nlipotafuta sikupata...sasa ndio wanapatikana...

nlipotafuta sikupata...sasa ndio wanapatikana...

Maalim Jumar

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2010
Posts
1,259
Reaction score
118
Habari wanaJF!
Dunia hii imejaa mambo kila aina...kila mtu anautashi wake..wengine wanatekeleza kwa usiri mkubwa...wengine wanayaweka bayana.
Yoote hii ndio dunia.
Sasa nlikutana na jamaa yangu wa karibu akawa amenieleza mambo yaliomfika..
Akanambia uwezo wa kuishi na mke anao...tatizo yule mke anaehitaji awe nae ndio hajafanikiwa kwa kipindi kirefu kiasi ambacho ndugu zake na jamaa zake hawakuridhika maisha aliyo kua nayo!
Sasa aliamua aoe yeyote aliejitokeza muda huo...hapo ndipo mambo yakaanza kumchanganya...alijitokeza dada mwenye sifa zote na huyo dada alikua tayari aolewe nae. Tatizo kwa jamaa alisaini ndoa moja..pia dada huyo nae hakukubali awe mke wa pili.
Jamaa amechanganyikiwa hajui afanyeje?
Tunamsaidia vipi wana JF?
 
Mshika mawili moja ....

Ngoja ninywe kahawa ntarurdi ..
 
Afadhali huyo mwanamke alijua mapema hataki ukewenza akamsainisha jamaa!
 
Sijaelewa tafadhali yan amsainishe ndoa mke wa pili halafu ndio amtafute wa kwanza? au mimi sijakuelewa ndugu?
 
Amesaini mwenyewe, tatizo sasa liko wapi!
 
zamani ndio haya mambo ya kusaini ndoa moja yalikuwa na tija,sasa hayapo tena so mkuu kipendacho rohoo hula nyama mbichi,amuwa moja wewe ndio mwamuzi kuacha na kuoa ama kubaki na huyo uliyesaini ndoa
 
Kama unahisi uliye nae huna hata mapenzi nae boraumuache kuliko kumsanif mwenzako
 
ni tamaa tu za kidunia, wanawake wazuri wanazaliwa kila siku, ataoa yupi aache yupi?
 
kama hukumpenda abuy bora umuache tuu atapata anae mpenda na yeye lakini sio kuja kumtesa baadae.... wewe ndio muamuzi kama walivyotangulia kusema wanajf hapo juu umuoe huyo au uoe uliempenda....sisi twaweza kukushauri lakini abadaan huwezi kuusemea moyo wa mwenzio.... soo wake up and make what can sound good and nice in ur mind...
 
kama amesaini ndoa si maaana yake ameshaoa?? sasa anachotaka kingine zaidi ni kipi?
huyo mwingine ni tamaa tu wala hakuna jipya huko
 
Aridhike na aliyenae.
Wazuri kila siku wanazaliwa.
Ataacha wangap?
 
A point of no return, imekula kwake, aendelee tu na huyo mke... Na iwe fundisho kwa watu wengine kusaini/kuingia mikataba yenye masharti magumu/wasiyo kubaliana nayo bila kufikiria yajayo
 
Habari wanaJF!
Dunia hii imejaa mambo kila aina...kila mtu anautashi wake..wengine wanatekeleza kwa usiri mkubwa...wengine wanayaweka bayana.
Yoote hii ndio dunia.
Sasa nlikutana na jamaa yangu wa karibu akawa amenieleza mambo yaliomfika..
Akanambia uwezo wa kuishi na mke anao...tatizo yule mke anaehitaji awe nae ndio hajafanikiwa kwa kipindi kirefu kiasi ambacho ndugu zake na jamaa zake hawakuridhika maisha aliyo kua nayo!
Sasa aliamua aoe yeyote aliejitokeza muda huo...hapo ndipo mambo yakaanza kumchanganya...alijitokeza dada mwenye sifa zote na huyo dada alikua tayari aolewe nae. Tatizo kwa jamaa alisaini ndoa moja..pia dada huyo nae hakukubali awe mke wa pili.
Jamaa amechanganyikiwa hajui afanyeje?
Tunamsaidia vipi wana JF?

Kuanza upya sio ujinga.
 
jamaa nilivyo muelewa ni kama ifuatavyo:
1- alihitaji mke wa kuishi nae.
2-alikua navyo vgezo vyake kwa huyo ataeishi nae.
3-kwa kua imemchukua muda mrefu i.e miaka mingi bila kumpata aliemhitaji ndio akaamua kumchukua yeyote aliependa kuolewa.
4-baada ya maisha ya ndoa ndipo akajitokeza ryt choice wake...
5-huyo dada mwenye vgezo ndio amempa masharti kua hahitaji uke wenza.
6-jamaa kwa ile ndoa yake ya kwanza alisainishwa hakuna kuoa zzaidi ya ndoa moja...
Hapo ndipo mambo yamemkalia pabaya...
Hana raha.
Nlimsikia atii anataka amtoroke first wife wake...ili asijulikane alipo...baadae ndipo amuoe huyo mwenye vgezo vya kuzingatiwa.
Hii dunia ina matukio ....mh!.
 
Ndo mkome kuoa na kuolewa for the sake of kuitwa wanandoa!Swala la kubebana na mtu ambae baadae utatamani asingekuwepo ili uwe na unaemtaka ni la kujitakia!Kama hujaridhika na mtu usioe au kuolewa nae!
 
Back
Top Bottom