Njia ya asili ya uzazi wa mpango kwa kupima vichocheo (Homoni) vilivyopo kwenye mkojo wa mwanamke

Njia ya asili ya uzazi wa mpango kwa kupima vichocheo (Homoni) vilivyopo kwenye mkojo wa mwanamke

Strong ladg

Senior Member
Joined
Jul 15, 2021
Posts
170
Reaction score
445
Leo nimekutana na hii njia ya asili ya uzazi wa mpango ambayo watumiaji wake wakubwa wako nchi zilizoendelea.

Njia hii inaitwa Marquette Method kwa sababu ilianzishwa na wataalamu waliopo chuo kikuu cha Kikatoliki cha Marquette cha nchini Marekani.

Njia hii huhusisha mwanamke kupima mkojo wake kwa kutumia kifaa maalum kiitwacho Fertility Monitor mara aamkapo asubuhi.

Kifaa hiki hupima homoni zinazohusiana na masuala ya uzazi zinazopatikana kwenye mkojo na kumwezesha mwanamke kujua kama yupo kwenye siku za kushika ujauzito au lah.

Baada ya kujua kama yuko kwenye siku za kushika ujauzito au lah, wenzi wataamua kushiriki tendo la ndoa au kutokushiriki (abstaining) kulingana na malengo yao kwa wakati huo.
Njia hii huweza kutumiwa na mwanamke yeyote ambaye yuko kwenye umri wa kuzaa i.e mwenye mzunguko wa kawaida, anaenyonyesha, mwenye magonjwa yanayovuruga mzunguko n.k ingawa masharti ya matumizi hutofautiana eg mwanamke anayenyonyesha anatakiwa kupima mkojo kila siku wakati ambaye yuko kwenye mzunguko wa kawaida hana haja ya kuendelea kupima baada ya kuthibitisha kwamba siku za kushika ujauzito zimepita.

Kabla ya kutumia njia hii, sharti mwanamke ajifunze kupitia wataalamu waliopewa mafunzo maalum na kuidhinishwa kuwa walimu wa Marquette Method. Pia ni lazima mwanaume ahusishwe kwa sababu bila mwanaume kuhusika, njia hii haiwezi kufanikiwa.

FAIDA ZA KUTUMIA MARQUETTE MÉTHOD
1. Haina madhara yoyote kiafya
2. Ina usahihi wa asilimia 99 kama ikitumiwa kiusahihi.
NB: Njia pekee ya kuzuia mimba kwa asilimia 100 ni kutofanya tendo la ndoa kabisa.
3. Huweza kutumiwa na watu wasiopenda kutumia njia za kisasa kama vile vidonge , sindano, kitanzi n.k
4. Huweza kutumiwa kwa ajili ya kushika ujauzito kwa sababu humuwezesha mwanamke kujua kwa usahihi siku za kushika ujauzito ni zipi.
5. Huimarisha uhusiano kati ya wenza kwa sababu ni lazima mwanaume ashirikishwe.

HASARA
1. Ni gharama kubwa kwa sababu itahitaji kununua kifaa cha kupimia( monitor), strips( vijiti) za kupimia na gharama za mafunzo kutoka kwa mtaalamu aliyeidhinishwa.
Hii ni sababu kuu kwanini watumiaji wakubwa wa njia hii wanapatikana nchi kama Marekani

2. Strips (vijiti vya plastiki) vinavyotumika kupimia ni lazima vitupwe kwa uangalifu kwa sababu vinaweza kueneza magonjwa kwakuwa huwekewa mkojo wa binadamu.

Reference:
"Efficacy of the Marquette Method of natural family planning - PubMed" Efficacy of the Marquette Method of natural family planning - PubMed

afm_hcp_0.jpg
clearblue-advanced-fertility-monitor-refill-tests-24-pcs.jpg
 
Back
Top Bottom