NMB msipokuwa mna wateja wengi ila maafisa mikopo wanawaharibia soko.

NMB msipokuwa mna wateja wengi ila maafisa mikopo wanawaharibia soko.

ndege joni

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
682
Reaction score
1,108
Sitaki kuongea sana ila mimi ni mtumishi wa umma, niliomba mkopo kwa ajili ya dharura ya kifamilia mwezi umepita. Nilifuata taratibu zote ila baada ya kila kitu kufanyika na makato kuingizwa kwenye mfumo na afisa utumishi.... form zilirudi kwa afisa mikopo. Cha ajabu tangu form zirudi kutoka utumishi ni wiki 3 na sijaona hako kamkopo na sikahitaji kwa sasa kwa sababu nimeshatatua tatizo langu. Najiuliza, hivi hawa maafisa mikopo kibiri hiki wanakitoa wapi? Pale ofisini ukienda mara nyingi hawapo wakati kazi yao ni kutoa mikopo... wanakuwa wapi? Kama wanataka rushwa si waseme tutoe? Nilimpigia simu mara nyingi hajawahi kupokea na kunujibu sms zangu. Kosa langu ni kuomba mkopo kwao? Kwamba hakuna taasisi nyingine za kukopesha?
 
Pole mkuu.kweli wamekukwaza mpaka unawafungulia uzi mida hii
 
Hii kadhia hata mimi imenikuta hadi nikagombana naye unakuta afisa mikopo kanuna hata hacheki sasa unajiuliza au anaona wivu mimi kuchukua pesa
 
Mi tayari nina mkopo,nilitaka ku top up,lakini figisu nyiingi nimeamua nitafute njia nyingine kupata pesa hiyo.
 
Sielewi hii kazi wanapeana kindugu au wanafata taratibu. Bora angeniambia ntachelewa kupata nijue nafanyaje sio kuniweka zaidi ya mwezi. Nafikiri kibiashara inazorotesha mapato yao
 
Back
Top Bottom