Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Wakuu,
Hii kali! Kuna uchawa afu kuna hii!
====
Maombi ya viongozi wa dini mkoani Njombe yaliyofanywa kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa Hapo Novemba 27 Mwaka huu yametajwa kusaidia zoezi hilo kufanyika kwa salama bila kuripotiwa kwa matukio ya mauaji wala vurugu.
Wakizungumza ofisi kwa mkuu wa wilaya ya Njombe aliyewaita kwa lengo la kuwashukuru kwa maombi yao baadhi ya viongozi hao akiwemo mchungaji wa kanisa la kiinjili kilutheri KKKT Njombe, Nelson Godiwe amesema nchi imefanya kampeni za kizalendo ambazo hazikuwa za matusi wala kashfa.
Naye Mchungaji wa Kanisa la Sabato Njombe, Yonasy Chatila amesema mikoa mingine watu walitamani kujifungia ndani lakini Njombe ni tofauti kwa sababu hawajasikia malalamiko ya vyama vya siasa kutokana na kila mtu kufanya kampeni zake kwa amani.
Kupata taarifa na matukio yote kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa kimkoa angalia hapa:
www.jamiiforums.com
Hii kali! Kuna uchawa afu kuna hii!
====
Maombi ya viongozi wa dini mkoani Njombe yaliyofanywa kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa Hapo Novemba 27 Mwaka huu yametajwa kusaidia zoezi hilo kufanyika kwa salama bila kuripotiwa kwa matukio ya mauaji wala vurugu.
Wakizungumza ofisi kwa mkuu wa wilaya ya Njombe aliyewaita kwa lengo la kuwashukuru kwa maombi yao baadhi ya viongozi hao akiwemo mchungaji wa kanisa la kiinjili kilutheri KKKT Njombe, Nelson Godiwe amesema nchi imefanya kampeni za kizalendo ambazo hazikuwa za matusi wala kashfa.
Kupata taarifa na matukio yote kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa kimkoa angalia hapa:
LGE2024 - Dar es Salaam: Matukio yaliyojiri kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 27, 2024
WanaJF, Mada hii itakuwa na 'Updates' za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 kama yanavyotujia kutoka kwenu kutoka mkoa wa Dar es Salaam. Ukiwa na taarifa yoyote ambayo ni ya eneo hili tafadhali usisite kushiriki na wengine. Ramani ya Jiji la Dar es Salaam HISTORIA YA JIJI LA DAR ES SALAAM Jiji...
Mkuu wa Wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa amewashukuru viongozi wa dini kwa kuombea uchaguzi na kufanyika kwa amani na kutoa rai kwa wananchi kuelekeza macho yao kwenye kilimo na uzalishaji uchumi.
Katibu Tawala wilaya ya Njombe, Agatha Mhaiki amesema kazi ilikuwa nzito lakini imekwenda salama kwa sababu kila jambo linalindwa kwa maombi na hivyo kutumia fursa hiyo kuwataka viongozi wa dini kuendelea kuwahimiza wazazi kufundisha watoto wao maadili.