Njooni mnaoamini Yanga SC atadondosha point na Simba atakuwa bingwa

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,292
Reaction score
15,250
Nataka mjitokeze mbele ya na mpige magoti huku mkiwa mnabubujikwa na machozi na kuomba radhi wanasoka wote.

Mjitokeze na mseme kwanini mlikubari dhana ya kipuuzi ya namna hiyo ipate nafasi ndani ya Mioyo yenu.

Ni nani miongoni mwenu mwenye kuamini 31yrs old Kagere atamaliza Ligi akiwa na mabao 7?

Ni nani miongoni mwenu anaye amini kuwa Mayele atamaliza Ligi akiwa chini ya mabao 20? Na ajitokeze hivi sasa nimzabe vibao.

Ni nani huyo anayedhani Ubora wa Mabingwa wa kihistoria wa msimu huu unafanana na Makolo FC walio sheheni wazee?

Ni uwanja upi na kwa kisingizio kipi kitapelekea Yanga SC apoteze alama hata kwa kutoa sare.?

Je ni kipi kimewasahaulisha kuwa Dar es Salaam Young Africans SC ni mabingwa wa kihistoria wa LIGI KUU TANZANIA BARA.

Tuliwapatua uhuru wa kuwa mabingwa kwa miaka 3 ili tupate fursa ya kujenga kikosi cha kutawala miaka 10 mbele.

Huu ni msimu wa 2021/22 - ni wa Yanga SC

Na pia msimu wa 2022/23 - ni wa Yanga SC

Tukutane msimu wa keshokutwa yaani 2023/24.
 
Subiri ubebe kombe acha maneno, mpira uko kama upepo ukivuma yanga yako utaitafuta kwa tochi.
 
GSM anawala sana ndogo kiasi kwamba hamuoni hamsikii..masikini akipata!
 
Yani ligi bado mzunguko wa kwanza tayari yanga wanaanza kubweka.
 
Pointi 7 nyingi mno
Yanga ana sare mbili hajapoteza mchezo.
Hizo ni sare moja na kupoteza michezo miwili tu mzee.
Tukiwapiga mpunga akina mayele wanaachia sare mbili na kufungwa mbili mchezo unaishia hapo.
 
Yanga ana sare mbili hajapoteza mchezo.
Hizo ni sare moja na kupoteza michezo miwili tu mzee.
Tukiwapiga mpunga akina mayele wanaachia sare mbili na kufungwa mbili mchezo unaishia hapo.
Waache wachukue. Au unataka Bundesliga ihamie huku?
 
Yanga ana sare mbili hajapoteza mchezo.
Hizo ni sare moja na kupoteza michezo miwili tu mzee.
Tukiwapiga mpunga akina mayele wanaachia sare mbili na kufungwa mbili mchezo unaishia hapo.
Kwa hiyo nyie kubeba ubingwa mpaka mtoe rushwa? Uhalali wa kusema mnahujumiwa unatoka wapi?

Inawezekana vipi ili uwe na matumaini usubili mwenzako afungwe?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…