Bila ushabiki wowote, kwa wale wanaoujua mkoa wa Iringa na jinsi wilaya zake zilivyojipanga wanaweza kutambua hilo. Uundaji wa mkoa wa njombe unalenga zaidi katika suala la kiutawala zaidi kuliko idadi ya watu. Kimsingi mtazamo wangu hupo katika vipengele vifuatavyo:
1. kufanya njombe kuwa mkoa itarahisisha ufanisi katika taratibu za kiutawala kwa wilaya kama za ludewa na makete. Hizi wilaya ziko mbali sana na Iringa na inahitaji zaidi ya masaa si chini ya 6 kufika katika wilaya hizi.
2. serikali inapoteza pesa nyingi kwenye mafuta, marupurupu ya watendaji katika wilaya hizi. Chukua mfano wa wilaya ya ludewa, kupeleka taarifa inamlazimu mtumishi wa serikali kutumia karibu siku nne kuifikisha Iringa na kurudi ludewa. Je kuna safari ngapi za namna hii zinazofanywa na watumishi wa idara mbalimbali za serikali?
Kwa upande wa maendeleo bado nina shaka kwani hakuna uwiano wa moja kwa moja. Nafikiri ukiangalia kwa upana zaidi 'saving' kubwa inaweza kupatika katika kubadilisha mfumo mzima wa uongozi katika wilaya. Hebu fikiri:
1. DED ndio kama accounting officer wa wilaya na idara zote ukitoa polisi wako chini ya DED
2. Mkuu wa wilaya ni cheo cha kisiasa zaidi kuliko utendaji na zaidi haina ufanisi wowote katika kuleta chachu za maendeleo katika wilaya.
Mtazamo wangu: sioni tatizo la kuongeza mkoa ila nina tatizo kubwa la 'organigram' ya wilaya na mkoa kwa ujumla. Kwa kipindi hiki kuna council 133 bila shaka na wilaya ni 133, sasa tufanye udhanifu ufuatao:
Kila mkuu wa wilaya anapata Shs 100m - bajeti ya mwaka 133 x 100m = 13,300,000,000
Kila wilaya ina land/cruiser angalau moja 50 m x 133 6,650,000,000
Kwa makadirio ya chini wilaya zote zinaweza kuwa na bajeti 19,950,000,000
Je Shs 20bn haziwezi kuleta mabadiliko katika idara nyingine na tukatoa 'inefficiency' inayotokana na ofisi hii?