Habari yako ndugu,
Kikawaida Claim status, huwa ziko katika mfuatano huu :- PENDING, LODGED, APPROVED, NA PAID.
PENDING - Ni kwamba faili lako linasubiri kufanyiwa kazi na maofisa wa mafao.
LODGED - Ni kwamba faili lako limewafikia mikononi na wameanza kulifanyia kazi.
APPROVED - Ni kwamba maombi yako yamekubaliwa na yanasubiri kulipwa.
PAID - Ni kwamba maombi yako yameshalipwa.
Mara nyingi mchakato wa baada ya maombi mpaka kulipwa huwa unachukua wiki sita kwa wale wa FAO LA WASIOKUWA NA AJIRA asilimia 33% au wale unskilled labour ambao hufanya kazi kazi ktk miradi mbalimbali.