Pre GE2025 Njombe DC: Bilioni 1.16 zakabidhiwa kwa vikundi 92 mikopo ya mapato ya ndani

Pre GE2025 Njombe DC: Bilioni 1.16 zakabidhiwa kwa vikundi 92 mikopo ya mapato ya ndani

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Zaidi ya shilingi bilioni 1.1 zimetolewa kwa vikundi 92 vya wanawake,Vijana na walemavu katika Halmashauri ya wilaya ya Njombe ili zikawasaidie kuendesha miradi mbalimbali Fedha ambazo hutolewa kupitia makusanyo ya mapato ya ndani.

Fedha hizo ni zile za Asilimia kumi za maelekezo ya serikali ambazo awali zilisitishwa kutokana na changamoto mbalimbali zilizoibuka ikiwemo ukiukwaji wa utoa na baadhi ya viongozi wakiwemo Madiwani kunuifaka nazo ili Hali sio walengwa.

Pre GE2025 Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Taarifa ya utoaji mikopo hiyo iliyosomwa na Ofisa Maendeleo Halmashauri ya wilaya ya Njombe Sarah Chambachamba imesema safari hii Wametoa kwa vikundi vilivyokidhi vigezo.

Mbunge wa Jimbo la Lupembe Edwin Swalle na Justin Nusulupila Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Njombe wamewataka waliopata Fedha hizo kwenda kuzitumia kwa kadri ya malengo na sio kuzifuja.

Akikabidhi Hundi hiyo Mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka Amesema anataka kuona matokeo chanya katika Fedha hizo kwa vikundi vyote huku Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe Deo Sanga akiwaonya na tabia ya kutumia fedha hizo kwenye pombe na starehe nyingine.

Baadhi ya wananchi wilayani Njombe waliopata mkopo huo wameahidi kwenda kuendesha biashara na ujasiriamali waliopanga kuutekeleza kwa umakini mkubwa.
1740137707729.png
 
. Barabara kutoka makambako hadi njombe ni chakavu sana..🙂 🙂.

. Viongozi wa nchi hii unaweza hisi hawakai hapa Tanzania
 
Vikundi 92.
92×10 =920
11000000000 ÷920 =1.1ml
Kwahiyo wastani wamemkopesha Kila mtu sh. Million 1.
Million moja huyo DC akienda nayo shipping hairudi chenji.
Hii mikopo ya kukuza umaskini kabisa
 
Back
Top Bottom