Makininick
New Member
- Sep 2, 2022
- 4
- 3
Waswahili husema "Mwanzo Mgumu" kutoka na msemo huu tunaweza kujenga hoja kwamba, kila kinachoonekana kuna mwanzo ulio mgumu.
Leo Jamii forum inawafuasi zaidi ya milioni moja lakini ilianza na mtu mmoja.
Mwaka 2013 nilimaliza kidato cha nne Shule ya Sekondari Orkolili iliyopo Wilaya ya Siha. Baada ya matokeo nilipata ujumbe uliosema, "njoo Kimahama Interview saa mbili asubuhi".
Namba ilikua ngeni na ilikua haipatikani baada ya ujumbe huo. Ilikua ni Interview ya kujiunga na kidato cha tano kwa udhamini wa gharama zote( full funded) kwenye shule ya Cornerstone leadership academy iliyopo Arusha, Ngaramtoni.
Siku iliyofuata nilianza safari alfajiri sana ambapo nilifanya mawasiliano na marafiki zangu waliopo Arusha kwasababu sikupafahamu Kimahama ni wapi. Saa moja asubuhi nikifika Kimahama nikitokea Sanya Juu, niliamka mapema na nilipanda gari la kwanza.
Ilipofika saa mbili, niliona wanafunzi waliongezeka huku wakiwa wamevaa vizuri sana, kama watu wanaoenda kwenye Interview. Walivaa mashati, suruali za vitambaa na viatu vizuri. Mimi nilikuwa nimevaa jeans na t-shirt na raba, nilijiona siko sawa. Niliamua kununua shati nyeupe walao nifanane na wenzangu.
Kulikua na watu wengi sana, nilipata rafiki hapo aliyetokea Tanga na alinieleza vitu vilivyohitajika, ambayo vilikuwa ni Transcript ya matokeo ya kidato cha nne, leaving Certificate, barua ya utambulisho kutoka kwa mwenyekiti wa kijiji na barua ya kiongozi wa dini. Hivi vyote sikua navyo, nilikua mikono mitupu.
Nilienda Stationery nika print matokeo ya shule na kwenye matokeo yangu nikachora mstari na kalamu.
Nilimfuata mmoja ya viongozi wa Interview na kuamueleza kwamba nimetoka Sanya Juu na sikuwa na viambatanisho vinavyohitajika ila nitaweza kuvileta wakati utakao fuata, alinijibu, "umetokea Moshi?, utaweza kweli?, Kesho saa mbili asubuhi gari litakua hapa kupeleka watu shule ilipo, Interview zitaendelea huko kwasababu watu wamekua wengi".
Makadirio yangu kulikua na watu zaidi ya mia tatu. Na waliohitajika ni watu 50 tu 25 wasichana na 25 wavulana, nchi nzima.
Niliondoka Kimahama haraka na kuanza kufanya mawasiliano namna naweza kupata nyaraka hizo kwa haraka. Sikufanikiwa ila Shangazi yangu alinitia moyo nisiogope.
Nilirudi Sanya Juu na usiku huo nilitumia ujumbe na rafiki yangu aliyepo Arusha kwamba na yeye atakuepo hivyo nisiache kufika tuwe na kampani.
Asubuhi niliwahi mapema sana. Saa kumi na mbili asubuhi nilikua Bomang'ombe kuvuka daraja la kuingia kwa Wasomali. Hapo gari halikuweza kuvuka mvua kubwa iliyonyesha usiku ilifanya daraja lifunikwe na maji, hakuna dereva aliyethubutu kupitisha gari lake. Hapo nilijua habari yangu kwisha. Mpaka Saa Mbili kasoro maji yalianza kupungua gari likapita. Nilipiga picha tukio hili hii, japo simu haikua na kamera nzuri sana.
link
Nilifika Arusha saa mbili na madakika na gari ya mwisho ilikua inaondoka nikaikimbikia.
Ndani ya gari kulikua na watu waliopendeza wenye kishkwambi( smart phones) mimi nilikua na Tecno isiyo na memory card, muito wake ulikua ala ya "happy birth day to you" niliwaona wenye furaha kama watu walioshinda Interview.
Tulifanya Interview japo mimi nilikua wa mwisho kwani sikua na viambatanisho viliyohitajika. Niliomba wanipe muda nifanye Interview niwaletee wakati utakao fuata, walinikubalia.
Nilirudi nyumbani nikiwa na mawazo sana, kwani niliulizwa siku ya ibada iliyopita tulifundishwa nini na kiongozi wa dini, hata kiongozi mwenyewe sikuweza kumkumbuka, na alijaza hivyo.
Siku moja nikiwa matengenezo bustani nilipokuwa simu kwamba nimefaulu Interview ya kwanza niende kwenye Interview ya pili. Nilifurahi sana.
Haikua rahisi kwani tuliishi pale wiki moja na walikua wanatazama tunavyoishi.
Hatukujua vigezo vyao, hivyo kila kitu kilikua sehemu ya Interview. Nakumbuka siku moja nilikua nadeki bafu nikavunja (mopper) dekio lenye mpini wa mti. Mbele ya kiongozi. Nilipatahofu sana yaani mpaka ninavunja mopper!.
Tulimaliza Interview tukapanda kwenye gari ambapo unakabithiwa barua yako ukiwa ndani ya gari. Gari liliondoka na nilichungulia barua yangu nikakuta nimefaulu Interview. Nilimshukuru Mungu kimyakimya.
Kuna masomo mengi nilijifunza kwenye Interview hii. Ikiwa ni pamoja na
- usiogope kuifuata nafasi(opportunity) iliyopo mbele yako.
- Kuwa mkweli binafsi na kwa wanaolizunguka, ishi maisha yako( usiigize maisha)
- Mafanikio yoyote huwa na kujitoa (sacrifice) kujizatiti ( commitment) na uvumilivu.
- usiogope hata kama mambo hayaendi vile ilitarajia.
- kuna furaha kubwa unapofikia mafanikio fulani.
- Kua na marafiki wanaotamani ifanikiwe.
Itoshe kusema usikate tamaa, na usiogope kuanza. " Njoo Kimahama Interview saa mbili asubuhi".
Ahsante

Upvote
5