Njombe: Ajiteka mwenyewe ili kumrudisha mume nyumbani

Muuza Kangala

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2021
Posts
1,242
Reaction score
4,813
Hii ni kali ya mwaka.

========

Joyce Ojala (32), Mkazi wa Matalawe Mjini Njombe, anashikiliwa na Polisi kwa kosa la kutoa taarifa za uongo kuwa ametekwa na Watu wasiojulikana ili kumlazimisha mumewe Mfaume Hussein Mzee (37), aliyekuwa Mkoani Ruvuma kwa zaidi ya miezi sita akifanya kazi za madini kurejea nyumbani.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Mahamoud Banga, amethibitisha kuwa Joyce alitoa taarifa kwa Mume wake akidai ametekwa na kwamba Mume wake anatakiwa kurudi haraka ili kushughulikia suala hilo, Mfaume alipokea taarifa hizo na kuamua kurejea mara moja baada ya kuambiwa kuwa mkewe yuko hatarini lakini baada ya ufuatiliaji wa Polisi ilibainika kuwa hakuna tukio la utekaji na kwamba Mwanamke huyo alijiteka mwenyewe kutokana na wivu wa mapenzi.

Kamanda Banga ameendelea kueleza kuwa Mume huyo alikuwa akiwasiliana na Mke wake mara kwa mara na kumjulisha kuwa anafanya shughuli za madini na hana uwezo wa kurudi mara moja hata hivyo Mwanamke huyo aliingia wivu na kuamua kutengeneza kisa hicho cha utekaji ili kumfanya Mume wake kurudi, Polisi walifuatilia tukio hilo baada ya taarifa kupokelewa na mwishowe walimkuta Joyce akiwa amejificha katika kibanda cha Fundi seremala Mjini Njombe.

Mfaume alipofika nyumbani baada ya kurudi kutoka Ruvuma alikuta Nyumba yao imefungwa na akaamua kusubiri hadi asubuhi kabla ya kutoa taarifa kwa Polisi ndipo Polisi walipoanza ufuatiliaji wa tukio hilo na kugundua kuwa Joyce alikuwa amepeleka taarifa za uongo kwa lengo la kumrudisha Mume wake.

Joyce Ojala sasa anashikiliwa na Jeshi la Polisi huku hatua za kisheria zikichukuliwa kutokana na kosa hilo la kutoa taarifa za uongo

Millard
 
Naona tunatembelea upepo wa Chalamila, ili vijana waliopotezwa wafichuliwe na kupewa kesi juu! Haya wacha tuendelee kunywa mtori nyama tutazikuta chini!

====

Wamuelewe tu huyo bila kusahau, tunazingoja ripoti kumhusu mzee Kibao, Soka na wale wengine.
 
images (3).jpeg
 
Taarifa hiyo ya uongo aliitoa kwa mtu wake sio polisi kwahiyo ni mambo yao wenyewe.
 
Huyo mwanamama katokea tanga ?
 
Back
Top Bottom