Lady Whistledown
JF-Expert Member
- Aug 2, 2021
- 1,147
- 2,008
My take: Ni ajabu na ni kweli mtoto mmoja kuwa na Wababa zaidi ya Mmoja. Wenyewe wanasema Wanawake ambao hufanya hivi lengo lao ni kupata Maokoto kutoka kwa Wababa wengi ilhali anajua mhusika ni mmoja
Na hii ni kwasababu mtu ukishapewa kadi unajua Mtoto ni wako
Njia moja ya kuepusha haya huko mbeleni ni kuwa na Mfumo wa Utoaji Kadi wa Kiditali. Yaani Mjamzito akishasajiliwa na kupewa kadi hawezi kusajiliwa tena kwenye Kituo Kingine cha Afya kwasababu database ina rekodi zake tayari
Kujiandikisha manually ndiko kunakotengeneza udanganyifu
Mama Gwajima tunalileta hili mikononi mwako, tunaomba uone namna ya kutatutua Changamoto hii
............
Ili kuimarisha makuzi na malezi ya watoto na kutengeneza kizazi salama,wanawake wametakiwa kuacha kuwatumia watoto kama biashara kwa kutengeneza kadi zaidi ya moja na kuwakabidhi wanaume ili waweze kusaidia kwenye malezi ya mtoto.
Wito huo umetolewa na Mratibu wa Afya ya Uzazi na Huduma za Mama na Mtoto mkoa wa Njombe Felisia Hyera kwenye kikao cha utekelezaji wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT-MMMAM) inayotekelezwa na shirika lisilo la kiserikali la UWODO kwa kushirikiana na serikali.
Felisia ametoa wito wanawake kuwa waaminifu ili kutengeneza familia bora kwa kuwa wengi wanaofanya hivyo hutokana na kushindwa kukubaliana na uhalisia wa mimba walizobeba hali inayopelekea mtoto kuanza kuyumbishwa tangu akiwa tumboni kwa mama.
"Siku zote huwa tunasisitiza mjamzito afike kliniki akiwa na ujauzito wa chini ya miezi mitatu na hausemi lazima uende kituo x, sasa mama huyu akifika ambapo mimi nipo nitamfungulia kadi lakini hatujui mama huyu wakati wa makuzi yake ilikuwaje anaamua kwenda kituo kingine, tena kule nako watampa kadi nyingine na kama bado hajatimiza akina baba aliokuwa nao atajitahidi kwenda kwenye vituo kulingana na idadi ya wababa alionao" Amesema Felisia.
Awali Godfrey Kiowi ambaye ni Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Njombe alieleza namna wanavyokutana na kesi ya mtoto mmoja kuwa na baba wanne huku akiomba serikali kuona namna ya kubadili mfumo wa upatikanaji wa kadi za watoto.
"Hizi kesi tunakutana nazo huko mtaani mtoto mmoja ana baba wanne lakini pia ukija kufuatilia kila baba amepewa kadi yake na kila baba anatoa huduma kwa muda wake halafu kesho linaibuka kila baba anasema mtoto ni wa kwake" Amesema Kiowi.
Kwa upande wake Hamis Kassapa ambaye ni Mkurugenzi wa Shirika la UWODO amesema katika kikao walichokaa na wataalamu mbalimbali wameweza kuwajengea uwezo juu ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto ili kwenda kuendelea kukabiliana na changamoto mbalimbali za watoto kwenye makuzi
Aidha amehimiza wazazi na walezi kutenga muda wa kukaa na watoto na kuwajenga kwenye ulinzi pamoja na afya ili waweze kuwa na afya wakati wa makuzi yao.
Chanzo: Jambo Tv