Njia za kukufanya uwe na nidhamu ya pesa

TEAM 666

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2017
Posts
4,399
Reaction score
8,594
Nilichojifunza kwenye makala ya wiki iliyopita ni kwamba wasomaji wangu wamekuwa na maswali yanayofanana juu ya ni jinsi gani wanaweza kutatua matatizo yao ya kifedha na bado wakafanikiwa?

Maswali hayo yaliegemea zaidi kwenye uwezo wa kuweka au kutunza fedha, namna ya kukwepa kupata madeni na jinsi ya kuepukana na mfumo wa kupata na kulipa bila kuwa na akiba.

Nilichojifunza katika maswali ya wengi ni kwamba chanzo cha yote hayo ni ukosefu wa nidhamu ya matumizi ya fedha.

68553fa45994eb5d5d714b14768f7615.jpg

UKOSEFU WA PESA SI TATIZO

Kujifunza kuwa na nidhamu linapokuja suala la pesa mara zote si kazi rahisi lakini ni lazima kama unataka kufanikiwa.

Watu wengi ukikutana nao watakueleza kwamba hawatengenezi pesa za kutosha lakini hata wakipewa pesa, kama wana tatizo la ukosefu wa nidhamu ya matumizi ya fedha hawatafanikiwa.

Kama nilivyosema, tatizo si pesa bali ni namna ya matumizi ya pesa zenyewe.

Katika kufunguana juu ya namna ya kutengeneza pesa katika kufikia lengo la kuwa tajiri, nitakupa njia za kukufanya uwe na nidhamu ya matumizi ya pesa unayopata hata kama ni kidogo kiasi gani.

Hapa tunajifunza jinsi ya mara zote tufanye nini ili kuwa kwenye mkondo sahihi wa matumizi ya pesa na kuanza kufanikiwa badala ya kuendelea kuwa kwenye mfumo uleule wa kila unachokipata unakitumia na kumaliza.

Yaani mfumo wa pesa kupita mikononi mwako kwenda kwingine.

Kwa nini unadhani unahitaji nidhamu ya matumizi ili ufanikiwe maishani? Nidhamu siyo neno tamu la kimapenzi au msamiati ambao kila mmoja wetu anaweza kuufurahia.

Baadhi ya watu wamezoea kupokea mishahara mwisho wa mwezi na kuutumia wote kwa siku moja au mbili kisha kujikuta mlemle kwenye msongo, maumivu ya kukata tamaa ya maisha na utumwa wa madeni.

Mfumo au utaratibu huu humjengea mtu duara la maisha ya kupata na kulipa. Mfumo huu hauwezi kwisha hadi utakapoamua kuwa na nidhamu itakayokuondoa kwenye maisha hayo na kuwa tofauti.

Mtu yeyote anaweza kujifunza na kuwa na nidhamu (hata wewe). Ni kiasi tu cha kuamua kubadilika na kuwa na mwenendo mpya wa matumizi ya fedha. Ukifanikiwa kubadilika, utashuhudia mabadiliko mazuri ya kipesa, utakuwa na pesa zaidi, utajikuta unaweka pesa zaidi na kujijengea ulinzi zaidi wa kiuchumi wa kwako na familia yako.

Njia hizo ni kama zifuatazo;

ZIELEWE PESA

Kama kweli unataka kufanikiwa na siku moja kufikia kwenye utajiri, ni muhimu mno kuzielewa pesa kama unataka kuwa na nidhamu ya pesa zenyewe.

Jitahidi kujisomea vitabu, mitandao, kuhudhuria semina na wakati mwingine kozi mbalimbali kuhusu matumizi binafsi, kujinasua kwenye madeni, kuwekeza kwa kuanza kidogokidogo na kadhalika.

Kwa kufanya hivyo, utajua unatakiwa uwe na tabia gani juu ya matumizi ya pesa ili kufikia malengo yako.

Huhitaji kujua kila kitu kuhusu pesa, cha msingi jifunze yale ya muhimu halafu uyazingatie walau kwa asilimia themanini (80%), utaona mabadiliko.

JILIPE MWENYEWE

Kuweka pesa inaweza kuwa moja ya tabia ngumu mno kuianzisha hasa unapokuwa na majukumu mengi ya kipesa.

Kinachotokea ni kwamba wengi hujikuta wakilipa kwanza kisha hufanya hesabu ya namna ya kuweka akiba ya zile zinazobaki kama kuna chochote kinachobaki kwa maana kuna wengine kiasi hicho wanachopata hakitoshelezi hata kulipia bili za umeme, maji na nyinginezo.

Jambo pekee unaloweza kufanya, hata kama ni kwa kulazimisha ni kujilipa mwenyewe. Kujilipa mwenyewe maana yake kutakufanya uweze kufanya hesabu na kujua asilimia ya kile unacholipa na kile unachotaka kuweka akiba.

Hii humfanya mtu kuwa na nidhamu ya namna ya kutumia kile alichojilipa na si zaidi ya hapo.

SONGA MBELE

Muda wote waza kufanya jambo jipya la kiuwekezaji katika maisha yako hasa unapojifunza kuwa na nidhamu zaidi.

Fikiria kama fursa ndiyo imejitokeza. Ifanyie kazi bila kujali matokeo ya haraka.

Endelea kufanya hivyo. Hakuna mtu aliyefanikiwa kirahisi bila kupitia changamoto mbalimbali katika kulifikia. Tumia msemo rahisi wa unapoamua kwenda peponi usisimame njiani. Pia wasiopumzika ndiyo ambao hupata wanachokitafuta.

WEKA MIPANGO

Weka mipango ya namna ya kutumia fedha zako kwa maandishi kabla ya kuziingiza kwenye matumizi. Jambo hili ni muhimu mno katika kujenga nidhamu ya matumizi ya pesa.

Kuweka mipango ni pamoja na kutengeneza bajeti ya mwezi mzima kwa maandishi.

Utaratibu wa kuwa na bajeti haina maana ndiyo ujinyime kama wafanyavyo wengi wakidhani ndiyo bajeti.

Bajeti ni namna sahihi ya matumizi ya pesa zako ili upate na akiba kwa ajili ya kutoka hapo ulipo kwenda mbele.

JILIWAZE KIDOGO

Ninaposema kuwa na nidhamu ya matumizi ya pesa simaanishi ndiyo ujinyime kiasi cha kushindwa kujipongeza walau kiduchu.

Naamini lazima ujiliwaze kidogo unapokuwa njiani kufikia lengo fulani.

Jipe liwazo hata kidogo. Inasaidia kuufanya ubongo wako uelewe kuwa kuna mambo mengi mema yanakuja hivyo utaufanya ufanye kazi kwa bidii zaidi.
 
Aisee hii ni shule tosha kwa maana wengi wetu, tunashindwa kukabiliana na changamoto za uwekaji fedha kwa ajili ya baadae.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hii hua ni ngumu mwanzoni especially kama umeshazoea maisha ya kukopa na kulipa ila ukiamua kujinasua inawezekana kabisa na kua na uhuru wa kifedha (financial independence).

nlianza pia na hiyo kanuni ya jilipe mwenyewe kwanza nikaona uzuri wake.,
 
Back
Top Bottom