Njia za kudhibiti ukatili baina ya dada wa kazi za nyumbani (house girl) na mwajiri wake

Angyelile99

Member
Joined
Oct 9, 2023
Posts
89
Reaction score
164
Utangulizi
lengo la nakala hii ni kutoa ushauri haswa kwa serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania dhidi ya namna gani tunaweza kupambana na vitendo vya ukatiri ulio shamiri kwa sasa katika maeneo tofauti tofauti dhidi ya dada wa kazi za nyumbani kwa familia wanazo zifanyia kazi. Mpaka ivi sasa kumekua na matukio ya kikatiri baina ya dada wa kazi za nyumbani (house girls) pamoja na familia wanazo zitumikia.

Matukio haya yamekua yakihusishwa kwa namna tofauti tofauti, aidha dada wa kazi kufanyiwa ukatiri ikiwemo vipigo, kuto pewa stahiki zake na kwa wakati ulio kwanye makubariano, pia kuto pewa haki zake za kimsingi kama mmoja ya wanafamimia, matumizi ya lugha mbaya dhidi yao kutoka kwa waajili wao pamoja na uwepo wa kesi za kimausiano ya mapenzi hali ambayo uperekea migogoro ya familia kati yao.

Lakini kwa upande wa pili pia kumekua na matukio mbali mbali ambayo yamekua yakifanywa na dada wa kazi katika familia wanazo zitumikia, ambayo hayakubariki katika jamii ikiwemo kunyanyasa watoto wanao achiwa na wazazi, vipigo kwa watoto, uchafu wa makusudi, pengine mpaka kufanya majaribio ya kutaka kutoa uhai wa watoto.

Sasa kwa mantiki hiyo hii ni moja kati ya ukatiri unao fanywa kwa dada wa kazi za ndani na ni moja kati ya sababu zinazo perekea dada wa kazi kua na fikra hasi dhidi ya familia za anayo itumikia.

Nini kifanyike
Je, nini kifanyike, ama ni mfumo gani sahihi ambao serikali inaweza kutumia ili kukomesha na kudhibiti kwa asilimia kubwa vitendo hivi vya kikatiri baina ya dada wa kazi na familia wanazo zitumikia. Kwa kuzingatia hoja zilizo elezewa hapo chini. Ni moja ya njia ambazo serikali kupitia wizara ya maendeleo ya jamii, Waze, jinsia na watoto inaweza fanya ili kupambana na hali hii iliyo kithiri kwa hali ya juu sasa.

1. Uundaji wa rejista ya kitaifa ya dada wa kazi za nyumbani - Serikali inapaswa kuunda mfumo au rejista ya kitaifa ambayo itasajili akina dada wote wanaofanya kazi za nyumbani, ikiwemo majina, umri, taaluma, maeneo wanaofanyia kazi, maeneo aliko toka, n.k. Hii itasaidia kudhibiti na kufuatilia hali yao.
Namna ya rejista (Usajiri)

Kuwekwe utaratibu kupitia ofisi ya raisi tawara za mikoa na serikali za mitaa. Ambapo sasa maafisa tarafa kwa kushirikiana na watendaji wa kata watakua na jukumu la kufatiria kila kaya inayo miliki dada wa kazi ili kuweza kukusanya taalifa ambazo zitakua sehemu ya taalifa za rejista. Taarifa hizi zita ambatana na kujengwa kwa uhusiano baina ya mtendaji ( mwakilishi wa serikali) dada wa kazi pamoja na bosi wa dada huyo ili kuwepo na uraisi wa utoaji wa taalifa, pale kunapo kua na changamoto baina ya mwajili na mwajiliwa.

2. Kuweka sheria na kanuni elekezi za ajira kwa dada wa kazi za nyumbani - Serikali inapaswa kuanzisha sheria na kanuni za kuzingatia katika ajira za dada hawa, ikiwemo masharti ya mshahara, malazi, chakula, muda wa kazi, likizo n.k. Hii itaondoa ukatili na kuongeza haki zao.

3. Kuanzisha mfumo wa usimamizi na ukaguzi - Serikali inapaswa kuanzisha mfumo imara wa ukaguzi na usimamizi wa dada hawa, ikiwepo uteuzi wa maafisa/wakaguzi, ama chama hai cha wafanya kazi za ndani kwa kila wilaya ili kuhakikisha masharti ya sheria zinafuatwa. Changamoto za wafanyakazi hao ama za waajili wao zinasikirizwa na kutekerezwa kwa ufanisi.

4. Uwepo wa vikao/ mikutano baina ya maafisa kata na wafanya kazi za ndani katika vipindi tofauti tofauti. Kama ilivyo kawaida kwa taasisi mbali mbali kua na mikutano ya pamoja kati ya waajili na waajiliwa pia hii inaweza kufanyika kati ya serikali kupitia maafisa kata na wafanya kazi wa kazi za ndani kwa kufuatiwa na uwepo wa wa wakilishi wao kutoka katika vyama vyao viliivyo undwa. Hii inaweza kusaidia kwa namna moja hama nyingine kujua namna watu hawa wanavo ishi na waajili wao, changamoto wanazo kutana nazo. Na kusaidiana kimawazo namna ya kutatua

5. Kuhamasisha na kutoa elimu kwa jamii - Ni muhimu kwa serikali kushirikiana na taasisi mbalimbali kutoa elimu kwa familia zinazo ajiri dada hawa kuhusu haki na wajibu wao. Kupitia vyombo vya habari ma kwa kuanzinza kampeni mbali mbali zoezi hili linaweza kukamirika

Nani wa kusimamia sheria hizi na mwenye majukumu ya ukaguzi
Bado swara la usimamizi wa namna gani sheria zilizo wekwa zinatekerezwa na ni nani wa kufatiria maisha kati ya dada hawa wa kazi na familia wanazo ishi nazo. Pia maafisa tarafa pamoja na watendaji wa kata na mitaa, wanaweza Kua ndo kiunganishi cha moja kwa moja ili kuweza kusaidia serikali katika namna ya kupambana na vitendo hivi vya ukatiri.

Faida zinazo weza jitokeza katika ukamilishwaji wa mchakato huu

1. Kuondoa ukatili na kukuza haki za wafanyakazi: Mfumo huu utaimarisha usimamizi na ulinzi wa haki za dada wa kazi za nyumbani, ikiwemo kuondoa vitendo vya ukatili. Familia zitawajibika kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa.

2. Kuimarisha uwajibikaji wa familia: Usajili wa wafanyakazi na wajumbe wa familia utasaidia kuongeza uwajibikaji wa familia wanaowajiri dada wa kazi. Familia zitakuwa na jukumu la kujilinda na kuwalinda wafanyakazi wao.

3. Kuboresha mazingira ya kazi na maisha: Mfumo huu utawezesha kuboresha masharti ya ajira, ikiwemo malazi, chakula, muda wa kazi na likizo. Dada wa kazi za nyumbani watakuwa na mazingira bora ya kufanyia kazi na kuishi. Hii utaweza kuondoa migogoro inayo weza kupelekea fikria potofu kwa dada wa kazi dhidi ya familia anayo ifanyia kazi ikidhaniwa Kua ni sehemu ya maripizo

4. Kuongeza uwazi na uwajibikaji: Mfumo huu utaongeza uwazi na uwajibikaji katika sekta hii ya wafanyakazi wa nyumbani. Taarifa za wafanyakazi na familia zitakuwa wazi na rahisi kufikia. Ambapo pia utaweza kurahisisha kwa miliki wa mfanya kazi huyoo kua na taalifa za ndani zaidi kuhusu binti anae mfanyia kazi.

5. Ukusanyaji wa taarifa sahihi: Mfumo huu utawezesha ukusanyaji wa taarifa sahihi za wafanyakazi na mahitaji yao. Serikali itaweza kutathmini kiwango cha ukatili na kukuza usimamizi bora. Kwa ujumla. Serikali ni taasisi ambayo imepewa dhamana ya kusimamia wananchi wote kwa ujumla. Lakini pia ili iweze Kua na utendaji kazi ulio tukuka.

Pia kunauhusiano mkubwa na uwepo wa ushirikiano na wananchi kupitia jamii zao wanazo ishi. Hivo basi kunahaja ya jamii kua kipao mbele katika kukomesha vitendo vya kikatiri vinavyo endelea baina ya wafanya kazi wa ndani na mabosi zao, ambavyo vimepeleka uwepo wa sito fahamu baina ya makundi haya mawili. Utoaji wa taalifa za kinyanyasaji kwenye ofisi zenye mamlaka ni muhimu zaidi ikiwa ni sehemu ya utekerezwaji wa kampeni hii ya kukomesha ukatiri katika familia zinazo miliki dada wa kazi.
 
Utangurizi:
lengo la nakala hii ni kutoa ushauri haswa kwa serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania dhidi ya namna gani tunaweza kupambana na vitendo vya ukatiri ulio shamiri kwa sasa katika maeneo tofauti tofauti dhidi ya dada wa kazi za nyumbani kwa familia wanazo zifanyia kazi. Mpaka ivi sasa kumekua na matukio ya kikatiri baina ya dada wa kazi za nyumbani ( house girls) pamoja na familia wanazo zitumikia.

Matukio haya yamekua yakihusishwa kwa namna tofauti tofauti, aidha dada wa kazi kufanyiwa ukatiri ikiwemo vipigo, kuto pewa stahiki zake na kwa wakati ulio kwanye makubariano, pia kuto pewa haki zake za kimsingi kama mmoja ya wanafamimia, matumizi ya lugha mbaya dhidi yao kutoka kwa waajili wao pamoja na uwepo wa kesi za kimausiano ya mapenzi hali ambayo uperekea migogoro ya familia kati yao.

Lakini kwa upande wa pili pia kumekua na matukio mbali mbali ambayo yamekua yakifanywa na dada wa kazi katika familia wanazo zitumikia, ambayo hayakubariki katika jamii ikiwemo kunyanyasa watoto wanao achiwa na wazazi, vipigo kwa watoto, uchafu wa makusudi, pengine mpaka kufanya majaribio ya kutaka kutoa uhai wa watoto.

Sasa kwa mantiki hiyo hii ni moja kati ya ukatiri unao fanywa kwa dada wa kazi za ndani na ni moja kati ya sababu zinazo perekea dada wa kazi kua na fikra hasi dhidi ya familia za anayo itumikia.

Nini kifanyike
Je nini kifanyike, ama ni mfumo gani sahihi ambao serikali inaweza kutumia ili kukomesha na kudhibiti kwa asilimia kubwa vitendo hivi vya kikatiri baina ya dada wa kazi na familia wanazo zitumikia. Kwa kuzingatia hoja zilizo elezewa hapo chini. Ni moja ya njia ambazo serikali kupitia wizara ya maendeleo ya jamii, Waze, jinsia na watoto inaweza fanya ili kupambana na hali hii iliyo kithiri kwa hali ya juu sasa.

1. Uundaji wa rejista ya kitaifa ya dada wa kazi za nyumbani - Serikali inapaswa kuunda mfumo au rejista ya kitaifa ambayo itasajili akina dada wote wanaofanya kazi za nyumbani, ikiwemo majina, umri, taaluma, maeneo wanaofanyia kazi, maeneo aliko toka, n.k. Hii itasaidia kudhibiti na kufuatilia hali yao.
Namna ya rejista (Usajiri)

Kuwekwe utaratibu kupitia ofisi ya raisi tawara za mikoa na serikali za mitaa. Ambapo sasa maafisa tarafa kwa kushirikiana na watendaji wa kata watakua na jukumu la kufatiria kila kaya inayo miliki dada wa kazi ili kuweza kukusanya taalifa ambazo zitakua sehemu ya taalifa za rejista. Taarifa hizi zita ambatana na kujengwa kwa uhusiano baina ya mtendaji ( mwakilishi wa serikali) dada wa kazi pamoja na bosi wa dada huyo ili kuwepo na uraisi wa utoaji wa taalifa, pale kunapo kua na changamoto baina ya mwajili na mwajiliwa.

2. Kuweka sheria na kanuni elekezi za ajira kwa dada wa kazi za nyumbani - Serikali inapaswa kuanzisha sheria na kanuni za kuzingatia katika ajira za dada hawa, ikiwemo masharti ya mshahara, malazi, chakula, muda wa kazi, likizo n.k. Hii itaondoa ukatili na kuongeza haki zao.

3. Kuanzisha mfumo wa usimamizi na ukaguzi - Serikali inapaswa kuanzisha mfumo imara wa ukaguzi na usimamizi wa dada hawa, ikiwepo uteuzi wa maafisa/wakaguzi, ama chama hai cha wafanya kazi za ndani kwa kila wilaya ili kuhakikisha masharti ya sheria zinafuatwa. Changamoto za wafanyakazi hao ama za waajili wao zinasikirizwa na kutekerezwa kwa ufanisi.

4. Uwepo wa vikao/ mikutano baina ya maafisa kata na wafanya kazi za ndani katika vipindi tofauti tofauti. Kama ilivyo kawaida kwa taasisi mbali mbali kua na mikutano ya pamoja kati ya waajili na waajiliwa pia hii inaweza kufanyika kati ya serikali kupitia maafisa kata na wafanya kazi wa kazi za ndani kwa kufuatiwa na uwepo wa wa wakilishi wao kutoka katika vyama vyao viliivyo undwa. Hii inaweza kusaidia kwa namna moja hama nyingine kujua namna watu hawa wanavo ishi na waajili wao, changamoto wanazo kutana nazo. Na kusaidiana kimawazo namna ya kutatua

5. Kuhamasisha na kutoa elimu kwa jamii - Ni muhimu kwa serikali kushirikiana na taasisi mbalimbali kutoa elimu kwa familia zinazo ajiri dada hawa kuhusu haki na wajibu wao. Kupitia vyombo vya habari ma kwa kuanzinza kampeni mbali mbali zoezi hili linaweza kukamirika

Nani wa kusimamia sheria hizi na mwenye majukumu ya ukaguzi
Bado swara la usimamizi wa namna gani sheria zilizo wekwa zinatekerezwa na ni nani wa kufatiria maisha kati ya dada hawa wa kazi na familia wanazo ishi nazo. Pia maafisa tarafa pamoja na watendaji wa kata na mitaa, wanaweza Kua ndo kiunganishi cha moja kwa moja ili kuweza kusaidia serikali katika namna ya kupambana na vitendo hivi vya ukatiri.

Faida zinazo weza jitokeza katika ukamilishwaji wa mchakato huu

1. Kuondoa ukatili na kukuza haki za wafanyakazi: Mfumo huu utaimarisha usimamizi na ulinzi wa haki za dada wa kazi za nyumbani, ikiwemo kuondoa vitendo vya ukatili. Familia zitawajibika kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa.

2. Kuimarisha uwajibikaji wa familia: Usajili wa wafanyakazi na wajumbe wa familia utasaidia kuongeza uwajibikaji wa familia wanaowajiri dada wa kazi. Familia zitakuwa na jukumu la kujilinda na kuwalinda wafanyakazi wao.

3. Kuboresha mazingira ya kazi na maisha: Mfumo huu utawezesha kuboresha masharti ya ajira, ikiwemo malazi, chakula, muda wa kazi na likizo. Dada wa kazi za nyumbani watakuwa na mazingira bora ya kufanyia kazi na kuishi. Hii utaweza kuondoa migogoro inayo weza kupelekea fikria potofu kwa dada wa kazi dhidi ya familia anayo ifanyia kazi ikidhaniwa Kua ni sehemu ya maripizo

4. Kuongeza uwazi na uwajibikaji: Mfumo huu utaongeza uwazi na uwajibikaji katika sekta hii ya wafanyakazi wa nyumbani. Taarifa za wafanyakazi na familia zitakuwa wazi na rahisi kufikia. Ambapo pia utaweza kurahisisha kwa miliki wa mfanya kazi huyoo kua na taalifa za ndani zaidi kuhusu binti anae mfanyia kazi.

5. Ukusanyaji wa taarifa sahihi: Mfumo huu utawezesha ukusanyaji wa taarifa sahihi za wafanyakazi na mahitaji yao. Serikali itaweza kutathmini kiwango cha ukatili na kukuza usimamizi bora.
Kwa ujumla. Serikali ni taasisi ambayo imepewa dhamana ya kusimamia wananchi wote kwa ujumla. Lakini pia ili iweze Kua na utendaji kazi ulio tukuka.

Pia kunauhusiano mkubwa na uwepo wa ushirikiano na wananchi kupitia jamii zao wanazo ishi. Hivo basi kunahaja ya jamii kua kipao mbele katika kukomesha vitendo vya kikatiri vinavyo endelea baina ya wafanya kazi wa ndani na mabosi zao, ambavyo vimepeleka uwepo wa sito fahamu baina ya makundi haya mawili. Utoaji wa taalifa za kinyanyasaji kwenye ofisi zenye mamlaka ni muhimu zaidi ikiwa ni sehemu ya utekerezwaji wa kampeni hii ya kukomesha ukatiri katika familia zinazo miliki dada wa kazi.

Huu si mkakati mwingine tu katika kuyasaka yale yanayoitwa kuwa mapato zaidi ya serekali?

GTFZt9qXIAAtaj0.jpeg
 
Back
Top Bottom