Njia zinazotumiwa na mashabiki wa Simba kumkataa Matola na baadhi ya wachezaji ni za kijinai

Mwishokambi

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2020
Posts
390
Reaction score
1,425
Jana mashabiki wamepaza sauti zao baada ya sare na KMC, makelele mengi yalikuwa ni kumkataa Selemani Matola kwa madai anaihujumu timu, wengine walifikia hatua ya kutaka kumpiga hadi inasemekana akaokolewa na mabaunsa, wengine walimrushia makopo beki wa kulia Israel mwenda na Pape Sakho.

Tatizo la Simba mashabiki maandazi hawajalijua, shida ya Simba iko kwenye uongozi, maelewano hakuna, kuna wanaodai kudharauliwa, kuna wanaojiona wana hela, hivyo hawawezi kushauriwa na maskini, wale wanaodharauliwa ktk bodi ndio wanachomesha mahindi kwa kushirikiana na wajinga wajinga wengine nje ya timu.

Kuna watu wao bila Simba maisha hayaendi, sasa wamebanwa na huyo dada CEO, hakitoki kitu bila utaratibu, hao wamepanga kuiua tena Simba dhidi ya Yanga. Mnaopanga kwenda kuiangalia Simba dhidi ya Yanga hapo Oktoba nawashauri acheni hiyo, endeleeni na shughuli zenu, vinginevyo hamtaamini macho yenu.

Njia ya sasa ya kutukana na kurushia watu makopo haisaidii, hao viongozi mbona mnawaacha. Wao hawaumiii hata kidogo, ndio kwanza wanafurahia maisha, wewe ulietoka Mbagala povu linakutoka, njia pekee ya kuwaadabisha hao viongozi ni moja tu, waende wao na familia zao uwanjani, kwa hali tuliyofikia hapana. Njia ya kutukana ama kurusha makopo utatesa ndugu zako kwa kupata kesi ya jinai.
 
"MBUMBUMBU FC" by Aden Rage.

Akiondoka Mo MNA uwezo wa kuendesha timu?

Nyie MBUMBUMBU mnakumbuka mlitaka kuchoma nyumba ya Hassan Dalali mwenyekiti wenu?

MBUMBUMBU mnakumbuka mliwahi kumsingizia Kaseja kauza mechi?

Akiondoka Mo kuna muwekezaji yupo tayari kuwekeza timu ya MBUMBUMBU kama nyie?

Nimeamini maneno ya Aden Rage "MASHABIKI WENGI WA SIMU NI MBUMBUMBU".
 
"MBUMBUMBU FC" by Aden Rage.

Akiondoka Mo MNA uwezo wa kuendesha timu?

Nyie MBUMBUMBU mnakumbuka mlitaka kuchoma nyumba ya Hassan Dalali mwenyekiti wenu?

MBUMBUMBU mnakumbuka mliwahi kumsingizia Kaseja kauza mechi?

Akiondoka Mo kuna muwekezaji yupo tayari kuwekeza timu ya MBUMBUMBU kama nyie?

Nimeamini maneno ya Aden Rage "MASHABIKI WENGI WA SIMBANI MBUMBUMBU".
 
Tumekusikia na tumekuelewa wewe usie na akili.
 
Tumekusikia na tumekuelewa wewe usie na akili.
Wewe kidogo unajielewa. Ila kuna mashabiki wanaingia na matokeo uwanjani. Simba ikifungwa au kudroo lazima mchawi atafutwe! Waache umbumbumbu SOKA linachezwa uwanjani.

Sio dhambi Simba au Yanga kufungwa au kutoa droo!
TUSIINGIE NA MATOKEO UWANJANI!
 
Sure mpira dkk 90. Tuwe na uvumilivu
 
Umeandika utumbo tu bakhresa anaitaka simba kama leo hata hyo muwekezaji wenu GSM anataka kuwekeza simba ina maana umesahau alivyotaka kuwavalisha magodoro simba wakakataa baada ya kupata hasara kule utopoloni au unajitoa ufahamu
 
Wewe Pwilo nakukumbuka vizuri ulitaka kuchoma nyumba ya Hassan Dalali!

Rage naye aliwakosea nini?

Tuanze kukumbusha matukio ya nyuma.

Sisi Yanga tulifanya makosa haya haya, tulichukua kombe miaka 3 mfululizo tukavimbiwa tukamfukuza Paulsen! Unakumbuka kilichotupata? Miaka 4 bila kombe na njaa Kali!

Simba laana ya Gomez inawatafuna! Ni kweli hana vyeti ila hata kumbakiza tu awe mshauri ilishindakana?

Kuna kocha was Simba mwenye mafanikio zaidi ya Kibadeni na Gomez!?
 
Mafanikio gani unazungumzia.
 
Kusema kuna viongozi wanahujumu timu ni uongo. Ukinambia Wachezaji waliosajiliwa Wana viwango vya kawaida nitakuelewa, labda huo ndo uhujumu. Nassoro Kapama anaweza kucheza Mbeya City na usione tofauti, Nelson Okwa anaweza kucheza Geita Gold na akazidiwa na Nashon, Kibu Denis anaweza kucheza KMC bado star akawa George Makang'a, Israel Mwenda anaweza kwenda Kagera Sugar na bado beki wa kulia akabaki Dickson Mhilu.
 
Paulsen aliyefukuzwa yanga ndio alikuwa nani
 
Wale ni wahuni tu, sio mashabiki
 
Shida ya Simba kwa uwanjani siyo Katoka Wala uongozi.

Wachezaji hawajitoi
 
Mashabiki sampuli ile ndiyo Rage aliwaita mbumbumbu, ni kama yule mwasisi wa jina Utopolo.

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…