Manyanza
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 16,464
- 35,629
Sehemu hii inaweza kufanyiwa kazi na mwanaume Rijali kwa kuzingatia yafuatayo
Pata utulivu wa akili kwa kutumia njia za kuvuta pumzi (Deep breath),kupiga miayo mfululizo,kutoa hewa tumboni kuja nje (belly breathing)
Ufumbuzi wa matatizo/migogoro upo kama ifuatavyo
👇🏿
1.MIGOGORO BAINA YA MWENZA WAKO NA WAZAZI WAKO
Mwanaume Rijali ukiona ugomvi baina ya mwenza wako na wazazi wako mara nyingi anakuwa mama yako pamoja na dada zako fanya yafuatayo
👇🏿
Kama mama/dada zako wanamfokea, kumtukana, kumkashifu, kumkaripia,kumpiga,kumtishia mwenza wako na ukirejea nyumbani wanageuza kibao na kumsingizia mwenza wako ili umpige kisha wakutafutie mwenza mbadala labda wanadai mwenza wako hana uzazi,siyo kabila lako,hana adabu n.k fanya yafuatayo
👇🏿
Pata utulivu wa akili kisha zungumza "Mama/baba/dada yangu ninakuheshimu sana na ninakupenda sana,umenilea,umenitunza mpaka sasa nimepata mwenza -pamoja na hivyo ninkuomba mama/dada pale ambapo utaona au kusikia mwenza wangu amefanya makosa nipe taarifa mimi.
Nitamuonya mimi mwenyewe -Sipo tayari kuona mwenza wangu anakuwa sababu ya mimi na wewe kugombana na vilevile sipo tayari kuona mama/dada yangu unakuwa sababu ya mimi kugombana na mwenza wangu .
Wewe ni mtu muhimu sana kwangu na vilevile mwenza wangu ni mtu muhimu kwangu .Mwenza wangu hawezi kuchukua nafasi yako kwangu na vilevile wewe hauwezi kuchukua nafasi ya mwenza wangu kila mmoja akae nafasi yake"
Ukifanya uadilifu utaishi kwa upendo,amani na utulivu.
Kama utaegemea upande wa mama /dada zako utagombana na mwenza wako kisha wataleta mwanamke ambaye wao wanamtaka kisha utashindwa kudumu nae pia na vilevile kama utaegemea upande wa mwenza wako siku utagundua kwamba mwenza wako hana uaminifu wala ubinadamu haya kidogo utakosa nguvu za kuzungumza na mama/dada yako.
Mpe mama/dada zako nafasi ya kusimama SEHEMU yao na vilevile mpe mwenza wako nafasi ya kusimama kama Mwenza wako bila kuingilia mipaka .
Kwa upande wa mwenza wako kama umegundua mwenza wako huwa anawafokea, kuwatukana, kuwadhalilisha,kuwajibu kwa jeuri,kufanya dharau kwa lugha ya mwili (body language) ongea nae kama ifuatavyo
👇🏿
" Fulani (taja jina lake huku ukimtazama usoni) nakupenda sana,na ninakuheshimu sana,ninahitaji tuishi pamoja mpaka mwisho wa uhai pamoja na hivyo sipo tayari kuona unakuwa sababu ya mimi na mama/dada yangu kugombana na vilevile sipo tayari kuona mama/dada yangu anakuwa sababu ya mimi na wewe kugombana.
Endapo mama/dada yangu atakuwa amefanya makosa niambie mimi mwenyewe nitazungumza nae.
Wewe ni mtu muhimu kwangu na vilevile mama/dada yangu ni mtu muhimu sana kwangu.
Sipo tayari kutengana na mama/dada yangu kwa sababu yako na vilevile sipo tayari kuona mama/dada yangu anakuwa sababu ya mimi na wewe kutengana.Kila mmoja asimame sehemu yake bila kuingilia mipaka ya mtu mwengine."
2.MIGOGORO BAINA YAKO NA MWENZA WAKO
Kama mwanaume Rijali lazima tu utakumbana na vitimbi vya wanawake katika maisha yako hilo haliikwepeki haijalishi utakuwa mchamungu au mshirikina, muongo au mkweli, mwaminifu au msaliti, mlemavu au upo na viungo kamili, uwe tajiri au maskini, uwe msomi au haujafika shule, uwe kijana au mzee n.k bado vitimbi vya wanawake vipo palepale.
Kama ukiona mwenza wako anakufokea, kukutukana, kukudhalilisha hadharani, kukuita majina mabaya, kukugombeza, kukutoa dosari za muonekano wako, kukejeli juhudi zako,kukufanya ujione hauna hadhi ya kuishi nae,kukufanya ujione hauna akili timamu za kujiongoza na kumuongoza fanya yafuatayo.
Epuka kuomba msamaha, epuka kuanza kulia,epuka kumnyenyekea,epuka kumpa vitisho, epuka kumpa fedha.Badala yake simama imara na kufanya yafuatayo
Mwambie
"Fulani (taja jina lake huku ukimtazama usoni), nakupenda sana, na ninakuheshimu sana, ninahitaji tuishi pamoja mpaka mwisho wa uhai, pamoja na hivyo sipo tayari kuvumilia kauli au kitendo chochote chenye lengo la kunitoa utu wangu na kunivuniia heshima tambua kwamba siwezi kuvumilia kufokewa, kutukanwa, kudhalilishwa,kujibiwa vibaya,kukarapiwa, muonekano wangu kufanywa kichekesho.
Badala yake ninataka tuheshimiane na endapo ukiona nimefanya makosa niambie kwa lugha ya heshima wapi nimefanya makosa nitakuwa tayari kujirekebisha muda wowote lakini endapo kwa makusudi kabisa utafanya au kuongea kitu chochote chenye lengo la kunitoa utu wangu na kunivunjia heshima nitakuwa tayari kuvunja mahusiano baina yetu papohapo bila kujali muda ambao tumekaa pamoja au uwekezaji ambao nimefanya kwako "
Migogoro yenye kuhusisha fedha toa fedha kulingana na uwezo,kuhusu kuzaa asikupangie mtu yeyote kuhusu jinsia ya mtoto kuzaliwa.
Mwanaume Rijali anamlinda sana na kumtetea mwenza wake na kumtunza , kumheshimu wakati huohuo haonyeshi UDHAIFU kwa kumnyenyekea sana mwanamke kwa hofu ya kusalitiwa au kuachwa ghafla
Na wakati huohuo mwanaume Rijali hayupo tayari kuona mama/dada yake anaingilia mahusiano yake na mwenza wake badala yake anaweka mipaka imara kukemea utovu wa nidhamu kwa pande zote mbili bila kuegemea upande wowote .
Kama wewe ni mwanamke na unaona mwenza wako hana uwezo wa ku-balance mapenzi baina yako na wazazi wake tambua kwamba hiyo siyo mwanaume Rijali bali ni mvulana katika mwili wa mwanaume bila kujali umri wake upoje.