Njombe: Watu 7 wakamatwa kwa kutishia kuwaua Mwenyekiti wa Mtaa, Katibu Kata wa CCM, Mtendaji Kata na Mtendaji wa Kijiji

Mtoa Taarifa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2024
Posts
213
Reaction score
671
TAARIFA KWA UMMA.
Jeshi la Polisi mkoa wa Njombe linapenda kutoa taarifa kwa umma kuwa linawashikilia watu saba kwa kosa la kutishia kuua kwa Maandishi huko katika kijiji cha Ngelenge Kata ya Luhuhu wilaya ya Ludewa Mkoa wa Njombe watu hawa saba walitenda kosa hilo tarehe 3.12.2024 kwa kubandika Mabango yenye maneno ya kutishia kuua katika ofisi mbalimbali za serikali katika kijiji cha Ngelenge wilaya ya Ludewa.

Watu hao waliotishiwa ni pamoja na Joseph Mapunda miaka 60, Mwenyekiti mchaguliwa katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2024 na wengine ni Yusuph Stephano miaka 50, Mtendaji Kata ya Luhuhu, Colina Michael miaka 25, Mtendaji wa Kijiji cha Ngelenge na Fernatus Michael Mgaya 52, Katibu Kata wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Luhuhu. Uchunguzi wa tukio hili utakakapokamilika watafikishwa mahakamani.

Jeshi la Polisi mkoa wa Njombe linatoa wito kwa Wananchi wenye tabia za kutoa vitisho kwa viongozi waliochaguliwa kuacha mara moja kutenda uhalifu huo na atakaebainika hatua kali dhidi yake zitachukuliwa kwa mujibu wa sheria.

Imetolewa na:
Mahamoud Banga - ACP
Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Njombe.
 
TAARIFA KWA UMMA.​

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…