Njia za kufungua NGO's

evance hubert

Member
Joined
Oct 14, 2012
Posts
36
Reaction score
20
Wanajukwaa kwa yeyote anaye fahamu njia za kufungua NGO's kuanzia hatua ya kwanza mpaka ya mwisho ninge waomba Sana msaada wenu.
 
Wanajukwaa kwa yeyote anaye fahamu njia za kufungua NGO's kuanzia hatua ya kwanza mpaka ya mwisho ninge waomba Sana msaada wenu.

Kwanza ni lazima uwe na majibu ya maswali yafuatayo:
*Scope:Unataka iwe ktk ngazi ya Wilaya,Taifa au ya Kimataifa?
*Thematic area:Unataka isaidie nyanya ipi? Elimu,Afya,Mazingira nk
*Location:Utaifungua wapi? Wilaya ipi,mkoa gani au nchi gani?
*Founder members: Waanzilishi wasiopungua 10 wakiwemo viongozi ukizingatia jinsia;
*Constitution:Katiba ya shirika andaa nakala 3;
*Stamp Duty:Stempu ya Serikali:
*Cv:Maelezo binafsi ya viongozi 3.Mwenyekiti,Katibu na Mhazini na picha zao za pasport size;
*Office:Ofisi halisi,yaani "Physical Office&Address"
*Ukikamilisha nenda Wizarani kisajili na pesa taslim kama Laki 1 gharama za kusajiri na kopi nk.
*Wizara ya mambo ya ndani au Wizara ya Maendeleo ya jamii,jinsia na watoto kulingana na aina ya shirika lako na kazi zake.

Hapo utasubiri kipindi kisichopungua wiki 2-3 ili kupata majibu ya maombi yako.Kunaweza kuwa na marekebisho au lah! Ndani ya mwezi mmoja utakuwa na shirika lako tayari.Ni muhimu pia latika kipindi hicho ukafungua pia akaunti ya benki na kuweka utaratibu wa kuiendesha ambao baadhi ya maelekezo ni lazima yatakuwa katika Katiba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…