Njia tano za usafirishaji

Cesar Saint

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2016
Posts
423
Reaction score
726
Habari za muda wanaJamvi

Nyanja ya usafiri imekuwa ikikumbwa na kasumba mbalimbali ulimwenguni kutokana na hali za uchumi za watumiaji lakini pia ongezeko la watu ambalo huongeza uhitaji wa usafiri wa haraka na uhakika ; Nyanja hii inasumbuliwa pia na adha mbalimbali ikiwemo foleni ,miundombinu isiyokizi na mingine isiyofaa na hivyo kuleta adha katika shughuli zima za usafirishaji.

July 2012 akiwa katika tukio la Pandodaily jijini Santamonica,California bwana Elon Musk alileta wazo ambalo inasadikika kuwepo kwa zaidi ya karne kwenye nyanja za watafiti wa maswala ya sayansi ya usafirishaji ;
Wazo hili si lingine bali ni “fifth mode of transportation” akiita HYPERLOOP hii inatokana na usafiri huu kutumia miundombinu ya loop kwa nadharia usafiri huu wenye mwendokasi wa ajabu ungeweza kuepukana na kadhia ya hali ya hewa ,matumizi madogo ya nishati , mwendo kasi mara mbili ya ule wa ndege ya kawaida , uwezo wa kuhifadhi nishati na nzuri zaidi COLLISION FREE.



Hyperloop transport ni nini?
Huu ni mfumo unaundwa na tube/tunnel ambazo zinakuwa zimefunikwa kila mahala yaani sealed ili kuwezesha chetezo ya usafirishaji (pod) kusafiri bila ukinzani wa hewa wala msuguano hii inawezeshwa na mipira ya kutoa hewa kwenye hizi tube/tunnel za kusafiria huku pod ikisukumwa katika air bearings zinazoendeshwa na linear induction motor na air compressors na kupelekea usafiri wa haraka na salama.






Mafundi kutoka kampuni ndugu za SPACE X na TELSA wanaendelea kushirikiana kukamilisha ujenzi wa Hyperloop transportation ya kwanza kutoka Los Angeles kwenda San Francisco Bay area ambapo itasafirisha abiria umbali wa kilomita 560 kwa kutumia mwendokasi wa 1200km/hr kwa kutumia muda wa dakika 35 hii ni zaidi ya muda unaweza kutumiwa na treni ya umeme ama ndege ya abiria .






Mradi huu unatarajia kugharimu USD billioni 6 kwa miundombinu ya kusafirisha abiria tu na USD billioni 7.5 kwa miundombinu yenye uwezo wa kusafirisha watu na magari yao .



Mradi huu tayari umeshaanza kutekelezwa na June 2015 SpaceX walitangaza kuanza kutengeneza test track ya kilomita 1600 ambayo itakuwa karibu na jengo lao la Hawthorne ambapo itatumika kwaajili ya kufanyia majaribio na maboresho.



Njia hii ya usafirishaji bado ni utafiti mkubwa hivyo milango ikowazi kwa taasisi na watu wengine kushirikiana na SpaceX pamoja na Tesla kuweza kuufanikisha .

Asante.
 
unafikiri hizi ni akili za kawaida za kibinadamu tuu. angalia kwa makini technology nyingi mpya utagundua kuna nguvu ya ziada tfaut na akili za kawaida za kibnadamu. unaweza usielewe ninachozungumza.
 
fafanua mkuu, sisi wa akili ndogo umetuvuruga kabisa
unafikiri hizi ni akili za kawaida za kibinadamu tuu. angalia kwa makini technology nyingi mpya utagundua kuna nguvu ya ziada tfaut na akili za kawaida za kibnadamu. unaweza usielewe ninachozungumza.
 
Huyu jamaa sio wa kawaida..wasije wakamuua tu maana!
 
Hawa Wapo Ulimwengu Mwingine Sijui Alliens Wanawapa Ujanjaujanja Kufanya Mambo Yao Ama Ufo
 
Hayo mambo yalikuwako toka kale na ni zaidi ya hayo,hamna ubunifu zaidi ya copy.
 
Huo ni usafiri wa watu wa dunia ya kisasa. Ngoja sisi tuendelee kuhangaika na standard gauge na bombadier.
 
Maendeleo huja kulingana na changamoto anazokumbana nazo mwanadamu na namna anavyozishughulikia, hapo hakuna ufo, aliens wala nini, hiyo ni namna binadamu anavyofikiria kukabiliana na changamoto za dunia ya kileo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…