Mkuu Lekanjobe Kubinika na wengine,
NMB baada ya kuuza hisa zake kwenye soko la msingi(primary market) through Initial Public Offer walizipeleka hisa kwenye soko la hisa la Dar-es-Salaam (secondary market).
Kama unavyosema, ni kweli share zilikuwa oversubscribed,kwa hivyo walionunua hisa zaidi ya kiwango kilichotengwa walirudishiwa pesa zao,kumbuka kwenye Initial Public Offer kila hisa iliuzwa kwa shilingi 600,lakini ziliendelea kupanda bei mpaka ziliwahi kufika Tshs1200,ingawa baadae zilishuka mpaka kufikia Tsh730,nilipoangalia mara ya mwisho zilikuwa Tsh 830.
Kuhusu gawio(Divident) walishawahi kutoa kila share Tsh30,kwa hiyo kwa ujumla NMB wanafanya vizuri kutokana na mwenendo wa soko la hisa la Dar-es-Salaam,nasema hivi kwa sababu ukilinganisha na hisa za CRDB ambayo toka hisa zimeingia sokoni hazijawahi kupanda hata siku moja na badala yake zimeendelea kushuka,ziliingia sokoni zikiwa Tsh200 kama sikosei ,lakini siku ya mwisho kuangalia zilikuwa zimeporomoka mpaka kufikia Tshs 130 kwa hisa ,na hawa wamewahi kutoa gawio ilikuwa shs 2 kila hisa.
Kingine NMB kutoa misaada kwenye soka na sehemu nyingine siyo kuharibu pesa,isipokuwa hiyo ni corporate strategy ambapo inafaida nyingi,lakini nitataja mbili tu kwa sasa,
1.Inacreate public awareness(kwa hiyo ni kama inafanya matangazo na promotion ya biashara hasa ukizingatia banking industry inaushindani mkubwa sana Tanzania at this particular momment).
2.Inatimiza wajibu wake kwa jamii(Corporate social responsibility),kwa kuwarudishia kidogo kati ya michango yao mingi waliyoitoa kwa NMB kwa kufanya biashara nao,kama kufungua account,kuchukua mikopo, kusafirisha pesa nk