dereva mpya
New Member
- Jul 22, 2022
- 1
- 2
Katika nchi ya Tanzania tangu tulivyoingia kwenye mabadiliko ya mfumo wa kidunia tulibeba dhana kwamba elimu ni mojawapo wa msingi wa ukombozi wa fikra kati yetu lakini pia elimu ndio nyenzo kuu katika kuendesha nyaja mbalimbali mfano za kiuchumi, kisiasa na hata kimichezo.
Hapo awali mfumo ulipoingia nchini watu waliobahatika kupata fursa za elimu walifanikiwa kwa kiasi kikubwa kwanza walielimika ipasavyo lakini pia walipata nafasi za ajira kutokana na elimu zao na lakuvutia zaidi maarifa mengi waliyoyapata waliweza kuyatumia na leo matunda ya elimu zao tunayaona mfano baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Mhandisi Patrick Mfugale ni baadhi ya wengi ambao matunda ya elimu zao kama taifa tunajivunia.
Kutokana na namna bora ya uendeshaji wa taifa katika nchi yetu suala la elimu kwa kila mtu lilipokelewa kwa namna njema hivyo ilimlazimu kila mtu lazima apitie misingi ya kupata elimu kuanzia elimu ya awali mpaka chuo, lakini pia zikaanzishwa elimu za watu wazima, kukariri mitihani kama mtu alifeli awali, ada za elimu ya msingi mpaka sekondari zimetolewa kwa shule za sekondari na mikopo ya elimu kwa wanachuo hata wale waliosoma shule binafsi lengo kubwa na zuri ni kuhakikisha inapatikana jamii ya watu walioelimika, watakaopata fursa za ajira na ambao wataweza kujiajiri na kuajiri wengine. Leo nchini Tanzania kuna idadi kubwa ya wasomi na bado kuna idadi kubwa ya watu wanaoendelea kusoma kwa dhana ile ya elimu ni mkombozi. Njozi njema inaotwa na wengi kama elimu inaweza kuwa msaada binafsi kwa watu na kua msaada mkubwa kwa taifa.
Hizi njozi ni njema lakini usingizi hauishi kwahiyo zinabaki kuwa ndoto zisizo kamilika sababu bado kuna wimbi kubwa la wasomi wapo tu mitaani wakiwa wamekosa ajira na hawawezi kujiajiri, lakini pia walioko mashuleni awajui kwa undani vitu wanavyosoma na hata baadhi waliomaliza elimu hawana uelewa hata chembe kwa waliyosoma.
Hoja mbalimbali zimejengeka kama njia zitakazo weza kuumaliza usingizi huu ili njozi njema zifanyiwe kazi. Wengi waliongea kuhusu lugha ya kufundishia na wengine waliongea kuhusu kubadilika mara kwa mara kwa mfumo wa elimu. Lakini mimi kama dereva gari langu linapita katika vituo vinne ambavyo kiuhalisa vinaweza kufanya kazi na matunda ya elimu yakaonekana.
Kituo cha kwanza ni wazazi na walezi, hapa ndio kwenye msingi mkubwa ambapo watoto au vijana hutokea kuelekea mashuleni na vyuoni. Wazazi na walezi wengi wamewapa Imani watoto wao kwamba elimu ya darasani ndio njia kuu ya kujikwamua na maisha na watoto wamefuata njia hiyo mpaka hizi changamoto za ajira zinapojitokeza bila kua na njia mbadala. Wazazi wana nafasi kubwa za kuwasaidia watoto ili kuweza kumaliza changamoto kwa njia zifuatazo;-
1. Wazazi kujipa nafasi ya kuzungumza na watoto kuhusiana na masuala ya elimu na changamoto wanazopitia huku wakiangazia njia nzuri za kimaisha, wazazi wengi hawana muda wa kuzungumza na watoto zaidi ya kuwapa mahitaji stahiki na kuwaacha wapambane kwa njia zao.
2. Kurithisha ujuzi kwa watoto. Wazazi wengi wamekua na ujuzi wa vitu mbalimbali mfano kuna wazazi ni mafundi, wapishi na wakulima wa kawaida hawa wana nafasi kubwa ya kurithisha au kufundisha ujuzi kwa watoto wao ili iwe msaada hata kama masuala ya kielimu yakiwa na changamoto kama sasa mtoto anakua na uwezo wa kujiendeleza katika masuala mengine pasi na kutegemea elimu tu. Dhana ya kuamini elimu ni njia sahihi ya kimaisha imefanya wazazi kuwanyima ujuzi watoto wao ambao ungekua msaada mkubwa.
Mfano leo baba anaweza kuwa fundi seremala mzuri au mama ni mpishi wa mgahawa mzuri lakini mtoto anaweza asiwe na ujuzi hata kidogo wa kazi hizo. Kunaweza kuwa na hoja kwamba mazingira ya kazi za wazazi yanaweza kuwa sio rafiki kwa watoto kujifunza kama ziada lakini kuna namna ambayo mzazi anaweza tumia ili mtoto apate ujuzi kama ana nia thabiti na pia kama mzazi kaweza kuendesha maisha kwa kazi hiyo basi inatosha kumjenga mtoto naye apate ujuzi huo umfae maishani.
Kituo cha pili ni mashuleni na vyuoni ambapo walimu wanakaa na vijana hawa, kwanza walimu wanatakiwa kujua ni watoto wa namna gani wanawafundisha ili waweze kuwasaidia kirahisi sababu katika wanafunzi 30 kati yao wanaweza kuwa wanafunzi 10 wana uwezo mdogo sana wa uelewa au wengine hawana mpango wa elimu kabisa lakini umri wao huwezi kuwaachia wakae mtaani hivyo walimu wanapaswa kutengeneza mazingira bora ambayo wale wenye uwezo, wasio na uwezo na wasiopenda shule kujiona wapo katika njia moja kwa namna zifuatazo
1. Kuepuka kuwagawa wanafunzi au kuwatolea lugha mbaya ila kuwajengea umoja ambao utafanya hata wale wenye uwezo mdogo kunyanyuka kitaaluma kwa msaada wa wenzao hata ikiwa kidogo
2. Kuhakikisha wanafunzi wanajua mtaala wao kila wanapovuka hatua, lakini kujua vitu wanavyosomea vinahusiana na nini ili wawe na muongozo sahihi.
3. Walimu wanapaswa kujua njia sahihi za kuwasaidia wanafunzi wenye uwezo mdogo mfano mwanafunzi anaweza kua na uwezo mdogo ila ana vipaji vikubwa hivyo walimu wanaweza kumjenga kupitia vipaji vyake na akapenda shule na vikawa ni msaada kwake.
Kituo cha tatu n taasisi za binafsi na kiserikali zinatakiwa kutoa fursa za vijana kujifunza kwa vitendo na zikitoa nafasi hizo basi zisisite kuwapa majukumu ya kufanya, taasisi zitoe nafasi za kujitolea kwa vijana ili wapate ujuzi sababu ili kuingia kwenye soko la ajira ujuzi unahitajika, taasisi za fedha hususani benki zinazotoa mikopo kwa wanafunzi au zenye akaunti kwa ajili ya wanafunzi zitoe elimu kuhusu umuhimu wa kutunza fedha na fursa za kibiahara ili ziwasaidie kujiajiri.
Wanafunzi wa kidato cha 4&6 hufanya kitu kinaitwa ‘project’ ambazo huishia kwenye makaratasi, wizara inatakiwa itengeneze mfumo ambao hizo ‘project’ ziweze kupatikana na taasisi mbalimbali kwa maendeleo ya taifa huku wahusika wakipewa nafasi ya kuzieleza vile vile tafiti zinazofanywa na wanachuo zipewe nafasi ya kufanyiwa kazi. Taasisi ziwe na mifumo mizuri ya kupokea madokezo, mapendekezo na maandiko pia na kujibu kwa wakati sababu taasisi nyingi zimeziba fursa kwa vijana kwa kutoshughulikia madokezo, mapendekezo na maandiko mbalimbali.
Mwisho kabisa ni serikali kwa kushiirikiana na wadau mbalimbli wa elimu kufungua mijadala itakayoonyesha dira na mfumo wa pamoja wa kuweka elimu katika mstari ambao utasaidia watu kuelimika, kuajiriwa, kujiajiri lakini maarifa ya elimu kuleta matunda katika taifa. Taifa likiwa na sera nzuri katika elimu basi usingizi utaisha na kufanyia kazi njozi njema.

Upvote
2