Njoo utufundishe kutengeneza juice zisizozoeleka

Njoo utufundishe kutengeneza juice zisizozoeleka

mitale na midimu

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2015
Posts
10,420
Reaction score
17,735
Mwenyezi Mungu ametupatia aina lukuki za matunda lakini ukipita mitaani au ukitembelea kwenye nyumba zetu, juice maarufu ni ya Pasheni,Parachichi na embe.

katika kusaka maarifa huku na kule nimejifunza aina ya juice ambayo pia ni muhimu saana.
fruit-Vegetable juice.
yaani juice ya mchanganyiko wa matunda na mbogamboga ni vigumu kutafuna spinach mbichi pamoja na faida zake lukuki kiafya lakini ni rahisi kuitafuna kwa njia ya juice.


karibu kwa kutupa michanganyiko ya juice unayodhani inawezekana na inafaida sana kiafya lkn haijazoeleka.
 
Lozera +ubuyu+iriki
Carrot iliyochemshwa na kuachwa ipoe +iriki +maziwa ya unga
Parachichi+maziwa
viazi vyekundu(beetrrot)+apple
asante mkuudada hiyo ya mwisho inaonekana ni matata sana.
 
Lozera +ubuyu+iriki
Carrot iliyochemshwa na kuachwa ipoe +iriki +maziwa ya unga
Parachichi+maziwa
viazi vyekundu(beetrrot)+apple

Najifunza
[emoji120] [emoji120] [emoji120]
 
Chukua machungwa 5 yaliyoiva vizuri (yasiwe machachu), Karoti za wastan 2, peach 1 kubwa, Tikiti maji vipande vikubwa 2

Menya machungwa, yakate vipande 2 kila moja. Yakamue kupata juisi yake(Ondoa mbegu), kisha mimina hicho kimiminika kwenye blender.
Chukua karoti zako, kwangua kuondoa layer ya juu, kisha zikatekate vipande vidogovidogo, kisha vichanganye kwenye blender iliyo na juisi ya machungwa.
Chukua peach, limenye kisha likate vipande vidogovidogo, kisha nalo lichanganye kwenye blender.
Chukua tikiti maji, ondoa ganda la juu, kisha likate vipande na kulichanganya kwenye hyo michanganyiko mingine( sio lazima utoe mbegu).

Saga mchanganyiko wako kwenye blender mpaka ulainike. (Usiweke maji) kwani machungwa, na tikiti hutoa maji, hivyo kufanya juisi yako kuwa na uzito mzuri tu.

Unaweza kuichuja au lah, weka juice yako kwenye glass tayari kwa kunywa.

N:B
Best served cool
Don't add sugar
KINYWAJI KIZURI KWA RIKA ZOTE

ENJOY
 
Mchicha Na Maziwa,juice Ya Ubuyu(juice Natumia Kumpikia Uji Mwanangu Hakuna Sukari,naongeza Karanga Nlizosaga
Maziwa Mtindi,parachichi,tende Ukiongeza Ndizi Si Mbaya
 
Back
Top Bottom