Njia za kuishinda hofu ya kupitia kipindi kigumu sana kifedha

Manyanza

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
16,464
Reaction score
35,629
Kila mtu huwa yupo na hofu ya kupitia kipindi kigumu sana kifedha.Watu maarufu yaani "Celebrity" na watu wenye fedha nyingi sana kama bilionea huwa wanaishi kwa "Stress" sana kuliko kundi lolote la binadamu ulimwenguni hasa linapokuja suala la hofu ya kupitia kipindi kigumu sana kifedha.

Hii inachangiwa na upweke kupita kiasi ambao watu maarufu yaani "Celebrity" na watu wenye fedha nyingi sana kama bilionea wanapitia kutokana na kuzungukwa na watu wengi ambao wapo kimaslahi zaidi kuliko kujali utu wao kama binadamu wengine.

Badala ya kuhofia nini fulani atasema juu yako pale ambapo unapitia kipindi kigumu sana kifedha unatakiwa kujiuliza juu ya umuhimu wa mtu husika katika maisha yako ya kila siku.

Kama hana umuhimu wowote kwa maana ukiugua, ukipata ajali,ukiwa na madeni n.k hauwezi kumshirikisha kwa chochote basi hakuna sababu ya kuhofia nini atasema au kuongea juu yako kwa sababu maoni yake hayana umuhimu wowote maishani mwako.

Hivyo leo tuangalie njia za kukabiliana na hofu ya kupitia kipindi kigumu sana kifedha.
Kabla ya kujua njia hizo 6 , tuangalie kwanza vyanzo vya kupitia kipindi kigumu sana kifedha,kisha tuangalie mabadiliko ya mwili kutokana na kupitia kipindi kigumu sana kifedha kisha tuangalie ufumbuzi wake.

SEHEMU YA KWANZA : VYANZO VYA KUPITIA KIPINDI KIGUMU SANA KIFEDHA
Mtu yeyote anaweza kupitia kipindi kigumu sana kifedha kwa vyanzo vitatu vifuatavyo

1.KUINGIZA FEDHA KIDOGO SANA KWA MWEZI
Mtu yeyote anaweza kupitia kipindi kigumu sana kifedha kwa sababu ya kuingiza fedha kiasi kidogo sana kwa mwezi.Vyanzo vya kuingiza fedha kiasi kidogo sana kwa mwezi ni
#Kipato cha mwezi kupungua ghafla,kudaiwa fedha nyingi sana,kukosa ajira au kukosa kazi ya uhakika,kulipwa fedha kidogo sana kwenye ajira au kibarua, biashara kuingiza fedha kidogo sana, kufukuzwa kazi, kufilisika, gharama za maisha kuongezeka sana bila kipato kuongezeka,

#kustaafu bila maandalizi, kucheleweshewa mishahara au posho,watu kukopa fedha zako nyingi sana lakini hawarudishi,talaka au kutengana na mwenza wako ambaye unamtegemea kifedha.

2.KUTUMIA FEDHA NYINGI SANA KWA MWEZI
Mtu mwengine anaweza kupitia kipindi kigumu sana kifedha kwa sababu ya kutumia fedha nyingi sana kwa mwezi.
Haijalishi utakuwa unaingiza kiasi kikubwa sana cha fedha kwa mwezi kama unatumia fedha nyingi sana kwa mwezi lazima utapitia kipindi kigumu sana kifedha.

Vyanzo vya kupitia kipindi kigumu sana kifedha kwa kututumia fedha nyingi sana ni
#Kusomesha watoto shule au chuo cha gharama kubwa sana, kuhudumia familia yenye watu wengi sana,kuishi maisha ya kifahari sana, kuzungukwa na idadi kubwa sana ya watu tegemezi kwako

#Kuwa na uraibu wa pombe kupindukia,kuhonga wanawake, kucheza kamari,kuvuta bangi,kutumia dawa za kulevya,kutumia fedha nyingi sana ghafla,kufanya starehe sana,kufunga ndoa ya kifahari sana,mwenza wako kutumia fedha zako nyingi sana bila ridhaa yako,

#Kuishi bila bajeti, kuchukua mikopo umiza,kufanya biashara ambayo hauna ujuzi nayo, kukamatwa na biashara haramu,kujiunga kwenye biashara ambayo haujui uendeshaji wake (Ponzi scheme),Kuzaa au kuoa bila maandalizi

3.DHARURA ZENYE KUATHIRI KIPATO CHAKO
Unaweza kupitia kipindi kigumu sana kifedha kwa sababu za matukio mbalimbali ya ghafla ambayo hukujiandaa kukabiliana nayo kama vile
#Ajali yenye kusababisha ulemavu wa kudumu,ajali yenye kusababisha uharibifu wa mali zako kama fenicha, vyombo vya moto,vifaa vya kielektroniki n.k

#Kuibiwa fedha, kudhulumiwa, kutapeliwa, kuvamiwa na majambazi,kupata kesi, safari za ghafla, kampuni kupunguza wafanyakazi ghafla, akaunti za benki kuzuiwa kutoa fedha.

MABADILIKO YA MWILI PALE AMBAPO UNAPITIA KIPINDI KIGUMU SANA KIFEDHA
Kama unapitia kipindi kigumu sana kifedha utaona mabadiliko yafuatayo mwilini mwako
-Utapata mshtuko,moyo kuuma sana, moyo kwenda mbio, miguu kuishiwa nguvu, kizunguzungu, kichefuchefu, kuchanganyikiwa, hasira, tumbo kuvurugika, kujichukia, kujikosoa, kujilaumu, kujuta, kutamani kujiua,kuanza kulia

-Kichwa kitauma sana, utapoteza hamu ya kula au utakula vyakula bila mpangilio,utakosa nguvu za kutoka kitandani, utapoteza hisia za mapenzi

-Utaona ukungu, kupumua haraka haraka sana,kifua kitauma sana,mwili utakufa ganzi, kuumia begani na shingoni, kutetemeka sana,kujiona mzee sana,kujiona mgonjwa,kuona aibu,kujiona kichekesho,kuhofia upweke,kuhofia kufa ghafla, kujiona upo hatarini muda wote.

Zifuatazo ni njia za kukabiliana na kipindi kigumu sana kifedha

1.HAUWEZI KUMRIDHISHA KILA MTU
Haijalishi utakula nini, uvae nguo gani, uishi nyumba gani, utumie usafiri gani,utumie simu gani,utumie fenicha gani,uishi mji gani baadhi ya watu watakuona mshamba,watakuona lofa masikini wa kutupwa,wapo watakuona umechanganyikiwa, wapo watakuona dhaifu,wapo watakuona hauna hadhi ya kuzungumza nao,wapo watakuona haujielewi,wapo watakuona unaishi maisha magumu sana hata kama utakuwa unajiona umepiga hatua kubwa sana kiuchumi.

Vilevile zingatia baadhi ya watu watakuwa na kitu ambacho hauna,baadhi ya watu watakuwa na fedha nyingi sana zaidi yako haijalishi utakuwa umepiga hatua kubwa kiasi gani,baadhi ya watu watakuwa na muonekano mzuri zaidi yako hata ukijiona umependeza sana,

Hakuna kitu chochote ambacho kinaweza kukufanya uwe juu ya watu wote ulimwenguni.

Kila mtu atakuwa na maoni yake juu yako,kila mtu anatamani kitu cha tofauti juu yako.
Watu wataona uwe na nguo tofauti,utumie simu tofauti,utumie usafiri tofauti,uishi nyumba tofauti,uishi mji tofauti,ufanye "shopping" sehemu tofauti,likizo uende sehemu tofauti na matarajio yako.Hali hiyo itatokea ukiwa na fedha nyingi sana au ukiwa hauna fedha kabisa.
Zingatia kwamba haijalishi utakuwa na fedha nyingi kiasi gani bado jumla ya fedha zako zote na mali zako zote itakuwa sawasawa na mchango wa hisani wa mtu mwengine kwa watu wenye uhitaji maalum.

2.WEKA MIPAKA YA MATUMIZI YA FEDHA
Weka mipaka ya matumizi yako ya fedha.Hakuna kiwango cha fedha ambacho unaweza kutumia au kumpa mtu mwengine atumie ambacho kiasi hicho cha fedha kinaweza kumaliza matatizo yake yote hapa ulimwenguni.

Kwa asili binadamu hawezi kuridhika na kitu chochote - leo akipata 200 kesho anataka 400,kisha 800,kisha 1600 kwa maana mahitaji ya binadamu huongezeka kadiri kipato kinazidi kuongezeka.

Kwa mfano kama kuna mtu kila siku akija kwako kuomba fedha unampa ,hata kama tangu utotoni mwake umekuwa unampa fedha nyingi sana lakini siku akija kuomba fedha endapo ukisema hauna fedha atakuchukia sana kama vile haujawahi kumpa fedha zozote tangu utotoni mwake.

3.KESHO HAITABIRIKI
Kesho haitabiriki.Hakuna mtu yeyote mwenye guarantee ya kuishi kwa furaha hapa ulimwenguni.Hakuna maandalizi ambayo unaweza kufanya kwa 100% yakatoa guarantee ya kuishi kwa furaha saa 24.
Hakuna mtu ambaye anajua nani atapoteza kazi kesho, hakuna mtu ambaye anajua nani atapata ajali kesho, hakuna mtu ambaye anajua nani kesho atakuwa mheshimiwa na nani kesho atakuwa DHALILI kwenye jamii.

Kazi ambayo leo unaona aibu kuifanya kesho inaweza kukupa heshima katika jamii na kazi ambayo leo unaona inakupa heshima kesho inaweza kukufanya uonekane DHALILI kwenye jamii.

Mtu ambaye leo unamuona mzigo kesho anaweza kugeuka kimbilio lako na yule ambaye leo unamuona kimbilio lako kesho anaweza kugeuka mzigo kwako.

Yule ambaye leo unamuona faraja kwako ,kesho anaweza kukutoa machozi,na yule ambaye leo unamuona anakutoa machozi ,kesho anaweza kugeuka faraja yako.

Kile ambacho leo kipo na mwanzo mzuri kinaweza kumalizika na mwisho mbaya na kile ambacho leo unaona kimeanza na mwanzo mbaya ,kesho kinaweza kumalizika na mwisho mzuri.

4.MABADILIKO LAZIMA YATOKEE
Hakuna chenye kudumu milele (The impermanence of our lives)
Fedha zinakuja na kuondoka, umaarufu unakuja na kuondoka,fursa zinakuja na kuondoka,cheo kinakuja na kuondoka, mahusiano yanajengwa na kuvunjika,ajali zinatokea, vitu vyenye thamani vinapoteza thamani kwa vitu vipya kuzalishwa, umri unasogea, vifo vinatokea.

Mahusiano yako na wapendwa wako yanakwenda kubadilika.
Wapo mtaachana kwa ugomvi na wengine mtaachana bila ugomvi,

Wapo watahama makazi yao kwenda masomoni,kuoa au kuolewa miji tofauti, wapo watasafiri miji tofauti,wapo watapata kazi sehemu tofauti

Wapo watapoteza maisha katika umri mdogo sana na wengine umri mkubwa sana lakini watakufa na kuondoka ukiwa bado unawahitaji

5.KAMA KUNA KITU KIBAYA KINAWEZA KUTOKEA KITATOKEA NA HAIWEZI KUWA MWISHO WA ULIMWENGU
Unaweza kujawa na hofu kubwa sana kuhusu nini kinaweza kutokea kesho , lakini hakuna mtu yeyote ambaye anajua kesho italeta nini.
Hatujui kesho itakuja na fursa gani au balaa gani.
Kile ambacho leo unajenga hofu kubwa kwamba endapo kikitokea maisha yako yatakuwa HATARINI sana,kesho kinaweza kugeuka kuwa BARAKA kwako,na kile ambacho unaona kitakuwa BARAKA kwako ,kesho kinaweza kugeuka HATARI kwako.
Tukio ambalo unajenga hofu kubwa sana kwamba likitokea maisha yako yatakuwa HATARINI sana kesho linaweza kutokea kisha linageuka kuwa fursa mpya yenye kuandika historia mpya ya maisha yako na tukio ambalo unaamini endapo likitokea itakuwa FURSA kubwa sana kwako yenye kukufuta machozi na kufungua ukurasa mpya wa maisha yako , linaweza kutokea kama ambavyo unavyofikiria na kutarajia kisha linaweza kugeuka HATARI kwako yenye kukutoa machozi na kuzidisha maumivu, majonzi, simanzi na huzuni .
Kila jambo zuri linakuja na BALAA ndani yake na kila BALAA linakuja na HERI zake.

6.MATATIZO YANATOKEA KWA WATU WOTE ULIMWENGUNI
Kipato kuongezeka huwa kinakuja na matatizo mapya ambayo awali ulikuwa hauna na vilevile kipato kikipungua huacha matatizo mapya ambayo ulikuwa hauna hapo awali.

Fedha zinakuja na marafiki wapya na maadui wapya na vilevile zikiondoka zinaleta marafiki wapya na maadui wapya.

Kusemwa vibaya wanasemwa watu wote ulimwenguni,kutengwa wanatengwa watu wote ulimwenguni, kubaguliwa wanabaguliwa watu wote ulimwenguni.

Mwenza wako anaweza kuwa muaminifu au msaliti bila kujali kipato chako,ndugu zako wanaweza kukupenda au kukuchukia bila kujali kipato chako.

Unaweza kuvunja mahusiano yako na mwenza wako muda wowote ukiwa na fedha nyingi au hauna fedha kabisa

Unaweza kuugua sana ukiwa na fedha nyingi sana au hauna fedha kabisa.

Watoto wako wanaweza kuacha shule ukiwa na fedha nyingi sana au hauna fedha kabisa

Msiba unaweza kutokea kwa wapendwa wako ukiwa na fedha nyingi sana au hauna fedha kabisa.

Ajali zinaweza kutokea ukiwa na fedha nyingi sana au hauna fedha kabisa

Upweke unaweza kutokea ukiwa na fedha nyingi sana au hauna fedha kabisa

Watu kukuchafua inaweza kutokea ukiwa na fedha nyingi sana au hauna fedha kabisa

Watu kukuibia inaweza kutokea ukiwa na fedha nyingi sana au hauna fedha kabisa

Unaweza kupata kesi mahakamani ukiwa na fedha nyingi sana au hauna fedha kabisa

Watu wanaweza kukusaliti ukiwa na fedha nyingi sana au hauna fedha kabisa.
 
Sawa,

Ila ni afadhali kuwa na fedha kuliko kutokuwa nazo.

Kulilia ndani ya Mercedes siyo sawa na kulia huku unachapa mwendo kwa mguu juani, na njaa na kiu juu..
 
Nimepitia kipindi kigumu sana mkuu,. Sanaa tena saaana lakini walau nashukuru kuna watu wapo upande wangu sikuzote wakiwemo wazazi wangu wanahakikisha kwa namna yeyote ile nasimama tena na tena...
That's good for You. Endelea kuwa baraka kwa wengine pia.
 
Sawa,

Ila ni afadhali kuwa na fedha kuliko kutokuwa nazo.

Kulilia ndani ya Mercedes siyo sawa na kulia huku unachapa mwendo kwa mguu juani, na njaa na kiu juu..
Kila kitu ni mtazamo na namna vile unavyochukuklia mambo
 
Somo zuri sana
 
Back
Top Bottom