LGE2024 Njombe: Rose Mayemba asema Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ulikuwa ni operesheni ya kuwashughulikia wapinzani

LGE2024 Njombe: Rose Mayemba asema Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ulikuwa ni operesheni ya kuwashughulikia wapinzani

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,


Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani Njombe Rose Mayemba amedai kuwa uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika jana, Novemba 27.2024 nchini kote haukuwa uchaguzi kama ilivyodhaniwa badala yake ilikuwa ni oparesheni kuwashughulikia wapinzani nchini

Rose ameeleza hayo alipofanya mahojiano na Jambo TV mapema leo, Alhamisi Novemba 28. 2024 ambapo amedai kuwa katika mkoa wa Njombe idadi kubwa ya mawakala waliondoshwa kwenye vituo vya kupigia kura wakati zoezi la upigaji kura lingali linaendelea, na wale waliokuwa wabishi kutoka walikuwa wakitolewa kwa nguvu na askari bila kupewa maelezo yoyote

Kupata taarifa na matukio ya kimkoa kuhusu Uchaguzi Serikali za Mitaa ingia hapa: LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Amesema baadhi ya mawakala walichelewa kuingia vituoni (kwenye vyumba vya kupigia kura) kutokana na kucheleweshwa kupata barua za utambulisho kutoka kwa wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya jimbo ambao ni Wakurugenzi wa Halmashauri, huku baadhi ya maeneo yakitaarifiwa kuingizwa kura feki alizodai kuwa zimetumika kuwapa ushindi bandia Chama cha Mapinduzi (CCM)

Ametolea mfano vurugu zilizoibuka jimbo la Njombe mjini, kata ya Mji mwema, mtaa wa Mji mwema kwenye kituo cha Msete ambapo yeye binafsi alipokea taarifa kuwa kuna njama zinaandaliwa kubadilisha matokeo ya kituo hicho kutokana na kile kilichoelezwa kuwa eneo hilo ni 'ngome' ya CHADEMA na ilikuwa vigumu kura feki kuingizwa kituoni hapo

Amedai walipoona njia ya kuingizwa kura feki imeshindikana ndipo wakaamua kubeba masanduku ya kura na kupeleka kwenye eneo wanalolijuwa wenyewe, wakati mpango huo mbaya unaandaliwa ndipo Rose Mayemba alipopata taarifa na kukimbilia eneo hilo, na kukuta kweli masanduku yanahamishwa kabla kura hazijahesabiwa

Anasema alipoona hivyo alihoji sababu inayopelekea kuondoa masanduku kituoni kabla kura hazijahesabiwa ndipo akajibiwa kuwa hayo ni maelekezo kutoka juu kuwa kura zote zikahesabiwe kwenye kituo cha majumuisho jambo ambalo hakukubaliananalo na katika majibizano hayo mwisho waliondosha masanduku hayo kwa nguvu

Ameendelea kudai kuwa katika kituo hicho idadi ya wapiga kura waliojitokeza ni ndogo hivyo masanduku ya kura hayakuwa na karatasi nyingi za kura lakini kwenye gari iliyopakiwa masanduku kulikuwa na masanduku mengine yaliyojaa kura ingawa hawakujuwa masanduku hayo yametokea wapi, baadaye kwenye kituo cha majumuisho mgombea wa CCM alitangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi huo.
 
Huyo Bwana hapo juu sijui ni nani hapo Nzega. Anaongea kabisa kama Kada wa CCM.

Yaani anasubutu kabisa kusema waliviita vyama rafiki.

Hivyo Vyama RAFIKI ni vyama gani?
 
Back
Top Bottom