Njombe yanusurika kuingia gizani kisa moto kuwaka kwenye kituo cha kusambaza umeme

Njombe yanusurika kuingia gizani kisa moto kuwaka kwenye kituo cha kusambaza umeme

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Sintofahamu imetokea mkoani Njombe na hii ni baada ya moto ambao bado haujafahamika chanzo chake kuwaka na kuteketeza eneo la kituo cha kusambaza umeme mkoani humo.

Mara tu baada ya kudhibiti moto huo, Kaimu meneja wa TANESCO mkoa wa Njombe Mhandisi Lazaro Bartazai alidokeza kuwa hakuna athari kubwa zilizojitokeza kutokana na moto huo na kuongeza kuwa wanaendelea kufanya tathmini ya athari zilizopatikana.

"Kilichotokea mpaka tukakata umeme ni moto umeunguza maeneo ya store jirani na kituo chetu cha kusambazia umeme lakini haujaleta athari kubwa"

Kituo Cha Kusambaza Umeme Chanusurika Kuungua.jpg


Injinia Lazaro Joel Mwakanyasa Mrakibu msaidizi wa jeshi la zimamoto na uokoaji ambaye ni kaimu kamanda wa jeshi la Zimamoto mkoa wa Njombe amesema wakati tukio hilo likitokea tarehe 4 Septemba 2024, majira ya saa tisa na nusu alasiri walipokea taarifa kutoka kwa raia mwema juu ya moto kuwaka eneo la kituo na kufika mapema kuudhibiti moto huo.

"Tulikuta moto umeshaanza kuwaka lakini kwa kushirikiana naa wanachi pamoja na wafanyakazi wa TANESCO tulishirikiana kuuzima lakini chanzo cha moto hatujatambua chanzo"

Aidha ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Njombe kuwa makini wanapochoma moto ili kutokuleta madhara ikiwamo kuchoma miundombinu iliyojengwa na serikali kwa gharama

Soma pia: Njombe: Afariki ndani ya gari akiota moto kwenye jiko la mkaa

Source: Jambo Online

 
tukio hilo likitokea tarehe 4 Septemba 2024, majira ya saa tisa na nusu alasiri walipokea taarifa kutoka kwa raia mwema juu ya moto kuwaka eneo la kituo na kufika mapema kuudhibiti moto huo.
Usishangae kusikia waliozima ni wananchi ila hao maofisa wanapambwa tu, maana huwa hawana jipya zaidi ya kufika kwenye matukio bila vifaa
 
Back
Top Bottom