Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Polisi mkoani Njombe wamekamatwa watu wawili wa CHADEMA, Emmanuel Raston Ngelime (44) na Obadiah Tedius Chogwa (47) siku ya Jumanne, Oktoba 15, 2024 baada ya video kusambaa, ikionyesha wakiwa wamemzuia na kumhoji kijana aliyejitambulisha kama kijana wa CCM, Antony Mtagawa baada ya kuadaiwa kusambaza majina hewa kwenye vituo vya kujiandikisha. Polisi wameeleza kuwa Ngelime na Chogwa walitumia nguvu kumshambulia Mtagawa.
“Ninafanya kazi kama coordinator wa vijana wa CCM wa Mgendela. Nilikuwa nikihamasisha watu kuja kujiandikisha,” alisema Antony Mtagawa wakati akihojiwa na wanaume wawili waliomshuku kuwa anashughulikia orodha ya wapiga kura katika eneo lao.
“Antony Mtagawa ni mwanachama wa CCM na alikuwa akifanya kazi kama wakala wa chama katika kituo hicho cha kujiandikisha kwa sababu mwenziwe hakuwepo. Hata hivyo, kwa kuwa hakuwa anafahamika na wakala wa CHADEMA, alishukiwa kuwa anashughulikia orodha ya wapiga kura,” alifafanua Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Njombe, Mahamoud Banga.
“Wanaume hao wawili walimshambulia Mtagawa, na kumletea madhara, lakini uchunguzi wetu umeonesha kuwa hakuna tatizo la kujiandikisha wapiga kura wa uwongo,” Banga aliongeza.
Polisi walithibitisha kuwa wanaume hao wawili watafikishwa mahakamani, na walitoa wito kwa umma kutofanya maamuzi wenyewe bali kufuata taratibu za kisheria.
Pia, Soma:
+ Wakala wa CHADEMA, Jacob Emily adaiwa kuumizwa alipokua akizuia majina yaliyoletwa na watu wa CCM kuingizwa kwenye daftari la uandikishaji wapiga
+ Waziri Mchengerwa: Hakuna Uthibitisho wa madai ya Uandikishaji Wanafunzi Kupiga Kura