Njombe: Akutwa akiwa uchi kanisani

Njombe: Akutwa akiwa uchi kanisani

Muuza Kangala

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2021
Posts
1,242
Reaction score
4,813
Mwanaume anayekadiriwa kuwa na umri wa zaidi ya miaka 40 anayetajwa kuwa ni Mkazi wa Mkoa wa Morogoro amekutwa akiwa mtupu kwenye Madhabahu ndani ya Kanisa la Anglikana lililopo Mtaa wa Matema Halmashauri ya Mji wa Makambako Mkoani Njombe huku sababu zikiwa bado hazijajulikana.

Katibu wa Kanisa hilo, Elias Ngailo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa Mwanaume huyo amekutwa akiwa mtupu amelala na kulazimika kumsaidia kumvalisha nguo na kumpeleka Kituo cha Polisi Wilaya ya Kipolisi Makambako huku wakiwa hawajui kama anajihusisha na imani za kishirikina au ana matatizo ya akili.

"Tumemuhoji baadhi ya maswali amesema yeye ni wa Morogoro sasa umekujaje huku hawezi kujieleza ila tulifadhaika tukaona walau tumsaidie kwa kumtafutia nguo asitiri mwili wake baada ya hapo tukampeleka kwenye Vyombi vya Usalama ili wajue namna ya kumsaidia"

Mwinjilisti wa Kanisa hilo John Kisogo amesema awali baada ya kumkuta Mtu huyo katika madhabahu walilazimika pia kumfanyia maombi “Huyu Mtu alisema alijikuta tu yupo Madhabahuni tukamuuliza ulikuwa peke yako akasema nilikuwa na mwenzangu"
 
Jamani, mimi naendelea kukumbusha tu kuwa ndugu yetu mzabzab anatokea morogoro. Ni vyema tukajua tu kama yuko salama na kama yuko bado morogoro maana humu ndani tunajuana kwa ID za siri
 
Vipi Milango ya Kanisa waneikuta imefungwa kama walivyoiacha jana?Kama ni hivyo itakuwa Engine failure.
 
Jamani, mimi naendelea kukumbusha tu kuwa ndugu yetu mzabzab anatokea morogoro..
Ni vyema tukajua tu kama yuko salama na kama yuko bado morogoro maana humu ndani tunajuana kwa ID za siri
mzabzab
Leo hata online sijamwona. Labda 2kamwekee dhamana polisi arudi aandike thread kwa yaliyomkuta kwa ushirikiano na DeepPond mwandishi nguli
 
Itakuwa alikuwa anatenda jambo kimasihara ...... just joking, should be mental health conditions
 
Mwanaume anayekadiriwa kuwa na umri wa zaidi ya miaka 40 anayetajwa kuwa ni Mkazi wa Mkoa wa Morogoro amekutwa akiwa mtupu kwenye Madhabahu ndani ya Kanisa la Anglikana lililopo Mtaa wa Matema Halmashauri ya Mji wa Makambako Mkoani Njombe huku sababu zikiwa bado hazijajulikana.

Katibu wa Kanisa hilo, Elias Ngailo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa Mwanaume huyo amekutwa akiwa mtupu amelala na kulazimika kumsaidia kumvalisha nguo na kumpeleka Kituo cha Polisi Wilaya ya Kipolisi Makambako huku wakiwa hawajui kama anajihusisha na imani za kishirikina au ana matatizo ya akili.

"Tumemuhoji baadhi ya maswali amesema yeye ni wa Morogoro sasa umekujaje huku hawezi kujieleza ila tulifadhaika tukaona walau tumsaidie kwa kumtafutia nguo asitiri mwili wake baada ya hapo tukampeleka kwenye Vyombi vya Usalama ili wajue namna ya kumsaidia"

Mwinjilisti wa Kanisa hilo John Kisogo amesema awali baada ya kumkuta Mtu huyo katika madhabahu walilazimika pia kumfanyia maombi “Huyu Mtu alisema alijikuta tu yupo Madhabahuni tukamuuliza ulikuwa peke yako akasema nilikuwa na mwenzangu"
Niliwahi kuambiwa kwamba Morogoro ni lango kubwa sana la wachawi nchi nzima. Kwamba kigoma na Sumbawanga wanasubiri
 
Masharti ya waganga yatawaua wana Njombe aisee...masharti kibao unawakuta wapo kwenye Escudo maisha bhana...
 
Back
Top Bottom