MlakiKaskazi
Member
- Aug 11, 2022
- 10
- 8
Wakati tulionao jambo kubwa zaidi kwa watu wengi ni kujimudu kimaisha. Kila mtu anaamini ili aheshimike anahitaji kujiepusha kuwa tegemezi kwa watu wengine.
Wengi tunaamini kuwa na uchumi mzuri ndio msingi wa furaha maishani. Hili ni kweli japo sio msingi pekee. Swali la msingi la kujiuliza hapa ni "je kila njia ya kutafuta uchumi/kipato inaleta furaha tunayoitafuta?"
Ukiangalia vijana wengi hapa Tanzania utagundua kuwa wengi wao wanachanganya kati ya 'furaha' na 'raha'.
Ilipokuwa lengo ni kuwa na uchumi mzuri watu wengi hawajali kuhusu njia wanazotumia kupata huo uchumi.
Mathalani wapo vijana wanaonekana kuwa na maisha mazuri lakini wanajihusisha na tabia hatarishi kama uwizi, ulaghai, uasherati, ushoga n.k
"Uchumi unaotokana na mambo ambayo sio sahihi hauwezi kukuletea 'furaha' maishani badala yake utapata 'raha' kitu ambacho si cha kudumu."
Haya yalikuwa maneno ya kijana Kaba mzaliwa wa Kilimanjaro, mbele ya wafungwa wenzake baada ya kutafakari Mapito yake kwenye maisha na alipo sasa.

Upvote
3