SoC01 Njia sahihi zaidi za kumjua mtu wa kumpa jukumu la Uongozi

SoC01 Njia sahihi zaidi za kumjua mtu wa kumpa jukumu la Uongozi

Stories of Change - 2021 Competition

smartdunia

Member
Joined
Jul 29, 2021
Posts
12
Reaction score
9
Na Smartdunia.

Uongozi ni jambo kubwa na lenye umuhimu mno katika ngazi yoyote Ile ya jamii.

Iwe ngazi ya familia,kitongoji,kijiji au,kata,tarafa na hata nchi,inahitaji kiongozi wa kufanya maamuzi ili mambo yaweze kuenda mbele.

Acha mbali kabisa kutokuwepo kwa uongozi,tuongelee swala la uongozi ulio bora.

Kikundi chochote kikikosa kiongozi Bora,basi mambo hurudi nyuma kwa kasi kama sio kusimama kabisa.

Tusiende mbali sana,fikiria familia yenye baba mlevi kupindukia,na ndiye anayetegemewa kulipa ada za watoto,matokeo yake ni yapi?

Watoto hawawezi kusoma mpaka nguvu nyingine iingilie kati.

Mfano huu ni sawa na nchi ikikosa rais na viongozi wengine walio bora,mambo hayawezi kuwa mazuri kabisa.

Basi kwa mifano hii,tunapata jawabu kwamba ni lazima tujue umuhimu wa kuchagua viongozi Bora katika jamii zetu ili kudumisha utawala Bora.

Je, tuangalie nini kabla ya kuchagua viongozi watakaohakikisha utawala wao unakua Bora?


Yafuatayo ni mambo makubwa sita ya kuzingatia.


1.Jinsi gani anavyoweza kujiongoza yeye mwenyewe.

Hapa tunaweza kuangalia jinsi anavyopangilia mambo yake na kupambana kutimiza ndoto zake bila kusukumwa na mtu yeyote,mtu asiyeweza kujua nini cha kufanya kutimiza ndoto zake,hawezi kusimamia ndoto za wengine.


2.Ana uwezo gani wa kutoa mawazo yenye nguvu.
Kiongozi siku zote,haishiwi hoja zinazochochea kutoa suluhisho la matatizo mbali mbali.Mtu wa aina hii,hata kuwe na hali ngumu kiasi gani bado anakua na moyo wa kujaribu akiamini ushindi upo tu.


3.Uwezo wake wa kujiamini kwenye hali zote.
Kiongozi mzuri hateteleshwi na hali,hata kue na hali ya kutisha husimama imara kwani anajua katika utulivu wa akili,matatizo husuluhishwa kwa uhakika zaidi.


4.uwezo katika ujuzi wa kuwasiliana.
Kiongozi mzuri anajua na pia hujifunza kila siku namna ya kuwasiliana na watu wa rika zote na katika mazingira yote.


5.Mienendo na tabia katika jamii.
Historia yake katika jamii,lazime iwe yenye kuridhisha.


6.Uwezo wa kusaidia wengine.
Anakua na historia ya kusaidia watu kwa hiari yake,hiyo hufanya hata akipewa jukumu,inakua ni rahisi na kawaida yake kuwatendea watu utu ambao ni asili yake.

Nikutakie maamuzi mema katika kuchagua mtu wa kukuongoza popote utakapotakiwa kufanya hivyo.
 
Upvote 2
Back
Top Bottom