SoC01 Njia ya kumaliza tatizo la ajira na umasikini hapa nchini

SoC01 Njia ya kumaliza tatizo la ajira na umasikini hapa nchini

Stories of Change - 2021 Competition

Tindo

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2011
Posts
63,730
Reaction score
111,542
Ni ukweli usiopingika kuwa maji ni uhai, na ni dhahiri maji ni huduma isiyo na mbadala. Kwa mtazamo wangu iwapo maji yatafika kila sehemu ndani ya nchi hii, kila mtu atakuwa na uhakika wa kupata ajira, na uzalishaji utaongezeka. Iwapo uzalishaji utaongezeka ni wazi kuwa nchi hii itakuwa na bidhaa nyingi za kutosheleza wananchi wa humu na ndani na ziada yote kuuza nje.

Ni kwa jinsi gani maji yatatoa ajira kwa kila mtu na kuondoa umasikini hapa nchini? Ukijaribu kuangalia zaidi ya 65% ya watanzania wanaishi vijijini, na shughuli kubwa za huko vijijini ni kilimo na ufugaji. Shughuli zote hizi zinategemea maji ili kuweza kufanyika. Lakini utakuta kutokana na misimu ya mvua kuwa mara moja au mbili kwa mwaka, na wakati mwingine mvua hizo huzidi ama kupungua. Hali hiyo hupelekea sehemu kubwa ya kilimo kuwa ni cha msimu, na wakati wa mvua haba, ama kuzidi mavuno huwa chini ya matarajio.

Lakini iwapo kutakuwa na maji ya bomba kote nchini, ni wazi baada ya msimu wa mvua bado watu wataweza kulima, na kufuga mifugo yenye tija. Kukiwa na maji kila mahali wale wafugaji wanaofuga mifugo mingi na kuitembeza ili kusaka malisho na maji, hawatahitaji kufanya hivyo. Wale wakulima wanaoshindwa kulima kutokana na kutokuwepo na mvua, na kuishia kukaa muda mrefu bila kitu cha kufanya wakisubiri msimu wa mvua, wataweza bado kulima kilimo cha kisasa kama mbogamboga, matunda na mazao mengine ya muda mfupi, hasa kwenye green house, na bustani zenye tija. Pia kitendo cha kusambaza maji nchi nzima ni lazima uoto utarajea kwa kasi kubwa nchini.

Ukijaribu kuangalia, vijana wengi wanaondoka huko vijijini kwani kilimo na ufugaji hakiwapi mapato mazuri kutokana na uhaba wa maji kwani mvua ni za msimu, na ni haba pia. Lakini iwapo kungekuwa na upatikanaji wa maji ya bomba, hawa wote wanaokimbia huko vijijini, wasingekuja mijini maana wangekuwa na kazi za kufanya mwaka mzima, na hatimaye kuondokana na umasikini kutokana na uzalishaji mali. Na iwapo huko vijijini kutakuwa na uzalishaji mali, ni wazi uzalishaji mali huo utavutia viwanda ili kuchakata mali hizo.
Nchi zote zilizoendelea dunia hii sio zile zilizotegemea raslimali tu, bali ni zile zenye uzalishaji mkubwa.

Je haya yanaweza kufikiwa vipi? Iwapo serekali ndani ya hii miaka mitano imeweza kufanya miradi inayofikia 20t, kiwango hicho hicho kingewekezwa kwenye maji nchi nzima, ni dhahiri kwa sasa tungekuwa taifa linaoongoza kwa uzalishaji mali hapa Afrika. Mradi wa SGR ni shilingi 10t+, mradi wa SG ni 6.5t na ndege zinafikia 2t. Miradi yote hiyo tungeweza kuipata hata kwa kukopeshwa, iwapo hiyo 20t ingewekezwa kwenye miradi ya maji nchi nzima. Sio lazima usambazaji huu wa maji uwe mara moja nchi nzima, lakini inaweza kufanyika kwa awamu. Ndani ya miaka mitano tutaweza kuona matokeo ya awali.

Kisha mapato toka sehemu zenye miundo mbinu ya maji kuwe na mfuko maalumu wa kunyanyua sehemu nyingine. Ndani ya miaka 15 tutakuwa tumeachana na tatizo la ajira kwa wananchi wetu, kwani tutakuwa taifa lenye wazalishaji wengi, kuliko wachuuzi, na wakulima wa kilimo cha kujikimu.
 
Upvote 3
Ninategemea serikali iweze kuchukua hatua stahiki kwenye hili.
 
Back
Top Bottom