Njia zinazoweza kukuongezea uwezo wa kupata mtoto

WLF Tanzania

Member
Joined
Oct 9, 2014
Posts
38
Reaction score
22
Wadau,

Sote tunapenda watoto. Watoto ni lulu. Watoto ni zawadi. Watoto ni furaha, hasa akizaliwa katika wakati uliokusudiwa.

Kwa bahati mbaya kuna wakati tunachelewa kuwapata kwasababu hatufanyi mambo fulani sawasawa.


Dondoo kadhaa zaweza kukupa unachotarajia:

Kwa wanawake, kudumisha uzito unaofaa wakati unakusudia kupata mimba ni jambo zuri. Hutakiwi kuwa na uzito mkubwa sana au mdogo sana, wastani utakuweka katika nafasi nzuri ya kuwa na afya inayofaa.

Kwa wanaume, weka mbegu za kiume katika afya bora.
Dumisha uzito unaofaa kiafya, kula mlo bora/kamili, zuia magonjwa ya ngono, dhibiti mkazo (stress) na fanya mazoezi.


Tutaendelea kuwaletea dondoo hizi mara kwa mara. Nawe unaweza kushare zingine unazozifahamu nasi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…