NMB mefikia hatua mbaya, Huduma zenu mbaya mbaya sana...

Dr. Ndimu

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2012
Posts
717
Reaction score
146
Nashindwa kuwaelewa ndugu zangu wa NMB, wakati huu wa kukua kwa teknolojia wao ndio wanarudi nyuma kwa kasi hususan kwa huduma zao za mobile, huwezi kuwa na hakika ukiaccess akaunti yako kwa simu na kufanya Transaction, iwe kuhamisha pesa katika akaunti ingine, kutuma katika M pesa ama hata Pesa fasta, mara nyingi zilizojaribu ama hela ilichelewa sana kufika ama haikufika nilikotuma na hakuna taarifa yeyote niliyopewa na hii ni zaidi ya mara kumi.
kwa hivi karibuni tatizo limezidi kuwa kubwa na wikii hii nlijaribu mara mbili kutumia huduma yao ya Pesa Fasta baada ya kuona ile ya kuhamisha katika Mpesa imezingua na mara zote Pesa ilienda nilikotuma lakini hakuweza kuchukua eti mtandao unasumbua na nilijua hilo baada ya kupiga simu customer service na kusubiri kwa dakika 16 kabla ya kuunganishwa na mtoa huduma ikiwa ni mara karibu ya 20 ya kujaribu na simu kupata connection, hata hivyo jibu lenyewe nililipata kwa lugha ya dharau kama nlikuwa nawaomba msaada wakati wao ndio walikuwa wamesababisha usumbufu bila hata kutoa taarifa.
kilichonichefua hasa ni kupata sms yao ikinisisitizia kutumia huduma hizo zote ili kufurahia huduma zao na kujisahaulisha nkajaribu pia kutuma hela kwa wazazi kwa PESA FASTA, hadi naadika hapa pamoja na kufika katika simu zao ila toka jana hawajaweza kutoa na wanaambiwa wasubiri baada ya siku tatu itarudi kwangu then nijaribu kutuma tena,wako sereous kweli hawa watu?watarudisha gharama nilizotumia kutuma?
 
Malalamiko ya wateja kuhusu huduma za ki-bank hapa nchini yamekuwa mengi sana,nadhani siku hizi wanaoajiriwa ni vibaka.Mtu yuko pale kupiga ma-deal.Pole sana mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…