Njombe: Aliyebaka mtoto wake kisa utajiri ahukumiwa jela miaka 30

Njombe: Aliyebaka mtoto wake kisa utajiri ahukumiwa jela miaka 30

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Mahakama ya Wilaya ya Wanging'ombe mkoani Njombe imemuhukumu miaka 30 jela Mwanaume aitwae Joseph Mwajombe (33) Mkazi wa kijiji cha Lulanzi, kwa kosa la kumbaka binti yake mwenye umri wa miaka 15.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo James Mhoni amesema Mtuhumiwa alitenda kosa hilo Agosti 7, 2022 baada ya kutoka kumpakia Binti huyo kwenye pikipiki yake akitoka shuleni hadi eneo la jirani na nyumbani kwao alikomfanyia ukatili huo.

Hakimu amesema alipofika kwenye eneo hilo ambako kuna bwawa alimwambia Binti yake kuwa amewasiliana na Freemason ambao walibandika tangazo lao kwenye nguzo ya umeme ambao wamemuagiza afanye naye mapenzi ili apate utajiri hivyo akamuomba binti yake huyo amkubalie.

Hakimu amesema Mtoto huyo alikataa kufanya hivyo ndipo Baba huyo akampiga na kumuingilia kimwili kwa nguvu na baadaye kumrudisha binti huyo nyumbani kisha akaondoka kuelekea kusikojulikana na ilipofika usiku Binti alishindwa kuvumilia na kuanza kulia huku akimsimulia Mama yake kilichotokea ambapo Mama huyo akatoa taarifa upesi kwa Mtendaji wa kijiji aliyeongozana na Mgambo kumsaka na kumkamata Mtuhumiwa na kumpeleka Polisi ambako alikiri kutenda kosa hilo.
 
Kuna watu wana akili ndogo mpaka basi! Yaani umeliona tangazo la matapeli kwenye nguzo za umeme, ndiyo uhalalishe huo upuuzi kwa mtoto wako wa kumzaa!!

Bora hata angehukumiwa tu kifungo cha maidha jela. Miaka 30 bado ni michache sana. Huyu binti ataathirika sana kisaikolojia.

Maana sisi wazazi wa kiume ndiyo walinzi na marafiki namba 1 wa watoto wetu wa kike! Sasa tukiwafanyia ukatili wa aina hii, watamwamini nani tena katika maisha yao!!
 
Inasikitisha sana... Sasa huko anaenda kuliwa yeye kwa miaka 30...
 
Afu kuna Kenge 1 linaamini kabisa kuwa Watu wasioamini ktk dini yake hawatakula bata mbinguni, kama si utaahira ni nini haswa?

Matukio kama haya hayana uhalali na inapaswa adhabu izidishwe ili Watu wazidi kujifunza kupitia wafungwa, inamanisha Watu hatuko sawa kiakili, kitabia, kiiutendaji na hata kimaamuzi.

Mwisho wa siku imani ni adui mwingine hatari sana anayeibukia kwa kasi kupoteza maisha yetu Binadamu kwa kukosa maarifa na kuishia kupata vifungo vya maisha na hata kupoteza malengo kimaendeleo.
 
Kuna watu wana akili ndogo mpaka basi! Yaani umeliona tangazo la matapeli kwenye nguzo za umeme, ndiyo uhalalishe huo upuuzi kwa mtoto wako wa kumzaa!!

Bora hata angehukumiwa tu kifungo cha maidha jela. Miaka 30 bado ni michache sana. Huyu binti ataathirika sana kisaikolojia.

Maana sisi wazazi wa kiume ndiyo walinzi na marafiki namba 1 wa watoto wetu wa kike! Sasa tukiwafanyia ukatili wa aina hii, watamwamini nani tena katika maisha yao!!
Halafu haya matangazo yanahamasisha mtu kufanya uhalifu lakini mamlaka zipo tu kimya mpaka tatizo litokee ndipo wanachukua hatua, sijui wanasita nini kupiga marufuku moja kwa moja haya mambo.
 
Kuna watu wana akili ndogo mpaka basi! Yaani umeliona tangazo la matapeli kwenye nguzo za umeme, ndiyo uhalalishe huo upuuzi kwa mtoto wako wa kumzaa!!

Bora hata angehukumiwa tu kifungo cha maidha jela. Miaka 30 bado ni michache sana. Huyu binti ataathirika sana kisaikolojia.

Maana sisi wazazi wa kiume ndiyo walinzi na marafiki namba 1 wa watoto wetu wa kike! Sasa tukiwafanyia ukatili wa aina hii, watamwamini nani tena katika maisha yao!!
Hapo ukute na pesa alishawatumia
 
Back
Top Bottom