Manyanza
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 16,464
- 35,629
MADHARA YA KASHFA NA TUHUMA ZA UZUSHI
Madhara ya kashfa ni kwamba unaweza kufukuzwa kazi,kutengwa na familia pamoja na jamii, unaweza kupoteza ajira, unaweza kupoteza uaminifu katika jamii, unaweza kupoteza heshima yako kwenye jamii, mahusiano/ndoa kuvunjika ghafla, mauaji, umwagaji damu hasa taarifa zikipokelewa na mtu ambaye anakuwa na hasira za karibu. Kashfa inawezekana kusababisha mtu kujiua au kuua , kashfa inaweza kusababisha mtu kufungwa gerezani maisha
UFUMBUZI WAKE
Kashfa zipo za ukweli na zingine za uongo, Ikiwa ni kashfa za kweli unaweza kutumia kama kioo cha kuboresha tabia yako kwenye jamii na ikiwa ni uzushi kuna mambo ya kuzingatia
1.TUMIA KASHFA KUBORESHA MAISHA YAKO
Badala ya kuishi kwa kutia huruma na kunyenyekea Watu wengine unaweza kufanya yafuatayo
-Epuka kuishi kwa kutaka kumfurahisha kila mtu,epuka kujitesa kwa lengo la kubadilisha mtazamo wa watu wengine,jifunze kujitetea na kuzungumza kwa ufasaha sio kuanza kulia, kupiga magoti,kutia huruma na kutaka watu wakuonee hauna hatia kwa sababu kama watu ambao wamezusha kashfa wapo na SADISTIC PERSONALITY watakuwa na furaha sana kwa hali yako badala ya kukuonea huruma.
-Kama ufumbuzi wake ni kwenda mahakamani nenda ufungue kesi,kama ufumbuzi wake ni kuvunja mahusiano yako na mwenza wako au marafiki zako fanya hivyo
-Kama ufumbuzi wake ni kuhama makazi hama,kama ufumbuzi wake ni kuacha kazi fanya hivyo,kama ufumbuzi wake ni kuripoti taarifa kwa mwajiri au "superviser" wako fanya hivyo,
-kama ufumbuzi wake ni kuzipuuza taarifa fanya hivyo, kama ufumbuzi wake ni kujenga taswira nzuri kwenye jamii fanya hivyo.
Kashfa huwa zinakuja kutegemea na afya yako, uchumi, elimu,umri wako,hali ya kifamilia, umaarufu, Wadhifa, mamlaka, nguvu ya ushawishi hivyo kila mtu hali yake ipo tofauti.Angalia njia bora kulingana na hali yako.
2.KUWA MFANO BORA WA KUIGWA (BE A ROLE MODEL)
Kutoka KUDHARAULIKA mpaka KUHESHIMIKA hiyo iwe kauli mbiu yako kila uendapo.Unataka kuwa nani kama mfano bora ? Tumia kashfa kama nguvu ya kubadilisha historia yako yote kwa ujumla.
Zingatia kwamba hakuna kashfa mpya hapa ulimwenguni zote ni marejeo.
3.ZINGATIA KWAMBA: MAISHA HAYATAKUWA RAHISI KWAKO KWA SABABU TU NI MTU MWEMA SANA KATIKA JAMII
Haijalishi utakuwa muaminifu au msaliti, mchamungu au mshirikina, muongo au mkweli, mzee au kijana, mvivu au mchapakazi, msomi au haujafika shule, masikini au tajiri bado utakumbana na kashfa, tuhuma za uongo, kuzushiwa uongo na kadhia kwa mambo ambayo haujasema wala haujafanya
Ukiwa mstaarabu sana utazushiwa jambo lolote kwamba "usimuone anaonekana mstaarabu anafanya mambo 1,2,3 " yatakuwa ya uongo lakini sio mwisho wa ulimwengu.
Epuka kutaka uonekane mwema sana, mstaarabu sana, muaminifu sana, mnyenyekevu,mpole sana, mwenye huruma,mwenye kujali sana kwa sababu sifa hizo zitatumika kama UDHAIFU wako badala yake kemea tabia ambazo hauzipendi.
Jifunze kujitetea, jifunze kukemea utovu wa nidhamu kwa watu wengine.Ukiwa na rekodi nzuri jamii itakuwa ngumu sana kushawishiwa kwa kashfa za uongo,epuka kuonekana mwema kwa lengo la kuzuia kashfa na tuhuma
Acha watu huru wenye kukuona mwema watakuona na wenye kukuona mbaya watakuona mbaya bila kujali utafanya nini au kuongea kitu gani.