Mimi ni mteja wa benki zaidi ya tano hapa nchini, nikijumuisha akaunti kadhaa za biashara na akiba kwa matumizi binafsi. Kilichonifurahisha wiki mbili zilizopita, nikiwa njiani kwenda Tunduma (mpakani mwa Zambia na Tz) ilinibidi nisimame kwa muda mjini Mafinga na kuingia katika tawi la NMB kufanya muamala wa kuhamisha fedha kulipia mzigo moja kwa moja kwenda akaunti ya supplier. Huduma niliyoipata iliniridhisha sana, wameboresha kwa kutenga dirisha la kupokelea fomu za funds transfer, hivyo mteja hakai foleni muda mrefu. Big up NMB Mafinga Branch!