SoC04 Njia ya kupunguza tatizo la ajira kwa vijana waliosoma na Wasiosoma na kuongeza pato la taifa nchini Tanzania

Tanzania Tuitakayo competition threads

ZANNUUN

New Member
Joined
May 12, 2024
Posts
1
Reaction score
0
Ajira ni tatizo kubwa linalozikumba nchi nyingi duniani, tatizo hilo linajulikana kama (Global Problem) likiwa na maana ya tatizo la kidunia. Kutokana na ripoti iliyotolewa na Decent Job for Youth 2024, inaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 13.3% ya vijana wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 35 wanakumbwa na tatizo la ajira.

Pia kwa Afrika, tatizo la ajira limeendelea kuwa changamoto kwa vijana na kupelekea vijana wengi kutokidhi mahitaji yao kikamilifu, na hii hupelekea vijana wengi kujiingiza katika shughuli zisizo za kisheria kwa ajili ya kujipatia kipato. Kwa Afrika tathmini inaonyesha kuwa vijana wenye umri wa miaka kuanzia 15 hadi 35 wana tatizo la ajira, ambayo ni asilimia 11.3 kwa mujibu wa ripoti ya Statistical of Economy 2024.

Kwa Afrika ya Mashariki, tatizo la ajira limekuwa likiongezeka siku hadi siku licha ya juhudi zinazochukuliwa na nchi hizo katika kutatua tatizo la ajira bado limekuwa ni changamoto kwa vijana waliosoma na wasiosoma. Hii hupelekea kupoteza nguvu ya taifa kwa nchi za Afrika ya Mashariki kwa vijana hao kwa kujiingiza katika shughuli za hatari kiafya ambazo sio za kisheria, ikiwemo uuzaji na utumiaji wa madawa ya kulevya, uasharati na wizi. Kwa mujibu wa ripoti ya Statistical Research Department 2023 inaonyesha kuwa asilimia 4.5% ya vijana wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 35 hawana ajira.

Pia Tanzania ni nchi inayoendelea ambayo watu wake wamejikita zaidi katika sekta ya kilimo, zaidi ya asilimia 75% ya Watanzania wamejikita katika shughuli za kilimo cha kujipatia mlo pamoja na kilimo cha biashara. Serikali pia imekuwa ikichukua hatua kubwa katika kupunguza tatizo la ajira, kama vile kutoa fursa za ajira katika taasisi za kiserikali, kutengeneza miundombinu ambayo itakuwa ni chachu ya kupunguza tatizo la ajira, na kuandaa mazingira mazuri ya uwekezaji ili kupunguza tatizo la ajira kwa waliosoma na wasiosoma.

Tukiangalia Tanzania inatakribani vijiji 12,423 kwa mujibu wa ripoti ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na ina idadi ya watu 61,741,120 kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2022, ambapo Tanzania bara ina watu 59,851,347 na Tanzania visiwani ina takribani watu 1,889,773. Idadi ya vijana wasiokuwa na ajira ni 12.2% hii ni sawa na vijana 1,732,502 wenye umri wa miaka kuanzia 15 hadi 35.

Pia tunafahamu kuwa serikali imeweka taasisi maalumu za utoaji wa mikopo kwa ajili ya kuwasaidia wajasiriamali wadogo wadogo wanaojishughulisha na kilimo au biashara nyingine. Licha ya kuwa na zaidi ya asilimia 75% kujikita katika shughuli za kilimo na serikali kusaidia kikamilifu katika nyanja mbalimbali kwa lengo la kupunguza tatizo hilo la ajira, bado suala la ajira limekuwa ni changamoto kwa vijana waliosoma na wasiosoma na kupelekea vijana wengi kukosa ajira.

Kwa ushauri wangu kwa serikali yangu tiifu juu ya suala la kupunguza ajira kwa vijana waliosoma na wasiosoma, kutokana na zaidi ya asilimia 75% ya Watanzania wamejikita katika sekta ya kilimo. Ipo haja ya kuyaongezea thamani mazao ya kilimo yanayozalishwa kama vile mazao ya mboga mboga kwa kutengeneza bidhaa tofauti ili kuyaongezea thamani na kuibua fursa kwa vijana. Kwa mfano, zao la nyanya tunaweza kutengeneza bidhaa kama vile tomato paste, tomato sauce na pia tunaweza kutumia maganda yake kama mbolea au chakula kwa wanyama.

Hivyo, ninashauri serikali yangu tiifu ianzishe viwanda vidogovidogo kwa kila kijiji kutengeneza tomato paste na tomato sauce ukizingatia uzalishaji wa nyanya nchini ni mkubwa na muda mwingine kupelekea wakulima kukosa soko na nyanya kuharibikia shambani. Hii itapelekea upatikanaji wa ajira kwa vijana waliosoma na wasiosoma, pia itahamasisha walimaji wa mboga mboga aina ya nyanya kulima kwa wingi na kuzalisha kwa wingi zaidi ili wajipatie kipato kutokana na uhakika wa soko kwenye viwanda hivyo vidogovidogo.

Utaratibu ambao ninapendekeza katika mradi huo wa viwanda vidogovidogo wa utengenezaji wa tomato paste na sauce ni kama hivi ifuatavyo:

  • Serikali itoe mashine hizo kwa kila kijiji, mashine hizo zinaweza kutolewa kwa awamu au kwa pamoja kutokana na bajeti ya serikali itakavyopitishwa.
  • Utaratibu wa utoaji wa mashine hizo uwe katika hali ya ukopeshwaji usio na riba na wala sio kupewa bure, hii itasaidia mashine hizo kutunzwa na kuwa katika sehemu salama kwa kipindi chote cha ufanyaji kazi, na baada ya miaka mitatu au minne kurejesha gharama hizo sehemu husika.
  • Kuzingatia gender (jinsia) katika watakao pata au kukabidhiwa mashine hizo kwa pamoja waliosoma na wasiosoma hii itasaidia ufanisi mkubwa wa ufanyaji kazi na kuzingatia haki sawa kwa wote, wake na waume.
  • Waandaliwe mazingira ya masoko ambayo itawasaidia kuuza bidhaa hizo ndani na nje ya nchi, masoko ni muhimu sana katika uzalishaji pakiwa na uhakika wa soko itasaidia kuzalisha zaidi kulingana na malighafi zilizopo.
  • Kupewa taaluma ya utengenezaji wa tomato paste na tomato sauce ili kuboresha bidhaa hizo ziwe katika kiwango cha kimataifa, bidhaa nzuri ni bidhaa yenye ubora katika kila hatua. Kupitia mafunzo na taaluma watakazopewa itasaidia kuzalisha kwa ubora na udhibiti mzuri pamoja na vifungashio ambavyo ni vya kisasa ili kufikia viwango vya soko la kimataifa.
  • Kushiriki katika maadhimisho ya kibiashara ili kuwavutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi na kuongeza maendeleo katika nchi, kupitia maadhimisho ya kibiashara itasaidia kujitangaza zaidi kwa wadau mbalimbali wakiwemo wateja, wasambazaji wanaouza kwa rejareja, jamii, wafanyakazi wengine, serikali, taasisi binafsi na mashirika ya serikali, na wawekezaji. Hii itakuza maendeleo endelevu katika viwanda hivyo vidogovidogo na kufikia malengo waliojiwekea.
 
Upvote 2

Wewe unanena vema. Thamani halisi ya kazi za mkulima ikitiliwa maanani tunakuwa tumetatua tatizo la ajira kwa kiwango kikubwa sana.
Waandaliwe mazingira ya masoko ambayo itawasaidia kuuza bidhaa hizo ndani na nje ya nchi, masoko ni muhimu sana katika uzalishaji pakiwa na uhakika wa soko itasaidia kuzalisha zaidi kulingana na malighafi zilizopo.
Na hui ndio mzizi wa tatizo letu, manaake hata hiyo tomato paste tunaitengeneza ni kwa ajili ya kutawala soko vizuri zaidi.
Kushiriki katika maadhimisho ya kibiashara ili kuwavutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi na kuongeza maendeleo katika nchi, kupitia maadhimisho ya kibiashara itasaidia kujitangaza zaidi kwa wadau mbalimbali wakiwemo wateja, wasambazaji wanaouza kwa rejareja, jamii, wafanyakazi wengine, serikali, taasisi binafsi na mashirika ya serikali, na wawekezaji. Hii itakuza maendeleo endelevu katika viwanda hivyo vidogovidogo na kufikia malengo waliojiwekea.
Nane nane inasaidia sana kwa suala hili. Nanenane effect.
 
Ajira ni tatizo kubwa linalozikumba nchi nyingi duniani, tatizo hilo linajulikana kama (Global Problem) likiwa na maana ya tatizo la kidunia. Kutokana na ripoti iliyotolewa na Decent Job for Youth 2024, inaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 13.3% ya vijana wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 35 wanakumbwa na tatizo la ajira.

Pia kwa Afrika, tatizo la ajira limeendelea kuwa changamoto kwa vijana na kupelekea vijana wengi kutokidhi mahitaji yao kikamilifu, na hii hupelekea vijana wengi kujiingiza katika shughuli zisizo za kisheria kwa ajili ya kujipatia kipato. Kwa Afrika tathmini inaonyesha kuwa vijana wenye umri wa miaka kuanzia 15 hadi 35 wana tatizo la ajira, ambayo ni asilimia 11.3 kwa mujibu wa ripoti ya Statistical of Economy 2024.

Kwa Afrika ya Mashariki, tatizo la ajira limekuwa likiongezeka siku hadi siku licha ya juhudi zinazochukuliwa na nchi hizo katika kutatua tatizo la ajira bado limekuwa ni changamoto kwa vijana waliosoma na wasiosoma. Hii hupelekea kupoteza nguvu ya taifa kwa nchi za Afrika ya Mashariki kwa vijana hao kwa kujiingiza katika shughuli za hatari kiafya ambazo sio za kisheria, ikiwemo uuzaji na utumiaji wa madawa ya kulevya, uasharati na wizi. Kwa mujibu wa ripoti ya Statistical Research Department 2023 inaonyesha kuwa asilimia 4.5% ya vijana wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 35 hawana ajira.

Pia Tanzania ni nchi inayoendelea ambayo watu wake wamejikita zaidi katika sekta ya kilimo, zaidi ya asilimia 75% ya Watanzania wamejikita katika shughuli za kilimo cha kujipatia mlo pamoja na kilimo cha biashara. Serikali pia imekuwa ikichukua hatua kubwa katika kupunguza tatizo la ajira, kama vile kutoa fursa za ajira katika taasisi za kiserikali, kutengeneza miundombinu ambayo itakuwa ni chachu ya kupunguza tatizo la ajira, na kuandaa mazingira mazuri ya uwekezaji ili kupunguza tatizo la ajira kwa waliosoma na wasiosoma.

Tukiangalia Tanzania inatakribani vijiji 12,423 kwa mujibu wa ripoti ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na ina idadi ya watu 61,741,120 kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2022, ambapo Tanzania bara ina watu 59,851,347 na Tanzania visiwani ina takribani watu 1,889,773. Idadi ya vijana wasiokuwa na ajira ni 12.2% hii ni sawa na vijana 1,732,502 wenye umri wa miaka kuanzia 15 hadi 35.

Pia tunafahamu kuwa serikali imeweka taasisi maalumu za utoaji wa mikopo kwa ajili ya kuwasaidia wajasiriamali wadogo wadogo wanaojishughulisha na kilimo au biashara nyingine. Licha ya kuwa na zaidi ya asilimia 75% kujikita katika shughuli za kilimo na serikali kusaidia kikamilifu katika nyanja mbalimbali kwa lengo la kupunguza tatizo hilo la ajira, bado suala la ajira limekuwa ni changamoto kwa vijana waliosoma na wasiosoma na kupelekea vijana wengi kukosa ajira.

Kwa ushauri wangu kwa serikali yangu tiifu juu ya suala la kupunguza ajira kwa vijana waliosoma na wasiosoma, kutokana na zaidi ya asilimia 75% ya Watanzania wamejikita katika sekta ya kilimo. Ipo haja ya kuyaongezea thamani mazao ya kilimo yanayozalishwa kama vile mazao ya mboga mboga kwa kutengeneza bidhaa tofauti ili kuyaongezea thamani na kuibua fursa kwa vijana. Kwa mfano, zao la nyanya tunaweza kutengeneza bidhaa kama vile tomato paste, tomato sauce na pia tunaweza kutumia maganda yake kama mbolea au chakula kwa wanyama.

Hivyo, ninashauri serikali yangu tiifu ianzishe viwanda vidogovidogo kwa kila kijiji kutengeneza tomato paste na tomato sauce ukizingatia uzalishaji wa nyanya nchini ni mkubwa na muda mwingine kupelekea wakulima kukosa soko na nyanya kuharibikia shambani. Hii itapelekea upatikanaji wa ajira kwa vijana waliosoma na wasiosoma, pia itahamasisha walimaji wa mboga mboga aina ya nyanya kulima kwa wingi na kuzalisha kwa wingi zaidi ili wajipatie kipato kutokana na uhakika wa soko kwenye viwanda hivyo vidogovidogo.

Utaratibu ambao ninapendekeza katika mradi huo wa viwanda vidogovidogo wa utengenezaji wa tomato paste na sauce ni kama hivi ifuatavyo:

  • Serikali itoe mashine hizo kwa kila kijiji, mashine hizo zinaweza kutolewa kwa awamu au kwa pamoja kutokana na bajeti ya serikali itakavyopitishwa.
  • Utaratibu wa utoaji wa mashine hizo uwe katika hali ya ukopeshwaji usio na riba na wala sio kupewa bure, hii itasaidia mashine hizo kutunzwa na kuwa katika sehemu salama kwa kipindi chote cha ufanyaji kazi, na baada ya miaka mitatu au minne kurejesha gharama hizo sehemu husika.
  • Kuzingatia gender (jinsia) katika watakao pata au kukabidhiwa mashine hizo kwa pamoja waliosoma na wasiosoma hii itasaidia ufanisi mkubwa wa ufanyaji kazi na kuzingatia haki sawa kwa wote, wake na waume.
  • Waandaliwe mazingira ya masoko ambayo itawasaidia kuuza bidhaa hizo ndani na nje ya nchi, masoko ni muhimu sana katika uzalishaji pakiwa na uhakika wa soko itasaidia kuzalisha zaidi kulingana na malighafi zilizopo.
  • Kupewa taaluma ya utengenezaji wa tomato paste na tomato sauce ili kuboresha bidhaa hizo ziwe katika kiwango cha kimataifa, bidhaa nzuri ni bidhaa yenye ubora katika kila hatua. Kupitia mafunzo na taaluma watakazopewa itasaidia kuzalisha kwa ubora na udhibiti mzuri pamoja na vifungashio ambavyo ni vya kisasa ili kufikia viwango vya soko la kimataifa.
  • Kushiriki katika maadhimisho ya kibiashara ili kuwavutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi na kuongeza maendeleo katika nchi, kupitia maadhimisho ya kibiashara itasaidia kujitangaza zaidi kwa wadau mbalimbali wakiwemo wateja, wasambazaji wanaouza kwa rejareja, jamii, wafanyakazi wengine, serikali, taasisi binafsi na mashirika ya serikali, na wawekezaji. Hii itakuza maendeleo endelevu katika viwanda hivyo vidogovidogo na kufikia malengo waliojiwekea.
Hivyo unavyosema vishafanyika na watu wakakimbia na hela na vitu havikufanyika inavyotakiwa. Solution ya kutokomeza suala la ajira ni kuwapa masharti ya makampuni makubwa na matajiri wa kubwa wa nchi. Hawa matajiri wapewe masharti ya idadi ya watu wanaotakiwa kuajiri, na mazingira ya kazi yawe mazuri walipiwe bima ya afya na social security fund. Hawa matajiri wakitimiza haya wasilipe kodi na wasaidiwe ruzuku pale wanapostahili.Social securities na bima ya afya inatosha kabisa kuendesha nchi. Kama kila mtanzania akipata ajira na akalipa bima ya afya na pensheni. Hela za hii mifuko nzinatosha kabisa kuendehsa nchi. Mwanzoni watakimbia wachache lakini mazingira kama haya tukiwa nayo watakuja matajiri wengi wakubwa wa dunia kuwekeza hapa nchini. Leo hii tunawapa ruzuku matajiri wakubwa ambao hawana mfanyakazi hata mmoja mwenye bima ya afya au ppf. Hii nchi tunaipeleka wapi, wanaofaidika na wafanyabiashara wakubwa ni wafanyakazi wa TRA na sio wananchi wala serikali.
 
Back
Top Bottom