Njombe: Lori na Coaster vyagongana

Njombe: Lori na Coaster vyagongana

Faana

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2011
Posts
38,657
Reaction score
44,759
Ajali mbaya imetokea jioni ya leo 24.04.2022 majira ya saa 11.30+ ikihusisha coaster na lori la makaa ya mawe, watu kadhaa wanatajwa kupoteza maisha, taarifa zaidi zitatolewa na mamlaka husika.

====

Zaidi ya Watu watatu wanahofiwa kufariki baada ya gari aina ya coster iliyobeba vijana wa kwaya ya vijana wakatoliki wa Njombe (UVIKANJO) ambao walikwenda kutembelea watoto yatima katika kituo cha Ibumila kugongana uso kwa uso na gari ya makaa ya mawe iliyoacha njia na kuigonga coster hiyo katika eneo la Igima.

Kuna majeruhi ambao idadi yao bado haijajulikana.

====

Taarifa kutoka vyanzo vya kuaminika zinasema hadi leo tarehe 25.04.2022 idadi ya waliofariki kutokana ajali ya jana vimefikia nane (8). Mwenyezi Mungu awarehemu wapumzike kwa amani
Screenshot_20220424-191003_Gallery.jpg


Screenshot_20220424-190939_Gallery.jpg


20220424_175129.jpg


Screenshot_20220424-205441_Earth.jpg
cover_279031957_1652903978399353_3630845854209569594_n.jpg
post_279296621_3241375982762335_3709950384511129277_n.jpg
 
Sijaelewa lori iimegong costa au costa imegonga lori
Ilivyoonekana lori lilihama lane likaifuata coaster na kuichota mpaka imegeukia ilikotoka
 
Specialised Hauliers, hawa jamaa nikiwa safari ndefu napishana nao kwa adabu sana. Na kama kumuovertake simpiti mpaka nihakikishe nimepigia honi za kutosha na kumwashia full light
Kuna mtu amesema huwa wanakijiubabe fulani njiani
 
Mungu awarehemu marehemu wote.
Hizi ajali za Lori na gari za abiria zimezidi kwa kweli, natagemea uchunguzi ungefanywa hata na waandishi wetu wa habari waseme nini chanzo. Binasfi nahisi baadhi ya madereva wameanza kutumia alcohol hasa nyakati za mchana.
 
Poleni sana kwa msiba mzito wa wanakwaya. Mungu awape faraja wafiwa wote.
 
Mungu awarehemu marehemu wote.
Hizi ajali za Lori na gari za abiria zimezidi kwa kweli, natagemea ungefanywa hata na waandishi wetu wa habari waseme nini chanzo. Binasfi nahisi baadhi ya madereva wameanza kutumia alcohol hasa nyakati za mchana.
Hakuna kingine Mkuuu.
Maaskari wa usalama barabarani wameanza kula kwa Urefu wa Kamba zao, hakuna cha ukaguzi wala onyo ni mwendo wa kukusanya pesa tu mifukoni mwao.
 
Back
Top Bottom