Njooni mnishauri ndugu, mtaji milioni 5 nifanye biashara ya bucha au niuze viatu?

Njooni mnishauri ndugu, mtaji milioni 5 nifanye biashara ya bucha au niuze viatu?

Chris wood

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2020
Posts
1,667
Reaction score
5,043
Habarini ndugu zangu nimekuja kwenu nahitaji ushauri nina milioni 5 nahitaji kufanya biashara moja kati ya hizo.

Je, ipi inaunafuu wa kuniingizia kipato kwa urahisi zaidi, changamoto za uendeshaji, risk ya kupoteza mtaji.

Natanguliza shukran, napatikana Dar es Salaam.
 
Huo wote ni uchuuzi, kutoboa kwenye uchuuzi kazi sana, wee hizo biashara umeona zimemtoa nani? Una reference?
Nunua mazao uza, fanya utafiti eneo ulipo kipindi cha mavuno mazao gani hupatikana kirahisi kisha nunua kwa wakulima na uuzie mabosi wenye mitaji mikubwa pesa ita tripple in one year
Kununua mazao na kuuza sio uchuuzi? Uchuuzi ni nini?
 
Kati ya hzo mbili naona bora viatu vya mtumba mana havina mwingiliano sana na serikali. Bucha utahtajka kuwa na kibali toka bodi ya nyama TMB, uwe na ule msemeno wa kukatia nyama wa kisasa, na vikorokoro vingne.
 
Huo wote ni uchuuzi, kutoboa kwenye uchuuzi kazi sana, wee hizo biashara umeona zimemtoa nani? Una reference?

Tembea uone zanzibar butcher ni maskin?
Unawajua wale Jamaa wa Mwenge pale?

Kila biashara ina utajiri ndani yake inategemea anaeifanya anafanyaje.
 
Kati ya hzo mbili naona bora viatu vya mtumba mana havina mwingiliano sana na serikali. Bucha utahtajka kuwa na kibali toka bodi ya nyama TMB, uwe na ule msemeno wa kukatia nyama wa kisasa, na vikorokoro vingne.
Mtaji utakata within a year
 
Kununua mazao na kuuza sio uchuuzi? Uchuuzi ni nini?
Mi pia nimeshangaa kwamba anaongea vitu asivyo vielewa.

Atafute maana halisi ya neno uchuuzi, tena biashara ya bucha yaani kuchinja na kuuza siyo uchuuzi.

Kununua na kuuza ndiyo uchuuzi.
 
Mimi naona bora ufanye biashara ya viatu ila kwa 5Milioni unapata faida nzuri kabisa, nakushauri viwe vya dukani.
 
Biashara ya bucha inalipa sana kama utapata location nzuri.

Hapo utadeal na bars, kwa mahitaji ya kuchoma nyama watakuja kuchukua kilo za kutosha

Mama ntilie, hakikisha unacheza na mama ntilie wote hapo mtaani.

Hao utakuwa unawuzia nyama kwa bei nafuu kidogo badala ya 8000 kwa kilo utawauzia 7000 kwa kilo.

Biashara ikichangamka vizuri ukaweza kuuza ng'ombe mmoja kwa siku, tegemea kuingiza 200k faida kwa siku.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nunua mazao uza, fanya utafiti eneo ulipo kipindi cha mavuno mazao gani hupatikana kirahisi kisha nunua kwa wakulima na uuzie mabosi wenye mitaji mikubwa pesa ita tripple in one year
Kwa hiyo hiyo sio biashara ya uchuuzi? Na nani alikudanganya biashara za uchuuzi hazina faida?
 
Back
Top Bottom