Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Wakuu,
Waziri Michezo Dkt. Damas Ndumbaro ametoa wito kwa Watanzania kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 kwani uchaguzi huo ni muhimu kwa kuwa unawezesha kupatikana viongozi wa ngazi za chini kabisa katika muundo wa uongozi hapa nchini
Kupata taarifa na matukio yote kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa ingia hapa: LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Dkt. Ndumbaro ametoa rai hiyo mkoani Njombe wakati akizungumza na wananchi wa Lupembe alipokuwa akifunga michuano ya Swalle Cup iliyokuwa ikifanyika katika kijiji cha Image ambapo pia ametumia jukwaa hilo kupigia chapuo chama chake (CCM) kwa kuwaomba wananchi hao kuwapa ridhaa wagombea wa ngazi mbalimbali wanaopeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi huo
"CCM ndio chama cha maendeleo na mashindano haya (Swalle Cup) ni utekelezaji wa ilani ya CCM ibara ya 243, juzi timu yetu ya Taifa (Taifa star imefuzu AFCON, ushindi ule ni utekelezaji wa ilani ambayo inasisitiza serikali iimarishe michezo, sasa hicho ndio chama chenye ilani, waulizeni wengine ilani zao ziko wapi?" -Dkt. Ndumbaro
Edwirn Swalle ni Mbunge wa jimbo la Lupembe (CCM) na mdhamini wa michuano ya Swalle Cup amesema kutokana na jitihada kubwa za kuleta maendeleo zilizofanywa na serikali ndani ya jimbo hilo anaamini wananchi hawana shida na wanafahamu nini cha kufanya Novemba 27.2024 na kwamba wapo tayari kuiunga mkono CCM ili kupata maendeleo wanayotarajia zaido
Waziri Dkt. Ndumbaro amefunga michuano ya Swalle cup na kushuhudia mtanange mkali wa fainali uliozikutanisha timu za Ikuna FC pamoja na Matembwe FC ambapo dakika tisini zimekamilika kwa timu ya Ikuna FC kuibamiza mabao mawili kwa sifuri na kutawazwa kuwa bingwa michuano ya Swalle Cup msimu wa 2024.