Chukua machungwa 5 yaliyoiva vizuri (yasiwe machachu), Karoti za wastan 2, peach 1 kubwa, Tikiti maji vipande vikubwa 2
Menya machungwa, yakate vipande 2 kila moja. Yakamue kupata juisi yake(Ondoa mbegu), kisha mimina hicho kimiminika kwenye blender.
Chukua karoti zako, kwangua kuondoa layer ya juu, kisha zikatekate vipande vidogovidogo, kisha vichanganye kwenye blender iliyo na juisi ya machungwa.
Chukua peach, limenye kisha likate vipande vidogovidogo, kisha nalo lichanganye kwenye blender.
Chukua tikiti maji, ondoa ganda la juu, kisha likate vipande na kulichanganya kwenye hyo michanganyiko mingine( sio lazima utoe mbegu).
Saga mchanganyiko wako kwenye blender mpaka ulainike. (Usiweke maji) kwani machungwa, na tikiti hutoa maji, hivyo kufanya juisi yako kuwa na uzito mzuri tu.
Unaweza kuichuja au lah, weka juice yako kwenye glass tayari kwa kunywa.
N:B
Best served cool
Don't add sugar
KINYWAJI KIZURI KWA RIKA ZOTE
ENJOY