Njia ya kulipa ada India

drilling

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2016
Posts
4,761
Reaction score
4,926
Naomba kujua nitamlipiaje ndugu yangu fees yupo India kupitia bank ya ICICI sijui kama ipo hapa Tanzania na pili kutuma fees bila kufungua Acc Bank nionyeshene njia mwenye kujua.
 
Nenda bank utaelekezwa,mbona sisi hua tunalipia magari japan na bank za huko hapa hazipo bila kua na account bank za huku,linawekana hili.
 
Ngoja waje wale wazee wa ile pesa tuma kwenye namba hii...jina litakuja Humphrey polepole.

Watu wengine mnatengeneza wenyewe mianya ya kupigwa
 
Naomba kujua nitamlipiaje ndugu yangu fees yupo India kupitia bank ya ICICI sijui kama ipo hapa Tanzania na pili kutuma fees bila kufungua Acc Bank nionyeshene njia mwenye kujua.
Muombe huyo ndugu yako mwanafunzi akutumie banking details za chuo ikiwemo account #,swift code,branch,location, na name of the account holder, na kiasi gani unastahili kulipa may be in Indian rupees au dollar, Omba pia wakutumie invoice/claim document ya kuthibitisha kwa nn uwalipe (wao wanajua mostly invoice). Invoice watakutumia electronically (email/whatsapp) utai-print.

Nenda bank yako hapa waeleze unachotaka kufanya waonyeshe na invoice uliotumiwa watakupa form special ya kutuma watakwambia gharama na exchange rate then utajaza hiyo form utawapa na hela bank watatuma wataweka na stamp zote. Halafu utaenda ku scan/piga picha na kumtumia huyo ndugu as a proof of payment/kithibitisho cha kulipa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…