Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
M. M. Mwanakijiji
Bunge la Katiba linaweza kujikuta linatumia fedha nyingi na muda na mwisho likakwama kwenye suala la Muundo wa Muungano kwenye sura ya sita ya rasimu ya Katiba. Lakini hili peke yake si sababu kubwa ya mimi kupendekeza kuwa kabla ya kwenda mbali na kupitia vifungu vingine vya rasimu hiyo wajumbe waamue kwanza suala la muundo wa Muungano kwanza. Kuna sababu moja kubwa.
Rasimu ya Katiba ilivyo sasa imeandikwa na kupangwa ikiwa imedhania (assume) kuwa kutakuwepo na Serikali tatu. Kwamba Ibara zake nyingi na muundo wake umefikiria kuwa Bunge la wananchi watakubali uwepo wa serikali tatu na kuridhia mfumo wa Shirikisho lenye nchi mbili na serikali tatu Serikali ya Tanganyika, Serikali ya Zanzibar na Serikali ya Muungano.
Kutokana na ukweli huo basi suala la uwepo wa Tanganyika na vyombo vyake vya kiutawala Mahakama, Baraza la Wawakilishi, Waziri Mkuu (Rais wake) ni la muhimu zaidi kuliko kuendelea na mchakato huu ulivyo sasa. Bunge halipaswi kuendelea na kupitia vifungu vingine vya rasimu bila kuamua kwanza aina ya muundo wa Muungano kama ni Serikali Mbili, Moja au Tatu kama inavyopendekezwa.
Pande Mbili Zinazokinzana
Hadi hivi sasa ni wazi kuwa upo upande mmoja unaotaka kuendelea kwa mfumo wa Serikali Mbili na wapo wale ambao wanapendekeza mfumo wa Serikali Tatu. Sasa, vyovyote itakavyokuwa kuna matokeo mawili yanayowezekana:
Moja, Wanaotaka Serikali mbili wengi wakiwa ni wana CCM wakashinda na hivyo rasimu ya Katiba ni LAZIMA ifanyiwe marekebiso makubwa na Bunge la Katiba ili kuondoa vipengele vinavyozungumzia muundo wa serikali tatu;
Pili, wanaotaka Serikali Tatu wapo wana CCM na wapinzani wakashinda na hivyo rasimu ya Katiba kuweza kuendelea bila mabadiliko makubwa ya kimuundo. Hata hivyo kukubalika kwa serikali tatu kutalazimisha mchakato huu wa Katiba ulilvyo sasa usitishwe kwani kwa maoni yangu na kwa unyenyekevu nayatoa Bunge hili Maalum la Katiba halipaswi kujadili rasimu ya Katiba ya Muungano bila wawakilishi kutoka vyombo na wananchi wa Tanganyika.
Nini kifanyike basi?
Naamini kuendelea na mchakato huu ulivyo sasa bila kuamua masuala haya makubwa ni kujaribu kukwepa kiini cha mgogoro. Wajumbe hawawezi kuendeleea kujadili mambo mengine kabla ya kuamua aina ya Muungano utakaokuwepo; kama utakuwepo. Naamini na napendekeza kuwa waamue kwanza suala la muundo wa Muungano kwani ni kutoka hapo ndiyo mambo mengine yataeleweka.
Napendekeza.

- Baada ya Mwenyekiti na Makamu wake kupatikana na wajumbe wote kuapishwa na baada ya taratibu zote za mwanzo kuwa tayari basi badala ya kuanza kupitia ibara za kwanza za Katiba ambazo hazina utata sana napendekeza wajumbe waende moja kwa moja kwenye moyo wa rasimu Muundo wa Muungano. Hili liamuliwe kabla kwenda kuamua mambo mengine kama ni serikali mbili au tatu lijulikane mapema kwani ibara nyingine zote (ukiondoa zile za mwanzo) zinasimama na kuanguka na Sehemu ya Sita ya rasimu ya Katiba.
- Endapo itapitishwa Serikali Tatu basi Bunge la Katiba lisitiswe kwa muda (indefinitely) hadi pale ambapo Tanganyika itakapokuwa na Katiba yake, Bunge lake na wawakilishi wake ambao wataingia kwenye Bunge la Katiba. Ikumbukwe hadi hivi sasa hakuna wawakilishi wa Tanganyika wa aina yoyote wakati Zanzibar ina wawakilishi wake.
- Baada ya Bunge Maalum kuridhia uwepo wa Serikali ya Tanganyika basu Bunge la kawaida liitishwe mara moja na kufanyia marekebiso Katiba ya sasa chini ya Ibara ya 98 ili kuruhusu kuundwa kwa serikali ya Tanganyika na vyombo vyake; mabadiliko hayo ya Katiba yaridhiwe na Baraza la Wawakilishi kwa mujibu wa Katiba.
- Mabadiliko hayo ya Katiba ya sasa yaweke utaratibu wa wananchi wa Tanganyika kutunga Katiba yao na kufanya uchaguzi wao mkuu ili kujipatia viongozi wake wa kitaifa na wawakilisi; uchaguzi huo ufanyike mapema mwakani ambapo viongozi wote wa kitaifa watapatikana wakiwemo wa Bunge wa Bunge la Tanganyika (sijui litaitwa Baraza la Wawakilishi au Seneti sijui)
- Wakati wananchi wa Tanganyika wanafanya mchakato wa kurudisha serikali yao na vyombo vyake vyote (pamoja na alama zake za kitaifa, wimbo wa taifa, bendera n.k) Mchakato wa Katiba Mpya wa hivi sasa utakuwa umesitishwa.
- Baada ya Serikali ya Tanganyika kurudi basi suala kubwa la kwanza ambalo litahitaji kuamuliwa ni kama tunahitaji kuendelea kuwa Muungano. Hili litafanyika kwa kupigwa kwa kura ya maoni pande mbili za Muungano na endapo kila upande utapata angalau asilimia 60 ya wapiga kura kukubali Muungano basi hatua za kuendelea kuandika Katiba Mpya itabidi zifuatwe; kinyume chake utaratibu wa utengano ufanyike ili hatimaye kupatikane mataifa mawili jirani ambayo yatakuwa na uhuru kamili yakidumisha ushirikiano wa kimataifa wan chi jirani.
- Endapo wananchi wa Tanganyika na Zanzibar watataka uwepo Muungano basi Baada ya Serikali ya Tanganyika kurudi na kuanza kazi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atavunja Baraza la Mawaziri la sasa na kuzingatia mabadiliko yale ya Katiba (namba 3 hapo juu) kuingiza katika Serikali ya Muungano wa wakilishi kutoka Serikali ya Tanganyika kwa ajili ya masuala ya Muungano na hivyo kupunguza ukubwa. Hili linaweza kuwa rais kufanyika chini ya Rais Kikwete ambaye atasimamia serikali ya mpito kuelekea uundwaji wa Katiba Mpya na Uchaguzi Mkuu Mpya mwishoni mwa mwaka 2015.
- Kama kutakuwa na Muungano wa Serikali tatu basi Bunge Maalum la Katiba liitwe wakati Sheria yake ikiwa imefanyikwa mabadiliko makubwa ya kimfumo ili liakisi uwepo wa Serikali na Wawakilishi kutoka Tanganyika na kutoka hapo mchakato wa Katiba Mpya Muungano uanze upya ili kuhakikisha Katiba Mpya inapatikana kwa njia nzuri zaidi.