa hawajui kutumia au wanajua kutumia lakini si kwaajili ya kusomea.
Mwandishi Shantanu Sinha anasema Teachers are given tools without integrating properly with technology in their day to day instructions, teachers are not teaching with computer but they teach to use computer. Mwandishi huyu kutoka Khan academy anamaanisha kwamba walimu wanapewa vifaa vya tekinolojia bila kuelekezwa jinsi ya kutumia katika kufundisha masomo mbalimbali darasani.
Pia wanaojua kutumia wanawafundisha wanafunzi wao kutumia kompyuta tu ila sio wanatumia kompyuta katika kufundisha masomo mbalimbali. Hii ni kwa baadhi ya shule zenye vifaa hivi. Zipo shule nyingi sana hazina Kompyuta na wanafunzi hawajawahi kuziona kwa uhalisia ila ni kwa kuona picha za kwenye vitabu. Makala ijayo itaelezea jinsi gani tunaweza kuiondoa hii changamoto.
Karibu kwa maoni.
0755102156/0655102156