Magical power
JF-Expert Member
- Sep 27, 2022
- 2,158
- 5,626
NJOO VIZURI
Kuna bwana mmoja aliniijia akanikuta mahali napata moja ya baridi,wenyewe husema kuchamba koo....
Sasa yule bwana akanishambulia kwa maneno unakunywa pombe ni dhambi,
Nikatulia kumsikiliza.
Akasema tena walevi wote mwisho wao motoni...
Mimi: Nikamuuliza nani mlevi ?
Yeye: Wewe hapo
Mimi: unamjua vizuri mlevi ?
Yeye: mtu yoyote anywaye ni mlevi .
Mimi: mlevi ni mtu yeyote aliye nje ya utambuzi ama ufahamu na pale anapoikosea sheria ama amri anakua amefanya dhambi...
Kuna mtu ni mlevi wa zinaa.,Ngono imefunga fahamu zake mpka anakosa upendo anaanza kuwakwaza wengine kwa kutamani na kulala na wake wa jirani zake.
Ulevi ni kukosa kiasi...
Hata wema ukipitiliza ni kama ulevi utajiangamiza mwenyewe.
Sasa hemu niambie nimevunja sheria na Amri ipi?
Yeye: Imeandikwa ole wake ampaye jirani yake kileo.
Mimi: Nikamuuliza mbona hilo andiko hulisomi lote au limeishia hapo,?
Yeye : Hapana halijaishia hapo acha nikusomee HABAKUKI 2:15 inasema "" Ole wake ampaye jirani yake kileo,wewe utiaye sumu yako,na kumlevya pia ili kuutazama uchi wake..!
Mimi: Nikamwambia sasa umeona mwandishi alimaanisha hivi,ole wa yule ambaye anampa kilevi mwanamke,na kutia sumu ili atoke nje ya ufahamu wake,ili akautazame uchi wake ama kuzini naye,Hilo ndio kosa,sasa nakuuliza wewe tena mimi umenikuta nimetulia nakunywa,sijagombana na mtu, sijamtukana mtu dhambi yangu ni ipi?
Yeye : Duh.
Mimi: Nikamwambia ndugu yangu Ufalme wa mbinguni haupatikani katika kula,ama kunywa
WARUMI 14:17 Maana ufalme wa Mungu si kula wala kunywa,Bali ni haki na amani na furaha katika Roho mtakatifu.😎
Nikamalizia na kumwambia ndugu yangu mimi sifungwi na chakula ama kinywaji chochote, ama kushika siku zozote kama sabato...
Ninakushukuru pia kwa kuja naamini umeondoka na kitu.
Yeye : Ahsante
Content created by : magical power