SoC03 Njia ya kukomeshwa rushwa na ufisadi

SoC03 Njia ya kukomeshwa rushwa na ufisadi

Stories of Change - 2023 Competition

Mdude_Nyagali

Member
Joined
Dec 11, 2022
Posts
79
Reaction score
1,444
Kutokana na sheria za rushwa na ufisadi kuwawajibisha watu kwa matabaka ya vyeo na uwezo, nilikuwa napendekeza mambo yafuatayo;

1. Tuwe na sheria ambayo inawapa mamlaka TAKUKURU kuwajibika kwa kuwachukulia hatua za kisheria watumishi wote ambao watakuwa wanatajwa kwenye ripoti ya CAG kufanya ubadilifu wa mali za umma kwa kila mwaka.

2. Sheria iizinishe kesi zote zinazohusu ufisadi na rushwa kusikilizwa kwa hati ya dharura ndani ya siku 30 huku uendeshaji wa kesi hizo ukirushwa mubashara kwenye vyombo vya habari ikiwemo tv.

3. Kwamba sheria itofautishe adhabu kulingana na kiwango ambacho mtu anatuhumiwa nacho sambamba na kurudisha kiasi unachotuhumiwa nacho.

4. Kuwepo na Utaratibu wa bunge kufanya tathimini ya hatua zilizochukuliwa kwa wabadilifu ripoti ya CAG n.k. kwa kila mwaka.

5. TAKUKURU ilindwe kisheria ili isiingiliwe utendaji wake na iwe huru.

6. Rais asiwe na mamlaka ya kutengua au kumhamisha mkurugenzi wa TAKUKURU mpaka astaafu kama ilivyo kwa CAG.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom