NMB: Makato mapya kwa wateja wa NMB yaja yakiwa yameongezeka mara mbili zaidi ya sasa?


What about kutazama salio? Nimesikia ati ni sh 2500+!!
 
Msisahau Magufuli anasubiria gawio kule
 
Maendeleo Hayana Chama
Yaani Bora Kumsaidia Nyoka Kuliko Nmb Bank
Hawa SasaHivi Ni Majizi Hayana Nafasi Awamu Hii Ya Tano
 
Picha
BENKI ya NMB imeondoa tozo kadhaa kuanzia Februari Mosi mwaka huu ikiwemo sh 1900/- iliyokuwa ikitozwa kila mwezi kwa ajili ya gharama za ufundi za kibenki.

Mkuu wa Kitengo cha Malipo ya Wateja NMB, Michael Mungure amewaeleza waandishi wa habari kuwa, tozo nyingine iliyoondolewa ni ile ya kufufua akaunti mfu.

Awali kufufua akaunti iliyokaa muda mrefu bila kutumika ilikua inatozwa shilingi 2200 na kama haijatumika mwaka mzima mteja angelazimika kuifufua kwa shilingi 26,400.

Mungure ameitaja tozo nyingine iliyondolewa ni ile ya uhamisho wa fedha kutoka benki moja kwenda nyingine, kwa mfano kuhamisha mishahara, kufanya huduma za kibenki kwa njia ya simu, na kuuliza salio.

Awali huduma hizo zilikuwa zikichajiwa shilingi 800 kwa kila moja. Meneja Mwandamizi Huduma ya Amana NMb, Steven Adil amesema, wameondoa tuzo hizo baada ya utafiti uliofanywa na taasisi za kimataifa uliobainisha kuwa, Watanzania wengi hawatumii huduma za kibenki kutokana na utitiri wa makato.

Amesema pia lengo la kuondoa tozo hizo ni kupata wateja wengi zaidi wa kufungua akaunti katika benki hiyo.

Kwa mujibu wa Adil, akaunti zilizondolewa makato ni zile za binafsi, akaunti za vikundi na fanikiwa, na kwamba, akaunti za kampuni makato bado yanaendelea kama kawaida. Mkuu wa Kitengo cha Wateja, Abella Tarimo amesema, NMB wanaendelea kuboresha huduma kwa njia ya kidijitali kwa gharama nafuu.

Amesema kwa sasa mteja anaweza kufungua akaunti kupitia simu ya mkononi.

“Pia bidhaa yetu ya Klik App, itakuwezesha kufanya miamala mbalimbali kutuma pesa, kulipa deni, kuomba mkopo, kulipia na huduma nyingine,”amesema Tarimo.

Amesema NMB imejipanga kumfikia kila Mtanzania na kumuingiza kwenye uchumi rasmi.

“Kwa kuwa na teknolojia ya kidijitali tuna fursa nzuri ya kuendeleza huduma zetu za mtandaoni katika matawi yetu lengo letu ni kuwapa wateja wetu mamlaka ya kutuma maombi kwa haraka na kwa usalama kwa njia ya kidijitali na kuwapa ushauri kupitia kwa mameneja uhusiano wetu,” amesema.

Tarimo amesema uwezo wa kufungua akaunti mtandaoni ni hatua ya kwanza na wataendelea kuongeza bidhaa nyingine kwa kuzingatia usalama wa fedha za wateja.

Alisema ili mteja aweze kufungua akaunti kupitia simu ya mkononi atatakiwa kubonyeza *150*66# na kufuata maelekezo na ndani ya dakika tatu atapatiwa namba ya akaunti ya simu yake.

“Unaweza kumfungulia mfanyakazi wako akaunti akawa anapata mshahara wake kupitia simu yake ya mkononi, hapa tumemrahisishia muda wa kwenda benki kufungua akaunti pamoja na kujaza fomu nyingi ili apate akaunti,” amesema Tarimo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna benki ya kijinga kama hii kubadilisha sahihi tu inachukua miaka 2 nilipotezaga kadi ya benki nilipata shida sana kila siku kutoa hela ndani mara wanauliza sahihi haifanani onana na meneja...nashukuru niliikausha akaunti sasa hivi wamebaki kutuma ujumbe mara usitaje namba yako ya siri etc etx
 
Yah,tupunguzieni hasira kidogo maana nyinyi ni watu wa ajabu sana katika ulimwengu wa kibiashara.
 
Hili tatizo la saini liliwahi kunikuta kadi yangu iliisha muda wake nikatakiwa kuihuhisha. Nikatekeleza hilo. Wakati nasubiri nikawanachukulia fedha ndani Bwana wee nilipokuwa nasaini Marazote niliambiwa saini haifanani na iliyomo kwenye kumbukumbu zao. nilikoma Kila siku naoneshwa meneja. kadi yenyewe inasubiriwa kuletwa dar kutoka tabora nikaona isiwe tabu nikaikausha akaunti na kuachana nayo Huu mwaka wa 4

Sent using Jamii Forums mobile app
 
CRDB wameongeza makato balaa yaan duh ngoja nihamie NMB
 
CRDB wameongeza makato balaa yaan duh ngoja nihamie NMB
Kilichotokea ni NMB wamewaingiza wenzao mkenge maana mwanzon mwa mwaka huu walitangaza ongezeko baadae kidògo nào CRDB wakatangaza ongezeko pia na sasa NMB wamepunguza hizo tozo, tunasubiri sasa kwa CRDB watafanyaje nao
 
Juzi nimesoma comment mmesema umefita gharama za kutoa fedha, kuhamisha fedha, gharama za kumiliki akaunti kila mwezi lakini sio kweli kwanini mnadanganya umma?

Ukisoma gazeti la mwananchi la Leo tarehe 30/01/2019 yenye kichwa Cha habari minimus disclosure of bank charges and fees hakuna Cha bure kwa mfano

1. Maintainance fee ni 1900 kabla ya vat Hadi

2. Statement shs 3,900 Hadi 212,400 kabla ya vat

3. Kutoa fedha shs 4,012 Hadi 120,000

4. Kufunga akaunti shs 9,440

Ukweli wenu ni Upi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…